Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

UMEWAHI KUJIULIZA VIPI KAMA WANGELITII HILO KATAZO NA WASINGEKULA MATUNDA YA MTI HUO KUNGEKUA NA HAYA MATATIZO?
Haya Nimeshajiuliza, kama wasingeliasi katazo hilo mambo haya yote yasingekuwepo

Sasa namimi nikuulize tu na unijibu, Ushawahi kujiuliza kama Mungu asingeweka hiyo Option? (Zingatia kwamba ana uwezo wa kila kitu)
 
Mkuu, usitafute kuchagua dini gani, tafuta kumtii Mungu na kutotenda dhambi.
Tafadhali nisaidie namna Gani naweza Kumtii Mungu Nje Dini? Yaan najuaje kwamba hivi ndo Kumtii Mungu? Na hayo maelekezo Mungu ameyaweka wapi? Ukifanya Hivyo itakuwa msaada kwangu, lakini pia naamini wengine wana Challenge kama yangu hapa
 
Haya Nimeshajiuliza, kama wasingeliasi katazo hilo mambo haya yote yasingekuwepo

Sasa namimi nikuulize tu na unijibu, Ushawahi kujiuliza kama Mungu asingeweka hiyo Option? (Zingatia kwamba ana uwezo wa kila kitu)
Vipi kama kuwepo kwa hiyo option pia kulikua na lengo kubwa jema nyingine ambalo Mungu aliikusudia?

Ambalo hilo lengo/ kusudi binadamu aliharibu kwa kukiuka maagizo ya Mungu.
 
Tafadhali nisaidie namna Gani naweza Kumtii Mungu Nje Dini? Yaan najuaje kwamba hivi ndo Kumtii Mungu? Na hayo maelekezo Mungu ameyaweka wapi? Ukifanya Hivyo itakuwa msaada kwangu, lakini pia naamini wengine wana Challenge kama yangu hapa
Usijifunge katika dini, Mungu hakuumba dini aliumba binadamu watawale vitu vyote alivyoviumba duniani na wamwabudu yeye Mungu.

Binadamu wakaasi, wakatawanyika kwa namna tofauti na kufuata upotevu wao.

Hayo maelekezo alipoyaweka upo tayari nikuelekeze yalipo?
 
Jibu lako hili bado halijanipa formation ya vitu vilitokeaje, katika ulimwengu huu ulio limited to time, space and matter kila kitu ni lazima kiwe kimeundwa na muundaji, vitu nilivyokuuliza kwenye post #584 bado haujanipa formation ya hivyo vitu mkuu.
 
Kwa u athest wangu mtazamo wangu juu ya dunia na vilivyomo huwa nina majibu mawili ya aidha ilianza ama haikuanza,sina uhakika.

Mtu akiniambia haikuanza huwa naomba uthibitisho wa huo uhakika wake,

Na pia mtu mwingine akiniambia dunia na vilivyomo vilianza huwa naomba uthibitisho wa huo uhakika wake wa kwamba ilianza,

Sasa ili swali lako liwe na mantiki unaweza kutuwekea hapa uthibitisho wa kwamba vitu hivyo ulivyovitaja vina chanzo ili tuanze kumtafuta huyo mwanzilishi?

Maana wewe inaonekana una uhakika wakati wengine bado tuko njiapanda ya kuanza ama kutoanza.

Tuhakikishie kwanza kuwa vyote hivyo vilianza na si kinyume chake kisha tumsake mwanzilishi.
 
Aliyesema asilimia 90 ya Wakatoliki ni Atheists, ni kweli, chukua kamfano kadogo, unaambiwa usiowe au kuolewa ili ufanye kazi ya Mungu unakubali, hata tendo la ndoa unakubali ni dhambi . Mungu alipomuumba Eva alimaanisha nini? Wewe unaenda kinyume na Mungu. Huenda Ukatoliki ni dili la nguvu hapa duniani. Kapalizwa Bikira Maria, jibu ni "ndio mzee" ni uuuuuuuungwana?
 
