Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Sasa mbona umekurupuka kuanza kusema Mungu ni dhana badala ya kueleza kwanza Mungu ni kitu gani?
 
Mbona nimekujibu kua ni kitu cha kufikirika
Mimi sijauliza kama ni kitu cha kufikirika au ni kitu halisi? vitu vya kufikirika vipo vingi mkuu ndio maana nikauliza Mungu ni nini sasa ukisema tu ni kitu cha kufikirika mimi nitawezaje kujua ni kitu gani Mungu katika vitu vingi vya kufikirika vilivyopo?
 
Kwani nani kasema umeuliza swali la multiple choice kati ya kuchagua kufikiria au uhalisia kiasi cha mimi kukupa jibu useme hujaniuliza kama ni kitu cha kufikirika au ni halisi?
 
Mi naona wewe ndio unashida samahani lakini... Kiranga anaamini kwamba mungu ni “dhana” tu maana yake ni fikra tu za watu sasa hawa watu wanatofautiana kwenye hizi fikra unapomwambia aelezee hiyo dhana itambidi aende India akawaulize dhana kuhusu Krishna aende arabuni akawaulize kuhusu Allah ... swali lako ni General sana ...kama unataka kupata jibu uliza moja kwa moja
 
Swali la Mungu ni nani au ni nini uliza mtu anaeabudu mana kila mtu ana mtazamo wake kuhusu MUNGU wake.
 
Ushasema Mungu ni dhana na ndio umetaka tuelewe hivyo sasa ukianza tena habari za sijui Mungu huyu na wale unakuwa unanichanganya, mimi naelewa Mungu ni dhana basi sielewi lengine zaidi ya hapo.
Dhana kwa sababu ni fikra kila mtu anaya kwake ikitokea zinafanana ndio jumuiya za kiimani zinazaliwa ... uliza swali vizuri
 
Swali la Mungu ni nani au ni nini uliza mtu anaeabudu mana kila mtu ana mtazamo wake kuhusu MUNGU wake.
Mimi namuuliza mtu ambaye anasema hakuna Mungu, sasa ni yeye ndio ataeleza kwa mtazamo wake Mungu ni nini ambaye yeye anasema hayupo. Kwahiyo hakuna kilichoharibika.
 
Dhana kwa sababu ni fikra kila mtu anaya kwake ikitokea zinafanana ndio jumuiya za kiimani zinazaliwa ... uliza swali vizuri
Ni fikra kila mtu anayo ya kwake, sasa neno Mungu linaingiaje hapo kwenye hizo fikra tofautitofauti za watu? hapo ndipo napotaka kujua maana ya Mungu ni nini?
 
Yeye amesema kiujumla kuwa Mungu ni dhana, sasa kabla ya kujadili Allah au Krishna kwanza lazima uijue hiyo dhana ya Mungu ni nini ndipo tuje hilo la Allah na Krishna, usipojua dhana ya Mungu ni ipi hutoelewa ni nini kinakusudiwa ukisikia Mungu Allah au Krishna.
 
Kwani nani kasema umeuliza swali la multiple choice kati ya kuchagua kufikiria au uhalisia kiasi cha mimi kukupa jibu useme hujaniuliza kama ni kitu cha kufikirika au ni halisi?
Nataka kujua meli ndio nini unaniambia ni chombo cha usafiri,sasa vyombo vya usafiri viko vingi kuna gari kuna treni kuna pikipiki kuna ndege. Hivyo vyote ni vyombo vya usafiri ila ni vitu tofauti vina sifa tofauti.
 
Kwa point hiyo mtu huyo anakua amekubali kua meli ni chombo cha usafiri ila anataka kujua usafiri wa aina gani si ndiyo, ok kwa situation hii nadhani angeambiwa ni chombo cha usafiri wa majini angeelewa, nadhani ndo ilikua point yako

So kwa mfano huo tukija kwenye hoja yangu ni kwamba wewe unakubali kua mungu ni dhana ya kufikirika haipo katika uhalisia ila unataka mimi nikuambie ipo katika category gani sindiyo?
 
Hakuna aina moja ya chombo cha usafiri majini,kuna boat ambayo ni tofauti na Meli na kuna mtumbwi ambao ni tofauti na nyambizi.

Hivyo vyote vina sifa tofauti na mwenzie ingawa ni vyombo vya usafiri wa majini.
 
Ni fikra kila mtu anayo ya kwake, sasa neno Mungu linaingiaje hapo kwenye hizo fikra tofautitofauti za watu? hapo ndipo napotaka kujua maana ya Mungu ni nini?
Ukiulizwa john ni nani we utatoa jibu gani mana kina-john wako wengi
 
Sasa swali lilitakiwa liwe hivi ... kwa jinsi ya uelewa wako embu nielezee dhana ya ki-mungu.
 
Huenda alishapiga Philosophy na Theology, akaamua kuacha. Philosophy inamsaidia kuchambua mambo.
 
Swali duniani kila jamii inamiungu wake na kila jamii inasema miungu wake ndio sahii , tuzungumzie miungu hii mitatu jehova ,yssu and allah wote hawa wamesema kuna siku ya mwisho je kama wakitofautiana kuita siku ya mwisho yani kila mmoja amepanga siku yake tofauti itakuwaje. Nani atakuwa sahihi
 
Hata kama kila mtu ataamua kuamini Mungu wake peke yake hiyo ndio imani ilivyo hakuna limit na kila mmoja ana haki ya kuona anachoamini ndio sahihi na ndio maana akaamini, japo haiwezekani wote wakawa sahihi.

Ukielewa imani ni nini huwezi kuuliza hivyo ulivyouliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…