Uchaguzi 2020 Kishindo: Sheikh Ponda atoa neno kwenye mkutano wa Lissu Dodoma, Uwanja walipuka kwa shangwe

Uchaguzi 2020 Kishindo: Sheikh Ponda atoa neno kwenye mkutano wa Lissu Dodoma, Uwanja walipuka kwa shangwe

Na safari hii wakijaribu kuiba kura watakoma, Lissu hataki ujinga, wafadhili/mabeberu nao hawataki ujinga, na wanaomuunga mkono Lissu wote nao hawataki ujinga, CCM itabidi wajue wataibaje hizo kura kwa akili vinginevyo kazi wanayo.
Hapa shida ni kwamba wajinga hawataki ujinga. Kwa hiyo hawataki ujinga kijinga.
 
Waaow leo nina akili fupi aisee. Hujajibu swali Genius chadema nzima,ni nani aliyewatupa uamsho huko walipo?
Kwa akili yako fupi nilikuwa natokwa POVU lakini Kikwete alikuwa DHAIFU na historia itamuandika hivyo. Kikwete alifikia hadi kuambiwa na Kinana kwamba kuna Mawaziri mizigo awafute kazi. Kikwete alilidanganya Taifa kwamba pesa za Escrow si za Watanzania leo hii Ruge na yule baniani wako ndani mwaka wa nne. Na huyo DHAIFU yuko kimya kabisa. Cha kushangaza pesa zile za Watanzania walizifaidi wengi sana lakini huyo MNAFIKI waliokuwa ndani ya maccm na Serikali kaogopa kuwagusa.

Haihusu kitu Mkapa alitaka Tume huru lini lakini hakuogopa kuongea hadharani kuhusu umuhimu wa uwepo wa Tume huru. Hakuna hata mmoja ndani ya maccm alimpinga au kumuunga mkono kutokana na UNAFIKI wao mkubwa.
View attachment 1603428
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo Wanaomuunga Mkono Tundu Lissu wanavyojitokeza na kuzidi kuongezeka.

Mwangalie Sheikh Ponda Issa Ponda alivyotikisa Dodoma leo.

Video hii hapa

====

SHEIKH PONDA: WAISLAMU TUMEKUBALIANA TUTAMPIGIA KURA LISSU

Sheikh Ponda Issa Ponda amesema Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu kushinda kura za urais katika Uchaguzi Mkuu 2020 sio tatizo

Amesema waislamu wote wamekubaliana kumchagua Lissu. Hivyo atashinda tatizo linaweza kuja kwenye suala la kutangazwa

Pia Sheikh Ponda amesema Mungu atashindwa kusikia maombi na sala za watanzania kama hawatamchagua Tundu Lissu kuwa Rais

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020

View attachment 1603231
Duh...!, huku sio kuchanganya dini na siasa?.
Viongozi wa dini, ni viongozi wa kiroho, hawapaswi kuwa amuru wafuasi wao, wamchague nani, au chama gani!, huku ni kuchanganya dini na siasa.

Maadam Taasisi rasmi ya Waislamu wa Tanzania ni Bakwata, then tunajua Waislamu wa ukweli wa Tanzania, wanataka maendeleo ya kweli, hivyo tunajua watamchagua nani na chama gani, kitakacho weza kuwaletea maendeleo ya kweli, lakini Waislamu wa Shura ya Maimamu, ambao ni kifuchu tuu na hawajai hata kwenye fumba, waache wampigie kura mtu walioshauriwa na Sheikh Ponda.

Tena naomba kukumbushia angalizo langu hili kuhusu Muslim extremism na fundamentalism baada ya CCM na JPM kushinda urais kwa kishindo...

Security alert kwa Serikali yetu, tuwe makini sana na Marekani: Kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga Kutu-Libya?
P
 
Waaow leo nina akili fupi aisee. Hujajibu swali Genius chadema nzima,ni nani aliyewatupa uamsho huko walipo?

..Uamsho wamefungwa na JK na Babu Ali.

