Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Unampaje uhuru wa kuchagua mtu ambaye unajua mwisho wake yani unajua atakachokichagua hata kabla hujamuumba na yet unamuumba ili akachague upande unaodai ni mbaya umpunish?
Rubani wa Boeing 777 akiamua kutua juu ya ndege nyingine halafu ajali ikatokea na kuua watu utawalaumu Boeing kwa kutengeneza ndege ambayo inaweza kuanguka?.

Ukifuata kanuni za muumba wala hakuna punishment.
 
Kulingana na maandiko ya wayahudi.
Uyahudi unasema Mungu aliumba Ulimwengu mkamilifu ila kiumbe wa Mungu aitwae malaika akahasi kwa kutumia uhuru wake wa kifkra kwa kuchagua kumpinga Mungu

Toka umalaika mpaka akawa Shetani

Ila kumbuka katika mtiririko huo wote Mungu alikuwa anajua kuwa siku moja ataumba kiumbe ambae ni malaika na baadae huyo malaika atahasi ili awe shetani

Na huyo Shetani baadaye aatatupwa na Mungu duniani ali awajaribu binadamu ili waweze kuutumia uhuru wao wa kumchagua Mungu au Shetani kwa ahadi ya Kuzimu kama wataamua kwa uhuru wao aliyowapa Mungu kumtumikia Shetani

Au ahadi ya uzima wa milele kama wataamua kumtumikia Mungu kwa uhuru wao

Huyo uhuru una faida gani kama mwisho wa siku umepewa alternative mbili tu?
 
Rubani wa Boeing 777 akiamua kutua juu ya ndege nyingine halafu ajali ikatokea na kuua watu utawalaumu Boeing kwa kutengeneza ndege ambayo inaweza kuanguka?.

Ukifuata kanuni za muumba wala hakuna punishment.
Boeing sio muumba, Mungu hapaswi kuwa na udhaifu huo.
Na watengenezaji wa boeing hawakujua kuwa ipo siku rubani kichaa anaweza kufanya hivyo maana hawajui ya mbeleni lakini Mungu anayajua hata kabla hajakuumba kuwa huyu lazima ataniasi. So mfano wako ni irrelevant
 
Uyahudi unasema Mungu aliumba Ulimwengu mkamilifu ila kiumbe wa Mungu aitwae malaika akahasi kwa kutumia uhuru wake wa kifkra kwa kuchagua kumpinga Mungu

Toka umalaika mpaka akawa Shetani

Ila kumbuka katika mtiririko huo wote Mungu alikuwa anajua kuwa siku moja ataumba kiumbe ambae ni malaika na baadae huyo malaika atahasi ili awe shetani

Na huyo Shetani baadaye aatatupwa na Mungu duniani ali awajaribu binadamu ili waweze kuutumia uhuru wao wa kumchagua Mungu au Shetani kwa ahadi ya Kuzimu kama wataamua kwa uhuru wao aliyowapa Mungu kumtumikia Shetani

Au ahadi ya uzima wa milele kama wataamua kumtumikia Mungu kwa uhuru wao

Huyo uhuru una faida gani kama mwisho wa siku umepewa alternative mbili tu?
Umeeleza vizuri. Kuna pande mbili na unatakiwa kuchagua moja.

Jambo moja la kukumbuka ni kuwa Mungu anamiliki dunia yote kwa haki ya uumbaji. Ni mali yake na anaweza kuamua atakavyo.

Wewe ukiwa na mali yako, mfano gari, utataka litumike kwa namna unavyopenda. Hutegemei mtu mwingine akupangie matumizi yake.

Sasa ni hivyo pia kwa Mungu. Anamiliki na anao uhuru wa kuamua kipi kiwe vipi.

Unataka alternative nyingine iwe ipi?
 
Boeing sio muumba, Mungu hapaswi kuwa na udhaifu huo.
Na watengenezaji wa boeing hawakujua kuwa ipo siku rubani kichaa anaweza kufanya hivyo maana hawajui ya mbeleni lakini Mungu anayajua hata kabla hajakuumba kuwa huyu lazima atanihasi. So mfano wako ni irrelevant
Huo ulikuwa ni mfano rahisi kuonesha namna uhuru unaweza kutumiwa vibaya. Mungu alijua uasi utaweza kutokea kwasababu ya uhuru aliompa mwanadamu. Ila upendo wake ulimfanya aamue kumwamini mwanadamu kwamba atafuata maelekezo yake.
 
So kumbe sio mjua yote? Aka assume kuwa atafuata maelezo yake, so kumbe sio mjua yote? So upendo ukamtia weakness? Na mwisho binadamu hakufuata maelekezo yake, which means hajui yote sasa.
Unajichanganya na unamwondolea sifa za kuwa ni perfect.
 
Anajua yote na ametengeneza njia ya kumsaidia mwanadamu. Anachotaka yeye ni Kuhakikisha unamchagua kwa hiari yako.
 
Back
Top Bottom