Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Naongela asili ya tamko "Sadaka", usiniulize swali hilo, halipo katika msingi wa tamko, bali limekuja kuelezea kwa lugha ya kiingereza. Elewa nilichokiandika.

Waulize wenye tamko lao "Sadaka" wanalofasili vipi.
Wewe unaongelea neno, mimi naongelea dhana.

Hivyo umebaki kwenye lugha moja, wakati mimi nimekusanya lugha zote katika dhana.

Hiyo ndiyo tofauti yako na mimi.
 
Bwana hili swala la Mungu kwakwel ni jambo ambalo lina utata mwingi sana kwa ninayoyaona mimi au kupitia kuna muda napata mashaka sana juu ya uwepo wake ingawa nimezaliwa kwene ukisto
Hapo bila ya shaka utakuwa unachanganya mambo ya ukristo na imani nzima ya uwepo wa Mungu, kuna vitu ambavyo ulitakiwa uhitaji ufafanuzi kwenye ukristo ila wengi mnaishia kutilia mashaka imani ya uwepo wa Mungu na wengine huitimisha hakuna Mungu kabisa kwa mashaka yenye kuhusiana na ukristo.
 
No mkuu unajua ninaposema kuwa nina mashaka uwepo wake ni pale anapo kuwa hajibu maombi kwa wakati
 
No mkuu unajua ninaposema kuwa nina mashaka uwepo wake ni pale anapo kuwa hajibu maombi kwa wakati
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, hata usingehitaji kumuomba lolote.

Angekupatia unachoomba kabla ya kumuomba, usingekuwa na haja ya kuomba.

Ukiona una haja ya kumuomba Mungu huyo chochote, huo ni ushahidi kwamba hayupo.
 
Wewe huwa unaropoka tu mtu ambaye unaona hata haya majadiliano yasingekuwepo et kama Mungu angekuwepo, sasa mtu kama wewe si unachosha watu tu humu.
 
Sawa sawa kumbe dhana ya sadaka inatofautiana sana maana kwa wengine sadaka ni kujitoa kwaajili ya watu wenye mahitaji maalumu ya kile ulichokitoa/ unachokitoa sio lazima kuwe na matarajio ya majibu flani kutokana na sadaka yako.
 
Kuna namna ambayo naweza kusema yupo sabab ya uumbaji au mpangilio wote wa mwanadamu na mazingira ya dunia kutokea ila sasa nahisi ameuacha ulimwengu ujitesekee wenyewe thus y anakua kama hayupo tu au nipo wrong mr kiranga
 
Ikiwa vilivyo complex na vinavyoonekana kuwa na mpangilio ni lazima viwe vimeumbwa, hilo linathibitisha Mungu muumba wa vyote hawezi kuwepo.

Kwa sababu, hata yeye, ambaye ni complex pia, atahitaji muumbaji wake.

Unaelewa hilo?
 
Mungu yupo. Anafanya mambo kama apendavyo kwasababu anamiliki kila kitu katika ulimwengu wote.

Maombi yanafanyika kwasababu Mungu alimpa mwanadamu utawala wa dunia. Mamlaka ya mambo yote alimwachia mwanadamu.

Mwanadamu alipoasi na kufuata maagizo ya shetani ndipo alipopoteza uzuri wa hii dunia. Mabaya yote unayoyaona yamesababishwa na distortion katika asili ya kila kitu.

Sasa maombi ndio yanatumika kutafuta msaada wa Mungu kukabiliana na mabaya ya duniani.

Mungu ameweka nyakati na majira. Mwisho atauondoa uovu wote.
 
No mkuu unajua ninaposema kuwa nina mashaka uwepo wake ni pale anapo kuwa hajibu maombi kwa wakati
Mtoto wako wa miaka mitatu anapotaka umwache akacheze peke yake huko barabarani na ukamzuia inamaana humpendi? Jibu ni hapana. Unaona hatari zilizopo na unamuepusha. Ndivyo ilivyo kwa Mungu. Wakati mwingine anazuia mambo tunayoona ni mazuri kwasababu yeye anajua mwisho wa kila kitu.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Umeandika tu yupo.

Hilo halithibitishi yupo.
 
Kila mwanadamu ndani yake anafahamu kuwa yupo Mungu. Tofauti inakuwa namna tunavyomtafuta na kuhusiana naye.

Umeongea vizuri. Majibu yakiwa na mashaka katika dini watu wanakimbilia kusema hayupo.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, mabaya yasingewezekana kuwepo.

Mabaya yanawezekana kuwepo.

Hilo linathibitisha Mungu huyo hayupo.
 
Kila mwanadamu ndani yake anafahamu kuwa yupo Mungu. Tofauti inakuwa namna tunavyomtafuta na kuhusiana naye.

Umeongea vizuri. Majibu yakiwa na mashaka katika dini watu wanakimbilia kusema hayupo.
Wewe unajuaje kila mwanadamu anavyofahamu?
 
Ikiwa vilivyo complex na vinavyoonekana kuwa na mpangilio ni lazima viwe vimeumbwa, hilo linathibitisha Mungu muumba wa vyote hawezi kuwepo.

Kwa sababu, hata yeye, ambaye ni complex pia, atahitaji muumbaji wake.

Unaelewa hilo?
Mungu sio complex. Hili umelitoa wapi ikiwa Mungu hayupo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…