Speculation.
Mambo magumu gani, umejuaje, unaweza kuthibitishaje hilo?
Mimi napinga uwepo wa Mungu kwa kuangalia logical fallacies na contradictions katika dhana ya kuwepo Mungu.
Si kwa sababu ya matatizo ya maisha.
Kama tunaangalia matatizo ya maisha, nilitakiwa kumkubali sana Mungu.
Kwa sababu.
Nimeanza kutembea corridors za Ikulu ya Tanzania tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu.
Nimepelekwa shule na Chauffeur driven Range Rover Classic Vogue 4.0. na Landcriser VX, Mercedes Benz, Pajero Intercooler Turbo among other luxury SUVs.Nimekaa na kukulia mitaa ya washefa Tanzania, nimeenda kusoma New York City Marekani, nikafanya kazi Wall St. Nina biashara nzuri tu za kupoteza $25,000 kwa siku, na kuzirudisha maradufu. Naendesha ndinga kali, nina kila kitu Mtanzania wa kawaida anachokitafuta.
Zaidi, hata nikivipoteza vyote hivi leo, nina uwezo mkubwa sana wa kuishi maisha simple tu bila kuwa na msongo mkubwa sana wa mawazo.
Kama ningekuwa mtu wa kuangalia shida na raha za maisha, nilitakiwa niwe namshukuru Mungu kila siku.
Sipingi uwepo wa Mungu kwa kuangalia maisha yangu binafsi. Napinga kwa kuangalia logical fallacies and contradictions in the basic tenets posing the existence of God.
Ukiacha mambo ya kawaida siwezi kusema nimepitia matatizo.
Naomba uache kufanya speculations kwenye maisha yangu.
Kama una swali, uliza.