Kisutu, Dar: Robert Kisena apandishwa Kizimbani kwa Utakatishaji fedha, asomewa mashitaka 33

Kisutu, Dar: Robert Kisena apandishwa Kizimbani kwa Utakatishaji fedha, asomewa mashitaka 33

Huyo jamaa amewekwa mtu kati, siku akikubali kuachia wanavyotaka wenyewe wataachana nae, na watafanya hivyo muda wowote, naamini hata hiyo kesi ni mojawapo ya njia za kumtisha ili awapishe.
Kumbuka ni kesi ya 2019 so msitake kusingizia watu
 
Lugumi, kisena, gwajima, mpina hawa ni wasukuma wajanja wajanja pamoja na lafudhi mbovu lakini wako kimjini ukizubaa unaliwa kichwa kama kawaida
Lugumi mzee wa tenda za silaha..haya majamaa yanatengezaje pesa mjini?

#MaendeleoHayanaChama
 
Usimtete huyu mwizi mshirika wa Ridhwani Kikwete kwenye miradi yao ya wizi wizi!! Hawa ndio walifirisi UDA kwa mambo yao ya kifisadi enzi ya Kikwete wakishirikiana na Marehemu Idd Simba na Alhaj Profesa Juma Athumani Kapuya!! Genge na Vasco Dagama!!
Mwendazake alimuacha pale Kwa sababu ni Msukuma wa kwao.
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (UDART) Robert Kisena na wenzake watatu wamesomewa mashtaka 33 katika kesi mbili tofauti kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwemo Utakatishaji wa fedha na kuongoza genge la uhalifu.

Kwenye kesi namba 21 ya mwaka 2022 inawahusu Kisena na wenzake wawili ambapo ni Charles Newe na Tumaini Kulwa wanadaiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu kaisi cha cha Shilingi 4.5 Bilioni huku wakituhumiwa kutakatisha na kusababisha hasara serikali kiasi hicho hicho.

Katika kesi namba 20 ya mwaka 2022 Kisena na washtakiwa wanne akiwemo Newe, Kulwa na Jonhn Samangu wanadaiwa kutakatisha kiasi cha Shilingi Milioni 750 ambazo zinadaiwa kuwa ni zao la kughushi na kulaghai.

Washtakiwa hawakuwa na haki ya kujibu chochote kwa Mahakama hiyo kwani haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo kisheria.

Watuhumiwa wamerejeshwa mahabusu ya magereza mpaka tarehe 23 Mei 2022 shauri hilo litakapotajwa.

Wote Wamekosa dhamana.

=====

UPDATES;

======

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo haraka, maarufu mwendokasi (Udart), Robert Kisena na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 33 yakiwemo ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia hasara Serikali ya Sh 5.2 bilioni.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu Mei 9, 2022 na kusomewa kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi mbele ya mahakimu wawili tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la mawakili watano wandaamizi wa Serikali wakiongozwa na Pius Hilla akisaidiana na Jackline Nyatori, Ester Martin, Iman Mitumemingi na Upendo Temu.

Mbali na Kisena, washtakiwa wengine ni Charles Newe (48) Mkurugenzi wa Udart, mfanyabiashara John Samangu (66) na Mtunza fedha Tumaini Kulwa (44).

Septemba 13, 2019 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) aliwafutia mashtaka manne ya utakatishaji fedha washtakiwa hao na hivyo kubaki mashtaka 15 kati 19.

Kati ya mashtaka hayo 15 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa hao, yapo mashtaka manne ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo; manne ya wizi; moja kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja ni kusababisha hasara UDART.

Mengine ni kuongoza genge la uhalifu, kujenga kituo cha mafuta ya petroli bila kibali kutoka Ewura na kuiba.

Chanzo: Mwananchi
View attachment 2218107View attachment 2218108View attachment 2218109
Mbwembwe nyingi hukumu ikitoka wanakaa gerezani miezi mitatu kisha wanaachiwa huru
 
Ngoja utasikia mwendelezo wa hii kesi!! Kesi ngapi za kusisimua umezisoma magazetini halafu ziiiiiiiiii huzisikii tena? Nchi hii inaongozwa na wahuni !
Kisha itabidi walipwe fidia kwa hasara waliyoipata !!
 
Na wale wananyonya mafuta yetu pale kigamboni na kuyafungulia ndani kwao kama maji, mliwapiga fine ya laki saba kimyakimya pale kisutu alafu mkabadilisha na RPC aliyetaka kufuatilia kipindi tukiwa busy na Sabaya Arusha..wakamatwe haraka sana.
 
Hilo pozi lake la kijinga ndio litakalowaponza yeye na wenzake.
Mahakimu wetu ni very emotional. Unaweza pewa mvua kwa kutotamka neno muheshimiwa. Hilo pozi ajiandae kuwa nalo Segerea.
Obvious hapo hakimu alikuwa hajaingia court hawezi kukaa hivyo mbele ya hakimu
 
Back
Top Bottom