Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Anajua yote na ametengeneza njia ya kumsaidia mwanadamu. Anachotaka yeye ni Kuhakikisha unamchagua kwa hiari yako.
Unajichanganya sana ujue.
Narudia tena, anajua kabisa huyu mwisho wake ni huu, ni kuniasi kwasababu ya udhaifu wake lakini bado unasema anakuumba na uhuru huku akijua utamuasi? So anakuumba akijua utamuasi ili akupunish?
Maana kama anajua mwisho wako ni uasi hategemei ubadilike maana mwisho ashaujua.
 
Unampaje uhuru wa kuchagua mtu ambaye unajua mwisho wake yani unajua atakachokichagua hata kabla hujamuumba na yet unamuumba ili akachague upande unaodai ni mbaya umpunish?
Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu ili nipate kumjibu anilaumuye.
meth27.
Hata Mungu anajua maumivu tunayoyapata wanadamu...wewe sio wa kwanza kila Binadamu anapopata matatizo hujiuliza maswali kama yako rejea kisa cha Ayubu mpaka mkewe alimshawishi amkufuru Mungu...
 
Kama Mungu mjua yote hata wakati anamjaribu Ayubu alijua kuwa atalishinda maana si anajua hata ambayo hayajatokea? Hivyo majibu tayari alikuwa nayo hata kabla ya kumuumba
 
Unajichanganya sana ujue.
Narudia tena, anajua kabisa huyu mwisho wake ni huu, ni kuniasi kwasababu ya udhaifu wake lakini bado unasema anakuumba na uhuru huku akijua utamuasi? So anakuumba akijua utamuasi ili akupunish?
Maana kama anajua mwisho wako ni uasi hategemei ubadilike maana mwisho ashaujua.
Kuna vitu viwili. Predestination na Foreknowledge.

Predestination, ni kwamba yeye ameweka plan toka mwanzo kwamba amekuumba na uwezo wa kumfuata yeye. Na ikiwa umefail basi amekuwekea njia ya kujirekebisha.

Foreknowledge, hapa ni Mungu anakuona wewe mwaka 2000, mwaka 2022 na mwaka 2040 (kwa maana ya past, present and future). Anaona unachofanya nyakati zote za maisha yako. Sio kwamba amekupangia au anacontrol unachofanya bali anakuona. Yeye hafungwi na muda.
 
Iliwezekana kwasababu Mungu alimpa mwanadamu uhuru wa kuamua.

Mungu ameumba tayari ulimwengu ambao dhambi haiwezi kufanyika. Ni ule unaofuata baada ya huu. Hapakuwa na dhambi tena.

Kwa nini hakuumba huu ukiwa hauwezi kufanyika dhambi?

Huo ulimwengu unaokuja unaweza kuthibitisha upo kweli na si hadithi tu?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao una uhuru, lakini hauna dhambi?
 
Kuna vitu viwili. Predestination na Foreknowledge.

Predestination, ni kwamba yeye ameweka plan toka mwanzo kwamba amekuumba na uwezo wa kumfuata yeye. Na ikiwa umefail basi amekuwekea njia ya kujirekebisha.

Foreknowledge, hapa ni Mungu anakuona wewe mwaka 2000, mwaka 2022 na mwaka 2040 (kwa maana ya past, present and future). Anaona unachofanya nyakati zote za maisha yako. Sio kwamba amekupangia au anacontrol unachofanya bali anakuona. Yeye hafungwi na muda.
Haimake sense, kama ni mjua yote na uwezo mnaosema mambo yake hayawezi kuwa ya probability na possibility lazima yawe ya uhakika yasiyokuwa na shaka kabisa.
Sasa hiki cha kukuona mbeleni na akajua nini kitakutokea na bado akakuacha upotee akakuumba ili aje akuadhibu ndo kinashangaza.
 
Kwa nini hakuumba huu ukiwa hauwezi kufanyika dhambi?

Huo ulimwengu unaokuja unaweza kuthibitisha upo kweli na si hadithi tu?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao una uhuru, lakini hauna dhambi?
Hakushindwa na ndio maana tayari ameuumba huo usio na dhambi. Utakuwa na uhuru na hautakuwa na dhambi.
 
Haimake sense, kama ni mjua yote na uwezo mnaosema mambo yake hayawezi kuwa ya probability na possibility lazima yawe ya uhakika yasiyokuwa na shaka kabisa.
Sasa hiki cha kukuona mbeleni na akajua nini kitakutokea na bado akakuacha upotee akakuumba ili aje akuadhibu ndo kinashangaza.
Hajakuacha upotee. Hata muda huu tunaandika hapa ni yeye anaendelea kukukumbusha ufuate njia aliyoiweka kwa ajili yako.
 
Kama Mungu mjua yote hata wakati anamjatibu Ayubu alijua kuwa atalishinda maana si anajua hata ambayo hayajatokea? Hivyo majibu tayari alikuwa nayi hata kabla ya kumuumba
Mungu hakututengeneza kama robort au midoli inayochezeshwa alituumba ili tutawale dunia. kama utapata muda soma mwanzo) ili ujue lengo lake kutuumba duniani.
 
Hakushindwa na ndio maana tayari ameuumba huo usio na dhambi. Utakuwa na uhuru na hautakuwa na dhambi.
Huo wa kuhadithiana uondoe, mimi sikubali kwamba upo na wewe huwezi kuthibitisha kwamba upo.

Kwa nini hakuumba huu uwe hauwezekani kufanyika dhambi?

Kwanini acheleweshe mpaka huo unaousema?

Anapenda watu waangamie katika dhambi?
 
Mungu hakututengeneza kama robort au midoli inayochezeshwa alituumba ili tutawale dunia. kama utapata muda soma mwanzo) ili ujue lengo lake kutuumba duniani.
Nimekuuliza, Mungu si mjua yote? Na freedom aliyonipa ya kuchagua si inabidi ajue mwisho wangu ni nini?
 
Huo wa kuhadithiana uondoe, mimi sikubali kwamba upo na wewe huwezi kuthibitisha kwamba upo.

Kwa nini hakuumba huu uwe hauwezekani kufanyika dhambi?

Kwanini acheleweshe mpaka huo unaousema?

Anapenda watu waangamie katika dhambi?
Kuumba ufanane vipi na lipi liwezekane au liwezekane ni uamuzi wake kama mmiliki wa ulimwengu.

Hajachelewa, anafanya kwa majira na nyakati alizoziweka.

Hapendi waangamie na ndio maana anaongea nao kila uchwao. Hata hapa anaongea na wewe.
 
Back
Top Bottom