Hivi nchini Kenya kuna wana vijiji ambao hawakusoma, lakini wanazungumza kingereza kama lugha yao ya pili au kingereza ni lugha ya wasomi tu? Nisaidie Mkuu.
Haya makelele ya utumiaji wa Kiswahili mbona huwa hamyaelekezi kwa majirani wenu wengine, kama vile Msumbiji, Malawi n.k.
Kila siku mnalialia eti Wakenya Kiswahili hawakitaki.
Inafaa iwaingie kama jinsi nimesema mara nyingi humu, kwamba Wakenya tunaongea lugha nyingi na ni vigumu kutufuga kwenye zizi moja kama alivyofanya Nyerere kwa Watanzania. Kenya tuna uhuru wa kutumia lugha tunazotaka bila shinikizo lolote.
Kiswahili tunakipenda, lakini pia tunapenda lugha zetu za asili na tunazitumia sana pamoja pia na lugha za kigeni kama Kingereza.
Utafiti umedhihirisha kwamba uwezo wa kutumia lugha kadhaa huwa unaboresha mtu hata kifikira.
Halafu mambo ya ubaguzi wa kikabila au aina yoyote ile hauletwi au kuzuiwa na lugha, maana Somalia kule wanaongea lugha moja, dini moja lakini hawana nchi, kutwa kulipuana na kuchinjana. Kuna matukio mengi hata ya kihistoria ambapo watu wanaotumia lugha moja ila walichinjana tu, nenda hata hapo Rwanda.
Ubaguzi upo kwenye fikira na mawazo ya mtu, nyie hapo kuna chembe chembe za ubaguzi kwa misingi ya dini, kitu ambacho nimekiona na sio kuhadithiwa wala nini. Hivyo hapa kwetu tunajaribu jinsi nyingi za kumaliza ubaguzi wa ukabila ambao uliletwa na mzungu hata kabla hatujapata uhuru, mzungu alitugawa kwenye divide and rule mechanism. Kwenu hakua na haja maana alihodhi nchi kutoka kwa Mjerumani hivyo alijua ataachia na hakua na nia ya kung'ang'ania.