Kisa cha rafiki yangu wa Mafia

Vile mwafrika alivyokuwa brainwashed..inashangaza sana.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umeupiga mwingii umeelezea kwa kina sanaa [emoji3059][emoji3059]
 
huu ndio ukweli mchungu: katika baadhi ya maeneo ya imani hiyo anayoiongelea wanaamini kuwa maovu yote yanafanywa na wasio na imanai yao. Wanaaminini kuwa wao ni wasaafi - hii ndiyo ajabu yenyewe
 

Tafuta Kanisa zuri karibu yako; wakristo wanafundishwa Upendo, Ila usiende Kwa Manabii Na wapiga ramli
 
Huyo mleta mada ama nae ni MUONGO au ni mtu kutoka vijijini, na wala asiseme "kwetu Mafia tunafundishwa...." bali aseme "kwenye familia yao wanafundishwa..."
Sawa, lakini "dini" haifundishwi kwenye familia pekee, naamini yukosahihi 100%
 
Sawa, lakini "dini" haifundishwi kwenye familia pekee, naamini yukosahihi 100%
Yuko sahihi fundisho lipi?

1. Kwamba Uislamu unakataza Mwislamu kukaa karibu na Mkristo kwa sababu Mkristo ni zaidi ya nguruwe au mbwa,

2. Au yupo sahihi kwamba Ukristo unakataza kukataza karibu na Mwislamu kwa sababu utapata majini, au

3. Ay yupo sahihi kwa yote hayo?
 
Nimejisikia vizuri sana aliposema ameanza kufikiria ikiwa kweli Mungu yupo?

Bila shaka hivi karibuni atatambua Mungu wa imani yake hayupo, wala Miungu wa imani nyingine tofauti na imani yake hawapo.
Namtakia kila la kheri.
Mbona unajijibu mwenyewe? Umesahau kuswitch id siyo
 
Na.2 na 3 umetengeneza ya kwako, huenda unauelewa juu ya hayo.
Na 1 ndicho alichosema: harafu unajua na unajifanya hujui, poor you.
 
Upo sahihi sana Mkuu ,hakuna dini inayofundisha kumchukia jirani yako haijalishi tofauti ya imani yake bali aya mambo yametokea sababu ya mitazamo ya wanazuoni mbalimbali katika kuendelea ku exist

Wakristo tulikuwa na mitazamo tofauti kwa waislamu katika kuonyesha sisi ni bora zaidi yao ndio maana kulikuwa na kejeli mbalimbali mfano: tulikuwa tunasema waislamu hawali nguruwe sababu mt.Muhamad maiti yake ililiwa na nguruwe na kwavile tulikuwa watoto tuliami kabisa

Pia kwa upande wa waislamu ni ivyo ivyo, hasa miaka ile 90's ya mihadhara kulikuwa na upinzani mkubwa sana ,Mimi binafsi nimeshawai kubaguliwa sababu ni mkristo jamii tuliyokuwa tunaishi ni mchanganyiko maeneo ya Temeke, sasa nilikuwa na rafiki yangu mmoja anaitwa Rajabu ambae ni muislamu tulikuwa tunasoma wote primary siku moja tunarudi home tukapita karibu na chuo chao madrasa ndipo tukakutana na kundi la watoto wenzake wa chuo ,wakaanza kumuuliza Rajabu rafiki yako anaitwa nani ,akawa kama anasita kujibu ndipo mimi nikaropoka jina la kikristo hauwezi amini (labda kwavile tulikuwa watoto) pale pale walianza kumwambia Rajabu kwanini anakuwa na rafiki mkristo kafiri na maneno mengine mengi siyakumbuki ,nilijisikia vibaya sana ingawa rafiki yangu Rajabu aliniambia niachane nao baada ya kutoka pale

Hivyo ni visa vichache katika jamii zetu, ingawa tuliishi vizuri mpaka Leo bila ubaguzi wowote kwenye sikukuu zetu tunaleteana mapilau mfano kwa upande wetu wakristo ikifika sikukuu zetu tunatafuta muislamu atuchinjie kuku ili iwe rahisi kwetu kuwapelekea vyakula ivyo

Rajabu mpaka Leo ni rafiki yangu na tumeshakuwa wakubwa ingawa sasa ivi tupo mikoa tofauti katika kutafuta maisha
 
Wape elimu hao wasioujua Uislamu ni nini?

