Inaonekana Kiranga ni mtu mmoja ambaye hakuwa na hatia yoyote, Lakini alipitia mambo Fulani magumu, Wakristo mnayaita majaribu, Kuanzia hiyo siku hadi sasa kapoteza Imani kwa mungu,, Unajua duniani watu wanapitia shida tofauti tofauti, Anyway sio kosa la Kiranga kutokumuamini Mungu Ila ni mazingira aliyopitia
Speculation.
Mambo magumu gani, umejuaje, unaweza kuthibitishaje hilo?
Mimi napinga uwepo wa Mungu kwa kuangalia logical fallacies na contradictions katika dhana ya kuwepo Mungu.
Si kwa sababu ya matatizo ya maisha.
Kama tunaangalia matatizo ya maisha, kwa maana ya kwamba maisha mazuri kwangu binafsi yameletwa na Mungu nilitakiwa kumkubali sana Mungu.
Kwa sababu. Nimepata neema tangu nipo tumboni mwa mama yangu.
Nimeanza kutembea corridors za Ikulu ya Nyerere Tanzania tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu. Nimekula ma apple ya Mama Joan Wicken.
Nimepelekwa shule na Chauffeur driven Range Rover Classic Vogue 4.0. na Landcruiser VX, Mercedes Benz, Pajero Intercooler Turbo among other luxury SUVs.Nimekaa na kukulia mitaa ya washefa Tanzania, nimeenda kusoma New York City Marekani, nikafanya kazi Wall St. na washefa wa dunia, weekend tunaenda Reykjavik. Just for the weekend. Nina biashara nzuri tu za kupoteza $25,000 kwa siku, na kuzirudisha maradufu. Naendesha ndinga kali, nabadilisha Beemers kama miwani, nina kila kitu Mtanzania wa kawaida anachokitafuta.
Tena nimewapa shavu machizi wangu wako poa, na wakiwa na shida wanajua napiga tafu sana tu. Wengine wako hapahapa JF hata sikuwajua kivile tumetick tu tumesaidiana.
Mimi nimeondoka kwenye shida ndogondogo kabla sijazaliwa, nafikiria nasaidiaje wengine wasiwe na shida.
Zaidi, hata nikivipoteza vyote hivi leo, nina uwezo mkubwa sana wa kuishi maisha simple tu bila kuwa na msongo mkubwa sana wa mawazo.
Kama ningekuwa mtu wa kuangalia shida na raha za maisha, nilitakiwa niwe namshukuru Mungu kila siku.
Sipingi uwepo wa Mungu kwa kuangalia maisha yangu binafsi. Napinga kwa kuangalia logical fallacies and contradictions in the basic tenets posing the existence of God.
Ukiacha mambo ya kawaida siwezi kusema nimepitia matatizo.
Naomba uache kufanya speculations kwenye maisha yangu.
Kama una swali, uliza.