Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Nasikitika kusema bado unakwepa kujibu swali Mkuu.
Kama unalijua jibu naomba uniambie/utuambie.
Kama haujui jibu pia naomba uniambie/utuambie.
Jibu nalijua, lipo ndani ya lile swali ambalo umelikwepa

Unakubali kua SNDANGUJA yupo?
 
Madhara makubwa yaliyotokea baada ya uharibifu(dhambi) kuingia duniani kumesababishwa na kiumbe binadamu mwenyewe ikiratibiwa na mpango kazi wa shetani
Nashukuru, Najifunza; Ila bado Nina maswali hapa; Kwanini Mungu Aruhusu Distortion; Yeye ni muweza wa Yote(Ikiwemo hata uwezo wa kuzuia uharibifu)
Inamaana Sisi wanadamu ambao ametuumba tuna uwezo Mkubwa zaidi yake? Kwamba yeye ametutengeneza kamili sisi tumeweza kupinga uwezo wake wa kutukamilisha na kuamua kujiingizia uharibifu.

Inatia mashaka kwa mimi ninayemwamini uwepo wake; Huku kukiwa na Maswali mengi sana, maumivu mengi, vurugu nyingi ambayo yako ndani ya uwezo wake kutoa Suluhisho; Hata kama sisi wanadamu ndio tumeleta, Naamini kwa uwezo wake ambao tumekuwa tukijifunza, bado yuko kwenye nafasi na uwezo wa Kuondoa kuliko sasa ivi machafuko duniani yanazidi watu wanauana; Anashindwa Kuzuia hawa waharibifu kwa njia iliyo nzuri na kuhakikisha uharibifu hautokei? Hatufiwi na wapendwa wetu? Imagine tu Rais wetu amefariki juzi kati wengi walimlilia? ivi kweli Haoni maumivu ya watu achilia mbali taifa; Familia yake je? Walipenda kuendelea kuwa naye, lakini inasemekana Mungu amemchukua? Sasa kulikuwa n haja gani anatuumba then anatuchukua? tena wengine wanachukuliwa akiwa na miaka michache sana? wengine wakati wa kuzaliwa wanakufa? Kweli kaka huwa napata shida sana kwenye kuamini kwangu.

Kuna kitu natamani nikielewe hapo ili kuondoa mashaka;
 
MWISHO, mkuu aonavyo Mungu au atakavyo yeye kifanyike au kisifanyike kitabaki kuwa ni maamuzi yake yeye mwenyewe
Hapa ndipo Mashaka yananijaa; hata nikisiaga Wahubiri wanasema; Ivi Kwanini aamue tu vyoyote? hata vitu vinavyoumiza aliotuumba yeye mwenyewe? Believe me Hii mijadala imekuja kwasababu kumekuwa na side mbili tangu mwanzo; Kama Mungu ahata anguko angelizuia; Kusingekuwa na Mtu wa kuwaza kinyume maana angezuia pia watu kuwaza kinyume, Asingekuwepo mtu mingoni mwetu anyewaza kuuwa mtu, Infact hata ukimuua Mtu hafi etc. Maswali haya nimekuwa nikijiuliza sana; Ivi kweli Binadamu wote tunajua kwamba tunahitaji kuwa na wapendwa wetu wanafariki wengine wakiwa na Umri mdogo sana, Wanatoweka Duniani ili hali iko katika uweza wa Mungu kuwafanya waendelee kuwa nasi? Je Mungu yeye anapenda Huzuni yetu? anapenda kutuona sisi tunahuzunika kwa kupoteza watu ambao tunawapenda? Kwa kuruhusu watu wa taifa moja kupigana na kuuwa watu wa taifa jingine; kitu ambacho si kizuri, na kwa uwezo wake ambao nimefundishwa anaweza kuzuia lakini hafanya hivyo, hapa ndipo wakati mwigne napata mashaka ndugu; How comes mambo mabaya yaje asizuie? Dini kadhaa wa kadhaa zinapingana kuhusu tabia za Mungu, kwanini asifanaye namna kwamba Watu wote tumwelewe bila support ya Dini? kiasi kwamba Tunadanganywa kwamba Mungu yupo ivi au Yupo vile; Kweli napata shida
 
Kama kutumia theories za watu ni kitu kibaya, mbona wewe unatumia alphabet ya watu, hujatunga yako?
Prove kwanza kwamba 'time is illusion' na tunaposema 'the earth is estimated to be 4.54 billion years old, plus or minus about 50 million years' ni nini hiki? How about seconds, minutes, hours, days, weeks, months and years we use? Are these mere illusions, aren't they? Then, why do we use them to measure the duration of a particular event or situation?
 