Wadau, vipi kiranga ametoa jibu la formation ya vitu kwenye post #584?

Au ameendelea kuliweka kwenye ignore list? Na hata kama halijui kwanini hataki kutuambia kwamba halijui? Na kama analijua kwanini
hatupi majibu?
Unajitungisha swali na kujiwekea mipaka halafu unataka upewe majibu? Leta ushahidi kwanza wa kwamba hivyo vitu viliumbwa ndiyo tusake jibu la huyo muumbaji.

Kuendelea kung'ang'ana swali ambalo kwanza hata msingi wake huna uhakika nao ni kupotezea muda watu.

Unaposema Ulimwengu upo limited kwenye time,matter and space una uhakika upi?
Na unaweza tuthibitishia kuwa Mungu wenu yuko beyond time, space na matter?

Ukitolea ufafanuzi haya basi swali lako litakuwa valid kupatiwa majibu.
 
Ulichoandika hiki sicho ulichoulizwa,

Umeambiwa hivi;Baba mzuri ni yule anayeweka options zilizo njema kwa watoto wake,

Kisha ukaulizwa; kwa nini Mungu aweke option ya Mti wa mabaya wakati uwezo wa kutouweka kabisa alikuwa nao?
Inamaana kwa ujuzi wake wa mpaka yajayo hakujua kuwa option hiyo hao viumbe wake watafeli na kuleta shida kiasi cha kuanza kusumbuka kuleta tena Mkombozi aje awafie?

Ama alijua italeta shida Ila akaamua aache ili baadae aje ajisumbue tena kuleta wokovu?
Kama ndivyo,inamaana huyo Mungu wenu hana kazi zingine za kufanya zenye tija zaidi kuliko huu utoto anaoufanya?
 
Tatizo la Atheists wao wameshapitisha kuwa misimamo yao ni sahihi hivyo wao kazi yao ni kuhoji na kukosoa wengine sasa ikitokea ukawa challenge wao na hiyo misimamo unawavuruga hawakuelewi.
 
Akili za Kiranga hazichunguziki mkuu, huyu ni miongoni mwa watu wenye uelewa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kuelezea mambo kwa marefu na mapana, huku yote yakiwa kwa ufasaha.
Ni akili za Mungu PEKEE ambazo hazichunguziki. Acheni kukufuru. Ninyi ndiyo mnamchukiza Mungu hadi anatuletea mapigo.
 
Ukristo haujibu maswali tata kuhuusu MUNGU. Ndio maana wengi wao wanakuwa hawana dini.kama saiz ulaya wengi hawasali wameonani ujinga
 
Its understandable for Catholics to doubt presence of God at times,Christianity has always go hand in hand with miracles and you will never see that in Catholic churches nowdays.But miracles are real in church of christ and are happening everyday but not in our Catholic churches.
 
Ukristo haujibu maswali tata kuhuusu MUNGU. Ndio maana wengi wao wanakuwa hawana dini.kama saiz ulaya wengi hawasali wameonani ujinga
Sio kweli,infact ukristu ndo umejibu maswali mengi zaidi kuhusu Mungu,yasiyojibika kwenye ukristu basi hakuna ambaye ana majibu yake
 
Lengo la Mungu kuweka mti wa mabaya as well lilikuwa ni kumruhusu mwanadamu ku-exercise freewill,Mungu anataka kuabudiwa,kupendwa kusifiwa lakini iwe ni choice.Mungu hakutaka binadamu awe Robot na sifa kubwa zaidi ya Binadamu ni kuwa na free will.Sasa kama pasingekuwa na choice tungesemaje tunampenda Mungu?Na upendo wake unajidhihirisha pale kati ya option nyingi sana zisizokuwepo mti wa mabaya ulikuwa mmoja tu kati ya mingi ya mema but still binadamu tukayeyusha.
 
Kama ameweka machaguo,kwanini Sasa aweke adhabu? Wakati ametaka watu wachague wanachokitaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…