Kisutu: Kesi ya kuvunja gereza la Segerea inayowakabili viongozi wa CHADEMA yafutwa

Kama wewe unajua zaidi si ungeenda kuwa shahidi
 
Mama samia aliishatoa muelekeo wa kuachana na kesi zote za kipumbavu zilizoanzishwa na utawala wa hovyo uliopita. kwa nini utekelezaji hauonekani?
Kesi ya kipumbavu kuvamia gereza? Kumchania afande sare?

Ulimuelewa mama alimaanisha nini?
 
Serikali yenye maadili hulinda na kuitetea katiba na huhakikisha kuwa hakuna mtu anaekuwa juu ya sheria. Hii ina maana kuwa mtu akivunja sheria anapelekwa mahakamani na kisha anapata haki yake.

Watu walifanya vurugu na kuingia eneo la gereza lisiloruhusiwa. Ushahidi upo na mbaya zaidi walimchania sare askari magereza. Mashahidi wakuu ni haohao maaskari magereza.

Kwa nini msipeleke mashahidi ili waliovunja sheria wapate haki zao?

Au sababu mmewapa ubunge wa kwenye sinia ndio maana mnawabeba hata wakivunja sheria?

Huku ni kukosa maadili ambako hakufai kabisa.
Mkuu kama adi leo unaamini kwamba ni kweli walivunja sheria na wameachiwa huru itabidi ufikirie tena. Gerezani ni mahali penye ulinzi mkali haiwezekani kikundi kidogo kama hicho wakavunje geti la gereza mbele ya askari wenye silaha, tena wavunjaji wenyewe hawakuwa hata na koleo mkononi. Hayo yalikuwa maigizo yenye malengo maalum na lengo limesha timia wenye macho wameona na wenye masikio wamesikia.
 
Serikali yenye maadili hulinda na kuitetea katiba na huhakikisha kuwa hakuna mtu anaekuwa juu ya sheria. Hii ina maana kuwa mtu akivunja sheria anapelekwa mahakamani na kisha anapata haki yake.

Watu walifanya vurugu na kuingia eneo la gereza lisiloruhusiwa. Ushahidi upo na mbaya zaidi walimchania sare askari magereza. Mashahidi wakuu ni haohao maaskari magereza.

Kwa nini msipeleke mashahidi ili waliovunja sheria wapate haki zao?

Au sababu mmewapa ubunge wa kwenye sinia ndio maana mnawabeba hata wakivunja sheria?

Huku ni kukosa maadili ambako hakufai kabisa.
Mkuu kuna mtu alitolewa gerezani usiku wa manane kwenda kuwa mbunge bila order ya mahakama, itoshe tu kuelewa hivyo.
 
Back
Top Bottom