Wewe unayekataa kutumia theories za watu, kwanza andika maswali yako kwa alphabet yako uliyoitunga wewe mwenyewe, halafu uyatume kwenye internet yako ya mabua uliyoigundua mwenyewe.

Hapo nitajua kweli hutaki theories za watu.

Kabla ya hapo utakuwa unajishaua tu kwa maneno usiyoyajua mwanzo wala mwisho, na kuji contradict kila sehemu.

Wewe hutaki theories za watu, unajua hayo maandishi unayotumia ni theories za watu?
 
Utawezaje kumwelewa bila support ya Dini ?
Kaka Mungu ni muweza wa yote; Je anahitaji Dini imsaidie ili sisi watu wake tumuelewe? Uweza wake uko kwenye kitu gani hasa kama anahitaji dini ili watu wamjue? Yaani kwa nilivyofundishwa uweza wake, naamini kabisa kwamba angeweza Kuwafanya watu wamjue bila support ya Dini..!! Hapa ndipo Mashaka yanaingia ndugu yangu; Wewe unachotakiwa ni kunieleweshe.
 
Moja ya sababu ya kuamua kueneza ukuu wake kupitia dini ni ili tumuabudu..
Sawa Ndugu ngoja nikubaliane na wewe kwa sasa huku nikiendelea kujifunza; Je Dini gani sasa ili mtu aifahamu kwamba hii ndio inmuelezea Mungu kwa usahihi? Maana Dini zote zinashutumiana tena shutuma zinatoka kwa Viongozi ambao zinaambukizwa kwa waamini na kuwashambulia watu wengine; Huku kila Mtu akijinasibu kwamba Dini yake iko sawa; Huoni hapo pia kutakuwa na ukakasi wa Mtu kumuelewa? Mchanganyiko wote wa Dini hizi na madhehebu mbali mbali kwa kila dini, Huoni kama mtu amepewa challnge ya kuchagua Dini ambayo itamsaidia kumueleza Mungu vizuri? Mtu lazima afahamu vigezo?

Kama ambavyo Mtoto huwa afundishwi kunyonya anapozaliwa, Kuangalia, kulia, kucheka etc; Kumekuwa na Ugumu gani kwa Mungu kufanya utaratibu Mtu amjue automatic..?? Ushahidi wa kwamba yeye ni muweza wa yote ni upi?
 
1. Mimi naikubali sayansi na nakubali pia imani watu waliyonayo juu ya kuwepo kwa Mungu.
2. Wewe umekuwa ukidai wanaoamini kuwepo kwa Mungu wathibitishe kisayansi kuwa Mungu yupo.
3. Mimi nimekuwa nikisema kwamba sayansi haiwezi kuthibitisha kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu, isipokuwa kuwepo kwa Mungu kunaweza kuthibitishwaa na disciplines zingine kama natural theology au metaphysics.
4. Wewe umekuwa ukidai kuwa ukikomalia methodolojia ya kisayansi ku'prove' kuwepo kwa Mungu.
5. Ndiyo maana na mimi baadaye nimesema sasa na wewe uthibitishe hizo theories za wanasayansi kama Einstein juu ya general au special relativity. Hapa ndipo tumeshindwana - maana wewe unataka mimi ni'prove', lakini wewe hutaki ku'prove' na badala yake umekuwa ukitumia maneno kama 'upumbavu', 'ujinga', 'ngumbaru wewe','obstructionist bullshit' etc - yote haya ni ushahidi wa kuishiwa/kutoweza kujenga hoja kwa sababu siyo sehemu ya mjadala.
 
