Kisiju mkoani Pwani watu wanaswali kuliko kazi

Kisiju mkoani Pwani watu wanaswali kuliko kazi

Nipo Kisiju idadi ya misikiti Ni mingi kuliko shule na hospitali. Wananchi wanaswali kuliko shughuli za kuingiza kipato. Kiuchumi hii ipoje? Kilimanjaro wenzetu wanapiga kazi na kulipa kodi. Hapa Kisiju ni tofauti Sana
SWala ndio kila kitu kwa muislamu, ni vyema kumkumbuka muumba wako , inakuwaje binaadamu unachukia na kuhoji kisa mwenzako anamkumbuka na kumuabudu muumba wake?
 
Kule hakufai kabisa. Pamesaharika sana. Watu hawaendi shule, badala yake ni Madrasa, akipiga zake Madrasa miaka minne tayari ni msomi wa heshima.
Kinywaji adui kuliko vyote kule ni 'Fanta'[emoji2]. Fanta ina historia yake kuke[emoji3]
Mkuu fanta ilifanyaje [emoji1787]
 
Kama hujui kitu tulia

Mbona una hasira za ghafla wee jamaa. Hivi unajua mitaa ya Tanzania yote wewe? Kama ambavyo wewe hujui kila eneo nchi hii basi na wenzako kuna maeneo hawayajui. so usimcheke mwenzako. Anyway, mimi nimeamua kutumia google isiwe kesi. Kisiju ni kata iko wilaya ya Mkuiranga. Haya na wewe naomba nikuulize ku na sehemu inaitwa Vunta unaifahamu?
 
Mkuu fanta ilifanyaje [emoji1787]
Ilikua ni kabla ya mwaka 1993. Inasemekana kuna ngalawa au mtumbwi ulipunduka huko Commoro, sasa kama ilivyo kawaida, watu wa Pwani wana msemo unasema bahari haikai na uchafu.

KIle chombo kilichozama kilikua na mzigo mkubwa tu, mzigo ule ulisukwasukwa na mawimbi hadi mizigo mingine ikatokea Pwani ya Kisiju. Katika mzigo ule kulikuwepo na vinywaji vilivyokuwa kwenye kopo.

Pakawa na udadisi sana kuhusiana na kilichokuwemo mule ndani. Hapo mzigo upo mikononi mwa wazee wanao heshimika na kule wazee wanaoheshimika na Shehe, Imam, Ostaadhi na wengineo ambao ni viongozi kwenye dini na wazee ndani ya jamii😀.

Wakati wanajiuliza kuhusu kilichomo mwenye vikopo vile, ikabidi akatafutwe kijana mmoja ambaye ndiye allikua ni mjanja mjanja pale Kisiju maana alikua ni mtu wa kuvuka sana, yaani kwenda sana mjini😀 (Mbagala na Mkuranga 1991 - 1993)😃.

Kijana alipoitwa, akawekwa kati na wazee ambapo wakamuuliza kuhusu vile vikopo. Kijana wa mjini alipoviangalia, akawaambia "aaah hizi ni fanta, ni soda tamu sana hizi" kijana akafungua, akaonja mbele yao akaomba na vikopo kadhaa aondoke navyo wakampatia vikopo vinne akasepa.

Wale wazee kwa kuwa palikua na cartons za kutosha wakaugawa ule mzigo haki bin haki na hata wasiokuwepo wakapelekewa. Basi wazee ma Mwinyi wakaanza kunywa fanta kikopo kimoja baada ya kingine.

Ikafika muda wa azana kimya, muda wa azana nyingine kimya...wanaanza kutafutwa viongozi msikitini wote hawapo, kuanzia Muazini hadi Mnadi swala, waumini ni mmoja mmoja. Walipowafuata majumbani wanakuta watu hawajitambua, kuja kustuka na kurudiwa na akili ni kesho yake.

Ikabidi kiitishwe kikao waulizane ni kipi kilitokea na yule kijana mtaalamu wa mjini naye akaitwa. Wakamleta wamembeba. Maana yeye baada ya kikopo kimoja alitulia , siku hiyo asubuhi ndiyo akanywa.

Yule kijana akaulizwa ina maana wakinywa fanta ndiyo inakuwa vile? Katika vitu viliwakwaza na kuwakasirisha wale wazee ni siku kupita bila azana na kwa ukubwa wa mzigo karibu waumini na wananchi wengi walikua bwii. Wakiulizwa nini kimetokea wanajibu kwa sauti ya kilevi "Fantaa", wakiulizwa ndiyo nini na imefanya nini wanajibu tena "Fantaa".

Katika kujadiliana Ilibidi wazee wafikie muafaka wa kuipiga marufuku Fanta pale Kisiju, na hatua kali kuchukuliwa kwa yeyote atakayekutwa anakunywa au hata kuileta Fanta pale Kisiwani.

Kumbe walichokuwa wamekunywa siyo Fanta bali ni beer aina ya Stella Artois ya vikopo ambayo ilikua maarufu sana miaka ile😃
Screenshot_20231015-005139_Google.jpg
 
Kuswali sana sio shida.

Labda kama kuna viashiria vya ushirikina.

Jamii nyingi zinazoendekeza ushirikina zinapumulia mashine kwa hali mbaya.
 
Sasa yanini kumshindanisha na Bakhresa kisa Bakhresa anaswali swala tano wakati wewe mwenyewe swala tano hauko kama Bakhresa.

Kama kuswali ndio kungekuwa kunaleta hela mbona masheikh wangekuwa matajiri sana.
Na aliyesema kuswali akuleti pesa kwa sababu tunapoteza muda unamchukuliaje?

Kama kuswali kunapoteza muda kwanini kina Bakhresa na mimi bado tuna pesa pengine za kuulisha na kuuvisha ukoo wenu wote kwa karne?

linapokuja suala la kufikiri jambo lolote linalowahusu waislamu mnatanguliza sana hisia mbele kuliko facts.
 
Nipo Kisiju idadi ya misikiti Ni mingi kuliko shule na hospitali. Wananchi wanaswali kuliko shughuli za kuingiza kipato. Kiuchumi hii ipoje? Kilimanjaro wenzetu wanapiga kazi na kulipa kodi. Hapa Kisiju ni tofauti Sana
Siyo kweli, Kiislam sala ni mara tano kwa siku, popote kule.

Labda ulienda siku ya ijumaa ambapo wengi hupenda kuwahi msikitini na kuchelewa kutoka sala ya Ijumaa. Hiyo ni kote duniani, siyo Kisiju tu.

Aisee, upo kwetu kabisa, chimbuko langu huko.
 
Back
Top Bottom