..lakini hiyo haimzuii Jiwe kuwatendea haki.

..miaka 7 ni mingi mno kumuweka mtu kizuizini bila kesi yake kuanza kusikilizwa.

..kama Jiwe aliweza kuwatoa kifungoni Babu Seya na Papii ambao walilawiti watoto anashindwa nini kuwatoa Mashekhe?
 
Haihusu kitu hiyo kwani Babu Seya na mwanaye ni nani aliwafunga na ni nani aliwatoa jela? Kama aliweza kuwatoa hao walawiti ni kipi kinachomshinda kuwatoa hao wa uamsho?
1602961492449.png

Waaow leo nina akili fupi aisee. Hujajibu swali Genius chadema nzima,ni nani aliyewatupa uamsho huko walipo?
 
..umetumia maneno makali.

..Lissu na mtu wa HAKI, na Sheikh Ponda ni mtu wa HAKI.
Hata lowassa nae aliitwa mtu wa haki,na wapo wengne wanamuita magufuli mtu wa haki.

Hakuna ukali wa maneno apo. Nachukia sana kuona mtu anatumia vazi la dini Kwenye upumbavu kama huo, shkh ponda ni ganda la ndizi.
 
Mbona hapa hukutia neno!? Au kwa kuwa uko busy kufukuzia teuzi? Wakifanya maccm ni sawa ila wakifanya Chadema ni makosa makubwa!!! Acha UNAFIKI wewe! Uchaguzi 2020 - Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!
Duh...!, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Viongozi wa dini, ni viongozi wa kiroho, hawapaswi kuwa amuru wafuasi wao, wamchague nani, au chama gani!, huku ni kuchanganya dini na siasa.

Maadam Taasisi rasmi ya Waislamu wa Tanzania ni Bakwata, then tunajua Waislamu wa ukweli wa Tanzania, wanataka maendeleo ya kweli, hivyo tunajua watamchagua nani na chama gani, kitakacho weza kuwaletea maendeleo ya kweli, lakini Waislamu ni Shura ya Maimam, ambao hawajai hata fumba, waache wampigie kura mtu walioshauriwa na Sheikh Ponda.

Tena naomba kukumbushia angalizo langu hili kuhusu Muslim extremism na fundamentalism baada ya CCM na JPM kushinda urais kwa kishindo...

Security alert kwa Serikali yetu, tuwe makini sana na Marekani: Kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga Kutu-Libya?
P
 
Kwahiyo mlianza na Mabeberu sasa mumehamia kwenye vibaraka?
Huyu ni mmoja wa Waislamu wanaojitambua Nchini siyo waislamu wanafiki wanaokumbatia udhalimu wa kutisha wa huyo anayejiita MWENDAWAZIMU kwa matonge machache ya UBWABWA na vibahasha vya 10,000 na 20,000. Ahsante sana Sheikh Ponda.
[emoji1421][emoji1421][emoji1421]
Maskini waislamu tunatumika kama beleshi ujenzi ukiisha tunawekwa store ewe Allah tuongoze waislamu kipindi hichi kigumu cha masheikh wanafiki wanaojipendekeza kwenye hizi siasa chafu ambazo hazina msaada wote na uislamu.

Sent from my SM-G920V using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama ni enzi za JK kwann lawama zote ziende kwa magufuli

Unajua mkuu kuna saa mnachanganya madesa mpaka wenyewe mnashindwa kujua mshike wapi muache wapi

Adui yenu mkubwa ni CCM na sio Magufuli mkifahamu hii mtaeleweka kirahisi. Lowassa alipokuja kwenu mlisingizia system. Kesho na keshokutwa nyalandu mtamsafisha(actual mmeshamsafisha)Jk akija mtamsafisha vizuri tu

Ya babu seya mlianzisha wenyewe magu akatenda msamaha baada ya uchaguzi hii ina maana chadema mliona babu seya kaonewa hakuwatendea vile watoto mkaipa kipaumbele zaidi kwenye ilani yenu
..Uamsho wamefungwa na JK na Babu Ali.