Hio ni baadhi ya mitihani ya Mola
Mambo kama haya ndio yanafanya ukakasi kwangu uwepo; Mtihani ni kitu kinachowekwa kwa kusudi la Kumjaribu Mtu/ kumpima uwezo wake kwenye jambo fulani; Ina maana Mungu hatujui Sisi watu wake kiasi cha kutaka kutujaribu kwanza ndipoa tujue? Wakati huo huo nimefundishwa kwamba Mungu anajua yote, naweza yote Je anashindwa kujua kwamba akinipa hili Nitaweza hili sitaweza? Tena unamjaribu vipi tena hata kwa mabaya? na ikitokea ameshindwa majaribu basi unamuadhibu? Huoni huu utakuwa ni uonevu.

Ninachoomba nitoe Ukakasi ili nisiwe na mashaka kama ambavyo nimekuwa nayo.
 
Unaikubali vipi sayansi bila kukubali theories za watu?
 
Unajua kwamba experience ni personal?,sio lazima experience yako iwe sawa na ya wengine?.
 
Kwahiyo kwasabu wewe "Mungu " amekusaidia,basi "Mungu " yupo?,vipi ambao hawajasaidiwa?
 
Hapo Qur'aan imesema au imeuliza swali?
 
Lazima uthibitishe kwa namna ambayo kila mtu anaweza kuelewa."Ukithibitisha" kwa namna unayoelewa wewe tu,watu wengine wataelewaje?
 
Kwahiyo kwasabu wewe "Mungu " amekusaidia,basi "Mungu " yupo?,vipi ambao hawajasaidiwa?
Hata sayansi kuna watu haijawasaidia. Mfano, watu wengi wanaougua kansa au hata magonjwa kama kisukari, TB, malaria nk. Je, unaweza kusema waliopoteza maisha huku wakitibiwa na kutegemea kupona sayansi imewasaidia? Je, kusema sayansi haijawasaidia (kwa mfano) ina maana kwamba sayansi haisaidii?
 
Unajua kwamba experience ni personal?,sio lazima experience yako iwe sawa na ya wengine?.
Sijasema kama experience yangu ni wengine pia. Hiyo ni starting point tu kwamba kila mmoja wetu ana experience fulani katika maisha yake.
 
Lazima uthibitishe kwa namna ambayo kila mtu anaweza kuelewa."Ukithibitisha" kwa namna unayoelewa wewe tu,watu wengine wataelewaje?
Wewe ni vitu vingapi umeweza kuthibitisha 'kwa namna ambayo kila mtu anaweza kuelewa'? Mfano, thibitisha kwamba from nothing then the universe became.
 
Mkuu maelezo yako yote ambayo yame-base kwenye kuhoji matokeo ya dhambi na madhara mbalimbali, nimeyajibu vizuri, Dhambi ndio imepelekea anguko la binadamu na kusababisha hayo yoote.

Baada ya binadamu kuasi maagizo ya Mungu, ilipelekea anguko lake. Binadamu aliambiwa usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya maana ukila utakufa. Binadamu akaasi na kula, dhambi ikaingia kizazi cha binadamu na matokeo yake ndo mpaka leo.

So Mungu hana kosa, then majibu ya maswali ya ulimwengu ulipotoka, ulipo sasa hivi na hatima ya ulimwengu baadae, kila kitu kipo wazi.
 
Kila unachokiona kipo na kinatokea ni ushahidi wa kwamba Mola ni muweza wa yote.
Unaweza kunisaidia Dini moja wapo ambayo Itaniongoza vyema kuhusu Mungu; Kama kweli unataka kunisaidia ili nianze kusoma na kuchambua kutoka kwenye hiyo Dini? Maana sasa kwa namna ilivyo Mungu kutuachia sisi Tuchambue, dini ipi nzuri ya kumjua, wakati dini almost nyingi zinamuelezea kwa namna tofauti, wakati huo huo ukikosea Dini anaenda kukuadhibu huoni hapo Kuna uonevu? Mungu aliyetufanya kutupa Akili, na logic kwanini asizuie mkanganyiko? kusema kwamba Anachoamua yeye ndio sahihi, unahisi Ni mwenye upendo, mwenye haki kama ambavyo tumekuwa tukifundishwa? Nia yangu nifike mahali nitoe shaka niliyonayo juu yake. usione nakusumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…