Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Mwalimu anafundisha huku anajidekeza.Wanaita swaga.Hana misisitizo wala umakini na umahiri.Bure kabisa hadi keshokutwa asubuhi.Siku hizi walimu wenye ni mabishoo halafu ni VILAZA hatari
Oxford nao wamekosea?Kama tunavyosema hapa, unaweza kushangazwa sana unapokutana na taasisi kubwa kama TUKI nayo inaboronga Kiswahili.
Wamekosea, hilo si neno sahihi.
Duh! 🤣😀🤣Wengi wanafupisha neno KWAHIYO kwa kusema KO.
Ko vipi sasa?
Ko unakuja au?
Hivi ni viswahili vya watu wasio na upeo wa kitaaluma au kielimu A.K.A MANGUMBARU / MABICHWA KOMWE.
Ko ndo kasema kwahiyo‘Kwaiyo-ko’ maana yake nini?
Yani inanikeraga mno 😀Wengi wanafupisha neno KWAHIYO kwa kusema KO.
Ko vipi sasa?
Ko unakuja au?
Hivi ni viswahili vya watu wasio na upeo wa kitaaluma au kielimu A.K.A MANGUMBARU / MABICHWA KOMWE.
Sikiliza hii video kuanzia dakika ya 1:26 hadi 2:06 jiulize public kiasi gani inaharibiwa [WARARAMIKAJI]Maneno mazuri ya kiswahili yamepindishwa kiasi inaleta kichefuchefu hata kusikiliza. Hapa nitaweka baadhi ya maneno.
Alikuwa = alikua
Kwa hiyo = ko
Baadhi = baazi
kufanikiwa = kujipata
sasa = saivi
Ndio hivyo = ndoivo
Ndio nini = ndonini
serikali = serekali/selekale
yaani = yani
mtaa = kitaa/kitaani
kwa sababu = co
Pasipo kuchukuliwa hatua za makusudi lugha hii inaelekea kupotea.
Siwezi kubisha sana kwenye hili, lakini ukweli kabisa, mzizi sahihi wa Kitenzi ONA ni "ON".Oxford nao wamekosea?
Hapana, wote hawajakosea. Wako sahihi.
Pia, zote, ‘onyesha’ na ‘onesha’ ni sahihi.
Kwa nini zote ni sahihi? Jibu ni lahaja.
Kiswahili kinazungumzwa Afrika Mashariki na Kati.
Hili ni eneo kubwa. Hivyo suala la lahaja za lugha haliepukiki.
Kimvita [Kiswahili cha Mombasa na pwani ya Kenya] kina tofauti za hapa na pale katika matamshi na tahajia za maneno na Kiswahili cha bara.
Mfano, ile mboga uijuayo wewe kama ‘biringanya’, kule Mvita na baadhi ya sehemu za Congo, inaitwa ‘biringani’.
Kuna baadhi ya maeneo namba 0 huitwa ‘sufuri’ na kwingineko huitwa ‘sifuri’.
Hata Kisukuma kina lahaja. Kinyantuzu, Kisukuma cha wenyeji wa Simiyu, kina utofauti na Kisukuma cha wenyeji wa Shinyanga
Mfano, kijiji cha ‘Gambosi’, watu wa nje huwa wanakiita ‘Gamboshi’.
Matamshi yote yanakubalika.
Hata Kiingereza kiko hivyo hivyo.
Mfano, neno ‘schedule’, kwa Marekani hutamkwa tofauti na litamkwavyo Uingereza na kwingineko kutumiako Kiingereza cha Uingereza.
Hata kwenye tahajia, kuna maneno huandikwa tofauti. ‘Center’ na ‘centre’ yote ni sahihi.
‘Defense’ na ‘defence’ yote ni sahihi pia.
Hivyo, ‘onyesha’ na ‘onesha’ nayo yote ni sahihi. Ni suala la lahaja tu.
Na ndo maana yote yapo kwenye kamusi zote za Kiswahili sanifu [ambazo ninazo na ambazo nimewahi kuziona].
Sikuwa na nia ya kujivika ualimu wa isimu matumizi. Ila, wakati mwingine inabidi tu iwe hivyo ili kutoa somo ambalo linaonekana kuwaepa watu wengi.
