Hoja yangu ninayokuambia umeshaielewa ila unajaribu kuzungusha maneno. Anyway
Majibu yako unayoyatoa ni ya kufikirika yaan kwa mfano unasema "Bahari imesababishwa na miamba na wingu lenye dust"
Sasa ndo nakuuliza hii miamba na wingu lenye dust vimetokea wapi? Kwanza pia uniambie vimesababishaje Bahari.
Usiponipa ufafanuzi huo wa hiyo miamba na wingu lenye dust vimetokea wapi jibu lako hilo ni la kufikirika halina uhakikisho wa kisayansi.
Kwanini?
Kwa sababu hilo wingu lenye dust na miamba vimetokea tu gafla(bila kuniambia vimetokea wapi? Formation zake) scientifically. Hii ina maana vimetokea kimiujiza yaan hata sayansi yenyewe inashindwa kuprove vimetokeaje? Na sayansi ikishindwa kuprove vimetokeaje, ni sawa na hivyo vitu vilikua formed na Mungu kwa uwezo wake na miujiza yake.
RUDIA TENA HAPA KUSOMA (Nimeuliza kwenye majibu yako ya kufikirika)
Unasema Sayari zimetokana na Nebula,
Nebula ni Matter niambie hii Nebula imetokea wapi? Formation yake kisayansi, imeform vipi sayari zote?, Au Nebula imetokea tu kimiujiza? Ukisema Nebula imeform sayari bila kuniambia Nebula ilitokea wapi kwanza, huo utakua ni muujiza na sio sayansi.
Niambie hiyo Nebula ilitokea wapi?(formation) yake, imeform vipi Sayari zote?
Niambie hilo wingu kubwa lenye dust na miamba imetokea wapi? (formation) zake au zilitokea tu kimiujiza? Ukiniambia bahari imetokana na wingu kubwa lenye dust na miamba bila kuniambia hiyo miamba na wingu lenye dust vimetokeaje (formation) scientifically huo utakua ni muujiza kitu ambacho nyie hamuamini katika muujiza.
Niambie hiyo miamba na wingu lenye dust formation yake, vimetokea vipi na vimeform vipi bahari, mito na maziwa yote? Kisayansi.
Kama gesi na mafuta husababishwa na mabaki ya mimea na wanyama waliokufa miaka mingi, nipe kwanza formation ya mimea na hao wanyama walitokea vipi?(formation) na wameform vipi gesi na mafuta kisayansi.
Kama samaki wametokana na maji, niambie hayo maji yametokeaje(formation) yake na yameform vipi samaki wa aina zote? Hayo maji yalikuwepo tu kimiujiza?
Uniambie theropods imetokeaje vipi(formation), au imetokea tu kimiujiza? Niambie kisayansi theropods imetokea vipi na imeform vipi Ndege wa aina zote?
Kama wanyama wame evolve kutoka tiktaalik, niambie tiktaalik imetokea vipi(formation) au imetokea tu kimiujiza? Kusikojulikana. Imeform vipi wanyama wa aina zote kisayansi.
Niambie formation ya binadamu wametokea vipi?
Uniambie hayo maji yametokea vipi(formation) yake na yameform vipi miti na mimea ya aina zote yalio baharini, mito maziwa na nchi kavu. Usiniambie miti imetokana na maji bila kuniambia maji kwanza yalitokeaje? na yameform vipi miti na mimea kisayansi.
NB: Bado nasubiria majibu. Mfano:- Nakukumbusha ukiniambia JUICE YA PARACHICHI IMETOKANA NA MAJI, TUNDA PARACHICHI NA SUKARI, NITAKUOMBA UNIAMBIE KWANZA(Formation) ya PARACHICHI LIMETOKA WAPI, MAJI YAMETOKA WAPI NA SUKARI, JE VIMETOKEA TU KIMIUJIZA? Uniambie kisayansi vimetoka wapi kwanza, alafu ndio uniambie process iliyotumika kuform juice ya parachichi