..lakini hiyo haimzuii Jiwe kuwatendea haki.

..miaka 7 ni mingi mno kumuweka mtu kizuizini bila kesi yake kuanza kusikilizwa.

..kama Jiwe aliweza kuwatoa kifungoni Babu Seya na Papii ambao walilawiti watoto anashindwa nini kuwatoa Mashekhe?
 
Yaani mtu anaetumia viongozi wa dini hasaa wa kiislamu jua kaishiwa kweli.

Waliowafunga uhamsho ni Dr Shein na JK nakuamua funguo zitupwe; wote waislamu.

Uhalisia ni kwamba kwa Tanzania bara (sio visiwani) hakuna dini iliyo tolerate kwenye kushirikiana kama ya waislamu, asilimia kubwa wanaishi Pwani maeneo ambayo washazoea kuchanganyikana na watu wa dini, makabila na rangi tofauti.

Yaani we ukisema utawatoa uhamsho ni asilimia chache sana watakao kuunga mkono kutokana na walichokuwa wakikifanya huko Zanzibar hawana support kubwa ya waislamu.

Hoja za waislamu ni kulinda namna zao za kuishi tu maswala ya ndoa, mirathi na kutaka jamii iheshimu taratibu zingine za dini yao.

Lakini we ukisema uende na demagogue wa kiislamu kama Sheikh Ponda kuropoka nae majukwaani ni kupoteza muda utapata support lakini si ya vileee, waislamu wengi Tanzania ndio wapo more tolerate kwenye jamii.

We chunguza hata JF ni mara chache sana utakuta muislamu kaanzisha mada kisa sheikh kasema jambo zuri juu ya upande wake wa siasa au anaponda kisa mchungaji kasema jambo baya kwa upande wake wa siasa.

Wengi ujitokeza na kuchangia kwenye mada ambazo namna zao za kidini zinapojadiliwa.
 
Fatilia style ya kuwatoa akina babu seya. Mliwataja kwenye ilani yenu akawapa mlichotaka. Uamsho mmewataja na mmemtumia ponda mkilaumu utadhan Magu ndie aliyewafunga. Adui yenu ni CCM kwa wengine tunzeni akiba ya maneno maana hamfahamu mwenye chama anawaza nini dakika yoyote anasafisha mtu kama lowassa.
Haihusu kitu hiyo kwani Babu Seya na mwanaye ni nani aliwafunga na ni nani aliwatoa jela? Kama aliweza kuwatoa hao walawiti ni kipi kinachomshinda kuwatoa hao wa uamsho? View attachment 1603443
 
Na hiyo ndiyo maana halisi ya maneno SASA BASI!!!

Lissu ataandikwa na kukumbukwa vizazi na vizazi Rais wetu
 
...ata lowassa nae aliitwa mtu wa haki,na wapo wengne wanamuita magufuli mtu wa haki...

Hakuna ukali wa maneno apo.......nachukia sana kuona mtu anatumia vazi la dini Kwenye upumbavu kama huo,shkh ponda ni ganda la ndizi.

..itabidi sasa uzoee mazingira mapya ya viongozi wa dini kupiga kampeni za kisiasa.

..ccm ndio walioanzisha utaratibu huo kwa kutumia kamati ya amani ya viongozi wa dini, wapinzani wao wanaiga tu.
 
Shekhe Ponda ni Shekhe jasiri sana CCM walipanga auwawe pale Morogoro kwa mshangao wa wengi Shekhe akazikwepa risasi kininja

Huyu Shekhe ni kaliba ya Lissu kama Lissu kaamua kumchukua Shekhe huyu ili amalizie nae kampeni basi ni jambo zuri sana
Ponda ndo ameshamaliza kazi hivyo. Ni kiongozi wetu na ametutia shime kuwa na msimamo thabiti. Lissu tutakufa na kupona nae!!!
 
Back
Top Bottom