Kamusi hutungwa na wataalamu wa lugha waliofanya tafiti za kutosha. Sidhani kabisa kama wataalamu wote hao wa Kiswahili, kutoka Afrika Mashariki na Kati, wakakosea kuliweka neno ‘onyesha’ na kutoa fasili yake, katika hizo kamusi za Kiswahili.
Kwenye lugha, neno moja kuwa tofauti katika matamshi na tahajia, ni jambo la kawaida sana, kwa kuzingatia muktadha wa lahaja.
Unatutusi kaka, na kweli ukicheki movie jinsi wenye lugha yao wanavyoongea na kina sie wa kidum na fagio ni tofauti kabisa 😂😂.Sio vizuri kuwa na kaida katika lugha ya mazungumzo . Lugha sanifu inaweza kutumika katika maandishi na katika maandiko rasmi. Ukiongea Kama Kiswahili kinavyotakiwa kuandikwa utaongea Kama kingereza Cha watanzania they talk like a book Yani wazungu wanashangaa Sana😆 afu utakuta lijitu linajinasibu linajua kingereza kumbe linaongea lugha ya kiuandishi😆
Ukitumia ‘onesha’, ni sahihi:Siwezi kubisha sana kwenye hili, lakini ukweli kabisa, mzizi sahihi wa Kitenzi ONA ni "ON".
Kutoka kwenye "ON" ndipo unapoweza kukinyumbua kitenzi kwenye muelekeo uutakao.
Kama ni lahaja sijui, na sijaelewa hii lahaja ya "ONYESHA" ni ya nchi gani au eneo lipi la kijografia!
Na ukumbuke pia lahaja zote za Kiswahili zilisawazishwa (standardized) tukapata lahaja ya sasa ya KISWAHILI SANIFU.
Na kwa ufahamu wangu usio na mashaka wala ubabaishaji, neno sahihi ni ONESHA.
Lakini pia ONYESHA linaweza kuwa sawa kwa hoja ulizozitoa. Lugha inapanuka na kukubalika kulingana na mazingira au mazoea.
Sipingi. Mimi nitaenda na ONESHA.
Dah!BICHWA KOMWE -
Nyani Ngabu
Nilitamani kulia Bado nimpe ela Bado ananiambia koh😀😀😀
View attachment 2967519
Nimehariri ujumbe wangu wa juu hapo, kuna jambo ukilisoma upya utanielewa uzuri zaidi.Ukitumia ‘onesha’, ni sahihi:
Atakayetumia tumia ‘onyesha’, naye atakuwa sahihi.
Sijui uko wapi. Ila kama upo Tanzania, kama unaweza, nunua kamusi ya Kiswahili sanifu, hususan ya toleo lililo jipya [2023/2024], halafu uyaangalie hayo maneno usome na maelezo yake.
Ukikuta ni tofauti na maelezo niliyokupa, rudi hapa unitafute 😀.
Jingine, lahaja huwezi kuzisawazisha. Kinachofanyika ni kuzikubali tu tofauti zilizopo. Na ndo maana kwenye Kiingereza, kwa mfano, ukilitamka neno schedule kama ‘skedyul’ au ‘shedyul’, vyote ni sawa tu maana matamshi yote ni sahihi.
Lugha na misamiati yake husawazishwa na matumizi ya watumiaji wake. Siyo taasisi.
Kwani unadhani Kiingereza walichokuwa wanaongea Waingereza miaka 800 iliyopita ni sawa na Kiingereza cha leo?
Hata Kiswahili cha leo si sawa na Kiswahili cha miaka 200 iliyopita na hakitakuwa sawa na Kiswahili cha miaka 200 ijayo.
Lugha huwa ina evolve.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣BICHWA KOMWE -
Nyani Ngabu
Nilitamani kulia Bado nimpe ela Bado ananiambia koh😀😀😀
View attachment 2967519
😂😂😂Koh ningefanyaje Sasa nilijibu tu poa yaishe🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Koh sasa uliamua kufanyaje?