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Na.2 na 3 umetengeneza ya kwako, huenda unauelewa juu ya hayo.
Na 1 ndicho alichosema: harafu unajua na unajifanya hujui, poor you.
Eti ndicho ulichosema...

Usichojua ni kwamba Post #2 kai-edit na akafuta aliposema Wakristo wanafundishwa wasikae na Waislamu kwa sababu watapata majini!

Na kama ndivyo alivyosema, ilikuaje anijibu:-
Imani za ukristo na uislamu wote wanafundisha chuki dhidi ya wenzao, ni vile tu kila dini inafundisha chuki kwa aina yake.
aise,

How come umefuta post yako ulipoandika habari za Wakristo kufundisha watoto wao kwamba wasikae na Waislamu kwa sababu watapata majini? Mbona umefuta simulizi za rafiki yako Swaumu na kwamba ukawa unahisi vyote vina majini?

NI kwamba ulidanganya sio?

Wewe unayejiita Gama siwezi kukushangaa kwa sababu nilishawahi kukutana na wewe kwenye mjadala mmoja uliokuwa unatetea mauaji ya Rohingya na bila aibu ukasema kwanza hao Waislamu wa Rohingya kule Myanmar sio kwao, wamefuata nini!!

Nilipokuambia wewe mwenyewe kwa hilo jina utakuwa Mngoni, na Wangoni Tanzania wamekuja tu kutoka SA, je itakuwa sahihi tukianza mauaji dhidi ya Wangoni... ukakimbia, na hukurudi tena!

Na kama wewe ni Mkristo kweli, utakubali angalau nafsini mwako kama utaona aibu kukiri hadharani kwamba nilichosema hapo juu ni KWELI KWA 100%!

Nimekukumbusha hayo ili kukuambia ACHA CHUKI!!!
 
Inawezekana wewe hupenda kunukuu na hujibidishi kubeba meaning ya content
 
Haya mambo yapo sana kuna Mwalimu wangu mmoja kwenye miaka ya mwanzoni mwa 2000 alipangiwa kazi huko Mbozi ndani ndani. Anafika kwenye huo mji yeye pekee ndio alikua Muislamu, kutokana na maelezo yake watu walikua wanamshangaa.

Kuna siku jioni yupo kwake akaja mzee mmoja na kumuuliza "Kijana nasikia wewe ni Muislamu". Jamaa akajibu "Ndio mzee mimi ni Muislamu". Mzee akauliza tena "Mbona upo kama sisi tu, hauna tofauti yoyote kabisa? Kwa maana tumekua tukiambiwa waislam sio watu kama sisi, wana manyoya mwili mzima na ni watu hatari sana". Ticha alibaki kushangaa tu.


Kutokana na mahali ulipozaliwa na kukulia unaweza kujikuta na mtazamo wa ajabu sana kuhusu watu wa jamii nyingine.
 
Inawezekana wewe hupenda kunukuu na hujibidishi kubeba meaning ya content
NImekuuliza, unafahamu kwanini alisema dini zote zinafundisha chuki?!

Use your common sense kijana! Wewe umeukutia uzi ukiwa na posts kadhaa wakati mimi nimeukuta ukiwa bado page ya kwanza! Unaona sina akili hadi nizungumzie kitu ambacho hakuandika?

Au angalia post yangu #11 yenye sehemu inayosema:-
Au tuseme katika maisha yako hujawahi kukaa na Mwislamu?! Inawezekana hivyo? Au ukigundua tu kwamba Mwislamu unamkimbia kwavile ulifundishwa (according to mtoa mada ambae umeamua kumwamini) ukikaa na Mwislamu utapata majini?!
Umeiona hiyo blacket?! Inakupa ishara gani?! Na ili usidhani kama nime-edit, angalia post #12 ambayo Khantwe alini-quote, na utaiona hiyo bracket! Unataka kusema sina akili hadi nikasema according to mtoa mada!

