Neo-colonialism on freak! Sio siri kuwa wakenya bado mnatawaliwa kifikra na waingereza! Ndio maana mnaona English ndo kila kila kitu! Huu ni ujuha wa kiwango cha PhD!
Ndugu yangu, mataifa yanayojitambua yanatumia lugha zao za asili, bila kujali udogo wa lugha hizo, angalia Korea, Japan, Hungary, China Myanmar nk bado wanazitumia!
Halafu wewe na ukubwa wako huo bado unadiriki kusema eti ndivyo tulivyolelewa hivyo, bila kujua ni akina nani hao walio walea hivyo! Wakoloni; waliwaaminisha hivyo nanyi kwa kutojitambua mkakishadadia bila kutumia akili zenu!
Tukiongelea kigezo cha lugha, Tanzania tuko superior kuliko nyie, Maana sisi tunathubutu kuongea kiswahili chetu mbele ya mataifa mengine, kitu ambacho nyie hamuwezi kwa dhana za kikoloni zilizojaa vichwani mwenu! You are so inferior to embrace your true Africanism!
Wewe ukijitapa kila mtaa na kujisifu eti unajua kuongea kiingereza sanifu, mwingereza yeye asemeje kwa mfano? Atajifunza nini akija kitalii kwenye nchi yako?
Sisi tunaendelea kupiga hatua kukikuza kiswahili, nyie endeleeni kumsaidia mkoloni kueneza kiingereza!
1.Tumefanya jitihada hadi kiswahili kimekuwa official language AU,
2. Rwanda walivyoona hii lugha inazidi kukua, wameifanya kuwa lugha rasmi ya taifa lao.
3: Vyuo vya kufundisha kiswahili vinaendelea kuongezeka nchi za ulaya, marekani na asia.
4: Kiswahili sasa hivi kinashika nafasi ya 13 kwa kuwa lugha yenyenushawishi mkubwa
The 25 Most Influential Languages in the World
5:Kiswahili kinashika nafasi ya 16 kwa kuwa lugha yenye wazungumzaji wengi duniani
List of languages by total number of speakers - Wikipedia
Sasa wewe endelea kushadadia ukoloni ma kuona eti ndio ujanja