Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Wewe unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu? Utajuaje kama huo utakaopewa ndio uthibitisho?
Hilo swali hana jibu lake kwa sababu huko kudai uthibitisho ni kama wimbo tu ni kitu alichokikariri, uthibitisho si kitu ambacho kilichomfanya aseme hakuna Mungu kwamba et hakuna uthibitisho ndio maana anasema Mungu hayupo.
 
Wewe unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu? Utajuaje kama huo utakaopewa ndio uthibitisho?
Nipe uthibitisho kwanza.

Mimi naanzia kutaka uthibitisho ulio logically consistent na usioweza kuwa contradicted.
 
Hilo swali hana jibu lake kwa sababu huko kudai uthibitisho ni kama wimbo tu ni kitu alichokikariri, uthibitisho si kitu ambacho kilichomfanya aseme hakuna Mungu kwamba et hakuna uthibitisho ndio maana anasema Mungu hayupo.
Swali nimelijibu.

Acha ku assume.
 
Unajuaje kupatikana au kutokea kile walichoomba kumesababishwa na maombi kujibiwa, na si kitu kingine chochote?
Maombi kwa Mungu ni suala la imani hivyo kwenye kupatikana au kutokea kwa kile kilichoombwa inawezakuwa ni majibu ya maombi kwa mwenye kuamini au inaweza kuwa ni kitu chengine.
 
Ume assume sitaweza kulijibu swali.

Nimelijibu.

Ume assume kwa makosa.

Kubali tu.
Makosa gani na wakati kweli haujajibu hilo swali, unachoulizwa chengine na unachokuja kukijaza chengine na ndio ulichokifanya.
 
Nakuuliza unajuaje ni A na si B.

Unanijibu inawezekana ni A au B.

Hujajibu swali.

Umekubali hujui kutenganisha A na B.
Ungeeleza basi hiyo B ni nini, wewe umeuliza najuaje kwamba kilichotokea ni majibu ya maombi au kitu chengine ila hujaeleza hicho chengine ni kipi ili tuchambue kilichotokea ni majibu ya maombi au ni hicho kitu chengine.

Mimi nimeonesha kukubali uwepo wa vyote viwili A na B.
 
Nipe uthibitisho kwanza.

Mimi naanzia kutaka uthibitisho ulio logically consistent na usioweza kuwa contradicted.
Uthibitisho mmoja ni moral law. Dunia nzima kuna ufanano wa tafsiri wa kufahamu wema au ubaya. Mungu ameumba utashi huu ndani ya kila mwanadamu. Imekuwa point of reference bila kujali mtu yupo wapi.

Sasa utafahamu vipi kwamba huu ni uthibitisho? Kwenye imani yenu ya hakuna Mungu, mnafahamu vipi kama jambo ni baya au jema ikiwa kila kitu kilitokea kwa bahati?
 
Maombi kwa Mungu ni suala la imani hivyo kwenye kupatikana au kutokea kwa kile kilichoombwa inawezakuwa ni majibu ya maombi kwa mwenye kuamini au inaweza kuwa ni kitu chengine.
Uthibitisho mmoja ni moral law. Dunia nzima kuna ufanano wa tafsiri wa kufahamu wema au ubaya. Mungu ameumba utashi huu ndani ya kila mwanadamu. Imekuwa point of reference bila kujali mtu yupo wapi.

Sasa utafahamu vipi kwamba huu ni uthibitisho? Kwenye imani yenu ya hakuna Mungu, mnafahamu vipi kama jambo ni baya au jema ikiwa kila kitu kilitokea kwa bahati?
Mmeanzisha ligi na Kiranga, poleni
 
Kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao unaweza kuruhusu mabaya, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?
 
Ikiwa vilivyo complex na vinavyoonekana kuwa na mpangilio ni lazima viwe vimeumbwa, hilo linathibitisha Mungu muumba wa vyote hawezi kuwepo.

Kwa sababu, hata yeye, ambaye ni complex pia, atahitaji muumbaji wake.

Unaelewa hilo?

Duh aisee apo sasa ushaniachanganya mkuu basi tufanye tu nimeelewa mana nikizid kuuliza najimix mimi mwenyewe
 
Kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao unaweza kuruhusu mabaya, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?
Kama ana muda wa kusoma,ebu asome dialogue hii kati ya Atheist Ivan Karamazov na Mdogo wake

Hoja zote za Kiranga kuhusu inakuwaje Mungu muweza wa yote,mjuzi na anayejua yaliyopita,ya sasa na yajayo inakuwaje anaumba Ulimwengu amabao watoto,walemavu na wasiojiweza wanateseka eti kwa kigezo kuwa wakiteseka ndiyo njia ya kuupata wokovu?

Mungu alishindwa nini kuumba ulimwengu uliyo perfect?

Kwanini alimuumba Shetani huku akijua kuwa baadae atahasi na kuusumbua ulimwengu?

Kwanini gharama ya binadamu anayolipia ili Mungu aamini kuwa binadamu anampenda ni maumivu na mateso yanyoitwa eti "majalibu"?

Kwahiyo upendo wa binadamu kwa Mungu wake proof yake ni mateso ya kimwili,kisaikolojia na kiakili?

Kwahiyo Mungu hajiamini?

Binadamu wakiteseka ndiyo proof Mungu anapendwa?

Anashindawa nini kuyafupisha ayo mateso kwa kuangalia tu ndani ya mioyo ya viumbe wake na kushuhudia?

Sasa kama kigezo ni mpaka uteseke ili uprove upendo wako kwa kujitwisha msalaba wa majaribu,vipi kwa wale wasioweza himili hayo mateso,watahukumiwaje siku ya hukumu?

Ibrahimu alijaribiwa kihusu kumtoa kafara Isaka,Mungu alishindwa nini kuuchunguza wa Ibrahimu na kujiridhisha kama anapendwa au apendwi badala ya kumtesa kiimbe wake kiaaikolojia?
 
Attachments

Back
Top Bottom