Na ndo hivi sasa naanza kumwelewa Khantwe kwanini alinihoji "Ni kitabu cha dini gani kimeandikwa kuwa watoto wao wakikaa na waislamu wanapata majini?"

Inawezekana nae alikuta jamaa kesha-edit sehemu ambayo jamaa aliandika "Kuna dini inafundisha watoto wao wasikae na Waislamu kwa sababu watapata majini"!!

Ni kutokana na hicho kipengele ndo maana post from my quote above niliweka bracket na kusema "according to mtoa mada..."!

Mwambie aise kama ana ujasiri aje hapa akatae kwamba hakuzungumzia suala la dini zingine kufundisha watoto wao wasikae na Waislamu ili wasije wakapata majini! Kama alivyoleta simulizi za Yohana, hapo akaleta simulizi za rafiki yake aliyekuwa anaitwa Swaumu!!!
 
Kiukweli Mafia mnayoisema mie siielewi ni ya wapi? Mie ni mkristo na nilipoenda mafia sikutegemea hata kitimoto ningeikuta Ila wazee Kuna pub na jamaa anatengeneza mbuzi katoliki safi sana na Kuna mangi mmoja anachoma mbuzi safi kabisa pale Mafia.

Haya mengine ni maneno ya kipuuzi ubaguzi huwa unakuwepo tu sababu ya kutozoea aina fulani ya maisha hata jamii ya kikristu huwabagua wengine sababu wanakuwa na Ile cultural shock ni Jambo la kawaida ambapo baada ya muda unakuja kuzoea tu.

Huu mchanganyiko wa jamii ndio husababisha watu kuzoeana na kuchukuliana na kuheshimiana Kama jamii iliyostaarabika ndio maana mzungu alipokuja alipewa maeneo na akakaribishwa akae wakajiweka kwenye maeneo yao kwa kuwa wenyeji wakiona Kama life ya wazungu ni tofauti.

Hata wahindi walipokuja nao walijitenga maeneo yao ya uhindini na wao kwa wao walijitenga unakuta wabohora Wana mtaa wao, jamatii Wana mtaa wao, waishamilia Wana mtaa wao, wasunni hivyohivyo basi ni ilikuwa wanaishi sababu ya kutozoea imani na maisha ya kila mwenzie.

Ila Mafia nguruwe nyama ipo Safi anayebisha aseme so huo ubaguzi wa kidini sijui na kama upo basi wa kawaida kwa familia na familia usigeneralize sheikh.
 
baada ya kumchunguza mtoa maada nimeona kuwa

YEYE SIO MUISLAM NA HAKUWAHI KUWA MUISLAM HATA SEKUNDE MOJA,
WALA SIO MKRISTO.
NI KAFIRI LILILOAMUA KUCHAFUA MAZINGIRA YA WATU, ILI WATU WAPIGISHANE MAKELELE.
VIZURI KULIPUUZA KAFIRI HILI LISILOKUWA NA NINI YOYOTE.
JAAHILI
 
Kwani huko Nairobi/Kenya hawana sheria za nchi? Kama wanayo unafikiri kuwa na sheria ndo kunazuia kutokea mambo ya ajabu. Ugaidi unatumia mwamvuli wa dini kupandikiza chuki tu kwa interest za watu wachache.
Chuki inaweza kupandikizwa hata kwa makundi mbalimbali iwe ya kisiasa au jamii ya watu flani dhidi ya jamii nyingine au chama kingine na chuki siku zote huleta machafuko rejea hata vita vya rwanda.
Hivyo kitu chochote kinachoenezwa au kutangazwa kwa chuki nicha kuwanacho makini. Naamini Maandiko yote Matakatifu yanisisitiza upendo kama msingi mkuu wa maisha.
N.b Lengo la huyu mleta mada nayo ni kuleta na kuchochea chuki ya kidini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…