The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Ni wakati sasa Maxence Melo atoe tamko la hakikisho la kutotoa siri za wateja wake kwa vyovyote vile!Au kama atatoa zikihitajika basi ni vema aweke wazi ili watu tujipange na wengine wakachome moto simu zao!
Inaweza kuwa ni sawa. Lakini "TAMKO" tu halitakuwa na msaada wowote.
Kumbuka hii ni hukumu halali ya mahakama bila kujali imetolewa kihalali ama kimizengwe zengwe na hukumu yoyote ya mahakama haitenguliwi na tamko tu la mtu yeyote.
Ili kuisaidia JF na mmiliki wake Maxence Melo, ni sharti tumtie moyo akate rufaa mahakama ya juu ili iweze kutengua hukumu hii.
Hili linaweza kufanyika kwa njia zozote zile zinazokubalika ikiwemo sisi wanachama kuchangia sehemu ya gharama.
Kama mahakama ya rufaa ita - side na mahakama kuu, then hatutakuwa na namna yoyote sisi sote pale itakapotokea mwanachama wa JF ameitia serikali na Magufuli vidole machoni.
Katika hatua hii, hata Maxence Melo, hatatusaidia kwa lolote wanachama wake isipokuwa ni sharti tucheze mziki kwa "tune" ya watawala wanayoitaka wao!