MWANDENDEULE
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 4,099
- 7,466
hivi ni dhamani ama ni thamani? lugha nayo...
anaelevusha= anaerevusha.
welevu= werevu
Mie nafahamu ni Dharura na sio kama unavyo sema.
Hii hapa ni kamusi ya TUKI.
Tatizo hili naona limekuwa kubwa sana kwenye matumizi ya kawaida na wakati mwingine hadi kwenye matumizi Rasmi ya Lugha yetu ya Kiswahili. Inanonesha kwamba watu wengi labda kutokana na Lugha zao za asili wanashindwa kabisa kutofautisha matumizi ya her " L " na " R " wakati wanafanya uandishi wa maandiko yao.
Mtu badala ya kuandika "Jaribu" yeye ataandika "Jalibu", au wengi wetu hatuwezi kuandika "Dharula" badala yake tunaandika "Dharura" na mengine mengi yanayohusisha matumizi ya herufi hizo mbili.
Mr. Prezidaaaa = RaisHehehehe Mr. Prezidaaaa tumsamehe tu maana ile ngoma ya sukumaland haiwezi kuchange.
Mr. Prezidaaaa = Rais
Sukumaland = Usukumani
Kuchange = Kubadilika
*Wasukuma wengi tu wameweza kubadilisha matamshi yao
Mr. Prezidaaaa = Rais
Sukumaland = Usukumani
Kuchange = Kubadilika
*Wasukuma wengi tu wameweza kubadilisha matamshi yao
Umeanza,
Haya sasa umekua mzee kifimbo cheza.
Unajua tupo kwenye jukwaa la lugha sio sahihi kuandika 'kiswanglish'
Umesahau kusahihisha na "Ngoma"
Tupo kwenye jukwaa la lugha ya kiswahili au jukwaa la lugha???
'kiswanglish' pia lugha.
Hilo ni tatizo la wengi aisee..Afadhali mtoa mada umedhihirisha ilo pia
Asante SaaMbovu.
Bwa Allen Kilewella mimi ni mzaliwa wa pwani ambaye nimekulia pwani, kiswahili ni lugha yangu na sina nyengine kabisa, na nimesoma kiswahili na kupasi vizuri mpaka form six.
Sijawahi hata siku moja kusikia mswahili akiita dharula.
Basi lugha yoyote iandikwe kwa ufasaha
'Kiswanglish' sio lugha, kwa mfano ulivyoandika 'kuchange' badala ya 'kubadilika' ni kutaka kuwajulisha wengine kuwa umezoea kutumia lugha la Kiingereza kuliko Kiswahili, kitu ambacho kinaua lugha yetu ya Kiswahili
Mzaliwa wa Pwani acha kuandika 'kiswanglish'Asante SaaMbovu.
Bwa Allen Kilewella mimi ni mzaliwa wa pwani ambaye nimekulia pwani, kiswahili ni lugha yangu na sina nyengine kabisa, na nimesoma kiswahili na kupasi vizuri mpaka form six.
Sijawahi hata siku moja kusikia mswahili akiita dharula.