Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Kuna vitu viwili. Predestination na Foreknowledge.

Predestination, ni kwamba yeye ameweka plan toka mwanzo kwamba amekuumba na uwezo wa kumfuata yeye. Na ikiwa umefail basi amekuwekea njia ya kujirekebisha.

Foreknowledge, hapa ni Mungu anakuona wewe mwaka 2000, mwaka 2022 na mwaka 2040 (kwa maana ya past, present and future). Anaona unachofanya nyakati zote za maisha yako. Sio kwamba amekupangia au anacontrol unachofanya bali anakuona. Yeye hafungwi na muda.
Thibitisha Mungu yupo na hizi habari za kuwapo Mungu si hadithi za watu kujitungia tu.
 
Anajua mwisho wako. Na anakusaidia ufike kwenye huo mwisho. Uchaguzi ni wako kuufikia.
Kwa hiyo akama alijua mwisho wa peter atanikosea atende madhambi, na bado akamuumba halafu unasema akampa uhuru ambao anajua fika atachagua kumkosea. Si ndio?
 
Kuumba ufanane vipi na lipi liwezekane au liwezekane ni uamuzi wake kama mmiliki wa ulimwengu.

Hajachelewa, anafanya kwa majira na nyakati alizoziweka.

Hapendi waangamie na ndio maana anaongea nao kila uchwao. Hata hapa anaongea na wewe.
Hujathibitisha Mungu yupo.

Hujatoa sababu ya kueleweka kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea.

Kwa sababu, huyo Mungu hayupo, katungwa na watu tu.
 
Kwa hiyo akama alijua mwisho wa peter atanikosea atende madhambi, na bado akamuumba halafu unasema akampa uhuru ambao anajua fika atachagua kumkosea. Si ndio?
Anajua mwisho wa kila mtu kwasababu anamuona anavyofanya maamuzi. Yeye anaona mwanzo hadi mwisho. Hapo anataka utumie uhuru wako kufuata anavyopenda.
 
Anajua mwisho wa kila mtu kwasababu anamuona anavyofanya maamuzi. Yeye anaona mwanzo hadi mwisho. Hapo anataka utumie uhuru wako kufuata anavyopenda.
Hivi unasoma unachokiandika kweli mkuu? Ashajua mwisho wako, sasa hayo maamuzi aliyokupa yatakusaidia nini wakati mwisho wake ashajua kuwa utaasi tu? Kuna mabadiliko anayategemea labda kwa mtu ambaye ashajua mwisho wake? Kama yakitokea basi atakuwa sio mjua yote.
 
Naelewa sana. Anajua kwasababu yeye anakuona wewe unavyofanya tangu mwanzo hadi mwisho. Kwahiyo ukibadilika na kufuata predestination then atakuwa anakuona na kujua mwisho wako.
 
Back
Top Bottom