Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, mabaya yasingewezekana kuwepo.

Mabaya yanawezekana kuwepo.

Hilo linathibitisha Mungu huyo hayupo.
Unajuaje kama duniani kuna jambo baya? Kila kitu si kilitokana na mlipuko wa utupu tena kwa bahati tu? Reference yako ni nini kujua lipi baya na lipi jema?
 
Mungu sio complex. Hili umelitoa wapi ikiwa Mungu hayupo?
Mungu si complex, kwa sababu hayupo.

Nakueleza wewe unayesema Mungu yupo.

Ikiwa kilicho complex ni lazima kiwe kimeumbwa na kilicho complex zaidi, hilo litathibitisha Mungu muumba vyote hawezi kuwepo.

Kwa sababu hata yeye itabidi awe na muumba wake, na akihitaji muumba wake, anakuwa si muumba vyote.
 
Shida yenu hamjui wapi mshike, hakuna aliyekataa kama mpagani hawezi kuwa mwema.

Hoja ipo katika matumizi ya tamko "Sadaka". Unatoa sadaka kwa ajili ya nini na kwa nani ?

Kingine hamjui hata wapi pakuchukua maana za maneno, mwenzako akaenda Wikipedia au huko alikochukua, nikajua amepita kwenye Kamusi ya Waarabu wenyewe hata moja akachukua maana ya tamko hilo, sababu hata "tabasamu" nalo ni sadaka, lakini utaulizwa kwa nani na kwanini ?

Sasa nina uhakika mimi nimesoma vitabu vingi nje ya dini kukuzidi wewe. Msifikiri sisi wajinga kama nyinyi, sisi kila kitu tunakirudisha kwa watu wake.
Wakipata vihela kidogo, wakawasoma philosophers wawili watatu basiii wanamfuta Mungu.. kiburi cha kijinga kabisa....!
 
Wakipata vihela kidogo, wakawasoma philosophers wawili watatu basiii wanamfuta Mungu.. kiburi cha kijinga kabisa....!
Hujathibitisha Mungu yupo.

Mimi nimekataa uwepo wa Mungu tangu nina miaka 18 nikiwa sijaanza kazi wala kupata hela.

Acha assumptions za uongo.

Jibu hoja kwa hoja, thibitisha Mungu yupo.
 
Mungu si complex, kwa sababu hayupo.

Nakueleza wewe unayesema Mungu yupo.

Ikiwa kilicho complex ni lazima kiwe kimeumbwa na kilicho complex zaidi, hilo litathibitisha Mungu muumba vyote hawezi kuwepo.

Kwa sababu hata yeye itabidi awe na muumba wake, na akihitaji muumba wake, anakuwa si muumba vyote.
Mungu ni muumbaji asiyeumbwa kwasababu yeye ni chanzo cha kila kitu. Hahitaji kuumbwa kwasababu yeye ndio chanzo cha hii dimension yote iliyopo.
 
Wewe unaongelea neno, mimi naongelea dhana.

Hivyo umebaki kwenye lugha moja, wakati mimi nimekusanya lugha zote katika dhana.

Hiyo ndiyo tofauti yako na mimi.
Kwanini unaandika uongo ? Nilikwambia unatakiwa ujifunze sana maana za maneno unayo yatumia.

Hilo neno halina maana ? Halitumiki mpaka useme naongelea neno na wewe unasema unaongelea dhana ? Dhana ni wazo, na neno ni tamko lenye maana na kufanyiwa kazi kwa munasaba husika.

Tamko ulilo litumia lina asili, na asili yake ni Kiarabu, kwahiyo watu wa kwanza kuwauliza wenye neno lao, kisha lugha nyingine inakuja kufasiri kwa kufata maana ya watu husika. Kama ilivyo maneno yenye asili ya Kiingereza, marejo ya maana ni kwa wenye neno lao.

Sasa lugha gani umekusanya, wakati aliyefasiri neno hilo kwa kiingereza hajakidhi haja ya tamko husika ?
 
Wa Shinto wanatoa sadaka?
 
Mungu ni muumbaji asiyeumbwa kwasababu yeye ni chanzo cha kila kitu. Hahitaji kuumbwa kwasababu yeye ndio chanzo cha hii dimension yote iliyopo.
Unajuaje hilo ni kweli na si hadithi uliyojazwa kwa uongo tu?

Na huoni kwamba, ukiruhusu Mungu kuwa muumbaji asiyeumbwa, umeruhusu hata vingine kuwepo bila kuumbwa na hivyo kuondoa sababu ya Mungu muumbaji kuwepo?

Mbona unaweka arbitrary rules?

Mara Mungu anahitajika kuwepo kama muumbaji, kwa kuwa complexity haiwezi kuwepo bila kuumbwa, mara Mungu hakuumbwa.

This is a contradion.

It shows that that God does not exist.

He is just a made up story, one that is not even logically consistent.
 
Basi niseme hajibu tu kwakwel mana mambo yanavyokwenda ni kama nisipotumia akili yangu aisee hakuna kitakachotokea
Ok nisiegemee upande wowote, wapo wengine ambao wanaomba na kujibiwa hao unawazungumzia vp?
 
Unajuaje hilo ni kweli na si hadithi uliyojazwa kwa uongo tu?

Na huoni kwamba, ukiruhusu Mungu kuwa muumbaji asiyeumbwa, umeruhusu hata vingine kuwepo bila kuumbwa na hivyo kuondoa sababu ya Mungu muumbaji kuwepo?

Mbona unaweka arbitrary rules?

Mara Mungu anahitajika kuwepo kama muumbaji, kwa kuwa complexity haiwezi kuwepo bila kuumbwa, mara Mungu hakuumbwa.

This is a contradion.

It shows that that God does not exist.

He is just a made up story, one that is not even logically consistent.
Haya mambo ya complexity nimeyaandika wapi? Kila kitu kina chanzo chake. Mungu ndio chanzo cha kila kitu.

Swali hapa ni je Mungu alitoka wapi? Kwa sehemu ninaona hili swali linakuja kwasababu sisi tupo kwenye ulimwengu ambao tayari unaonesha kwamba kila kitu lazima kiwe na chanzo. Ni kanuni ya asili. Lakini hii haiwezi kutumika kwenye dimension ambayo Mungu yupo. Yeye yupo nje ya uasili huu.

Lakini pia kwa kuzingatia logic ya maandiko, Mungu hajasema sana chanzo chake lakini ameeleza tu kwamba yeye hana mwanzo wala mwisho.
 
Sasa huoni kwamba umeshajimalizia habari za sadaka bila kujua mambo mengi sana na ndiyo maana hatuelewani?
Unajua maana ya tamko "msingi" ? Mimi nina msingi yaani mizani, kwayo linalokuja linapimwa humo kisha hukumu inatoka. Kwahiyo kutokuwajua hakubadilishi chochote kwa namna yoyote. Wewe unaye wajua sema kisha tuwaweke sehemu wanayo stahiki.
 
Back
Top Bottom