Sipo nyumbani sasa hivi. Nikirudi nitakuwekea picha ya ukurasa yenye neno ‘onyesha’ na fasıli yake toka kamusi tatu tofauti zilizochapiswa na taasisi tofauti.Nimehariri ujumbe wangu wa juu hapo, kuna jambo ukilisoma upya utanielewa uzuri zaidi.
Usawazishaji wa Kiswahili hapa Afrika Mashariki ama kama wengi wanavyoita Usanifishaji wa Kiswahili, sio HADITHI, ni mchakato rasmi uliofanywa na Wajerumani na ukaendelezwa baada ya uhuru baada ya kuzuka mtafaruku wa kimawasiliano hususani pale ambapo Wajerumani walitaka kukitumia Kiswahili mashuleni.
Kwahiyo, usawazishaji wa Kiswahili ni kitu halisi kilichofanyika, na kwa minajili hiyo, Lugha sanifu ya Kiswahili iliyotambulika ni ile ya lahaja ya Kiunguja na marekebisho yake machache.
Lahaja zingine ziliendelea kubaki na kutumika lakini hazikutambulika kama lahaja sanifu.
Na nikurudie tena kwa kusema kwamba, "onesha" na "onyesha" yote yaweza kuwa sahihi, lakini pia kuna uwezekano TUKI wakawa wamekosea pia. Sijasema wamekosea, nimesema wanaweza kuwa wamekosea.
Lolote linawezekana, lakini mimi kama mtaalamu wa lugha asiye na ukanjanja, siku zote ninaamini kuwa, MZIZI WA KITENZI ndio msingi wa usanifu wa kitenzi hicho pamoja na unyumbuaji wake.
Maneno ya mfano uliyoyataja hapo juu ni NOMINO si Vitenzi, kwahiyo ni vigumu kubaini au kupinga usahihi wa lahaja za NOMINO kuliko usahihi wa lahaja za VITENZI kwa sababu VITENZI vinapimwa usahihi wake kwenye MIZANI MADHUBUTI YA MNYUMBULIKO WA VITENZI.
Kama mzizi wa neno "ONA" ni "ONY" basi uko sahihi, Lakini kama mzizi wa neno ONA ni "ON" basi nitakuwa sahihi.
Unaweza ukasema "gari limeONYekana? HAUWEZI!
Kwanini? Kwa sababu huo si mzizi sahihi wa kitenzi "ONA". Na kwa sababu hiyo, mzizi huo hauwezi kunyumbulika kwenye maneno mengine pia kama "oNYesha".
Kwa hiyo iwe "kwahiyo'. Ni neno mojaKwa utafiti wangu mdogo hakujawahi kutokea matumizi mabovu ya lugha ya kiswahili kama muda huu tulionao.
Kibaya zaidi hata baadhi ya vyombo vya habari vikubwa vinashiriki dhambi hii.
Maneno mazuri ya kiswahili yamepindishwa kiasi inaleta kichefuchefu hata kusikiliza. Hapa nitaweka baadhi ya maneno.
Alikuwa = alikua
Kwa hiyo = ko
Baadhi = baazi
kufanikiwa = kujipata
sasa = saivi
Ndio hivyo = ndoivo
Ndio nini = ndonini
serikali = serekali/selekale
yaani = yani
mtaa = kitaa/kitaani
kwa sababu = co
Pasipo kuchukuliwa hatua za makusudi lugha hii inaelekea kupotea.
Chanzo kikuu cha haya ni uholela wa vyombo vya habari hasa habari za mtandaoni.
Nashauri mambo makubwa mawili yafanyike kwa haraka.
Kuwe na takwa la lazima kwa waleta habari kwa jamii wote kuwa na ufaulu mzuri wa lugha hii
vyombo vya habari vyote yaani vya kawaida na mitandaoni lazima visajiliwe kwanza na mamlaka za kiserikali kabla ya kuanza kupeleka habari yoyote kwa jamii.
Tuungane pamoja kuinusuru tunu yetu kuu ya lugha ya kiswahili
Neno "nikuchane" kwa namna ulivyolitumia hapa na maana yake halisi kwenye kamusi ya Kiswahili ni sawa??????huu ni uhuni kabisa.
Ukituma ujumbe kwangu wa hivi lazima nikuchane.