Ukisoma kitabu cha Enoko, anasimulia kuanzia mwanzo mpaka mwisho, jinsi alivyotokewa na malaika wawili, na kama ilivyo kwa malaika wote wanapowatokea wanadamu huanza na neno “Usiogope”.
Kwa nini?
Ni kwa sababu malaika ana muonekano wa kutisha, kwa binadamu, huwezi kuwa kawaida tu unapomuona malaika ametokea mbele yako, ndiyo maana husema usiogope.
Aliambiwa Mariamu Magdalena pia.
Enoko alianza kuwaelezea malaika ambao walikwenda chumbani kwake wakati amelala.
Kwanza walikuwa wakubwa, wenye mbawa lakini sura zao zilikuwa na mng’ao mkubwa kama jua lakini macho yao yalikuwa yanawaka kama taa.
Katika maisha yake, anasema hakuwahi kuwaona viumbe wakubwa namna hiyo.
Lipsi zao zilikuwa na moto, mbawa zao zilikuwa na mchanganyiko wa rangi mbili, zambarau na dhahabu inayong’aa kupita kawaida, mikono yao ilikuwa ni meupe kama theluji.
Hebu fikiria unakutana na kiumbe kama hicho, hutoogopa? Ndiyo maana walimwambia kwanza, usiogope.
Anasema malaika hao walisimama pembeni ya kitanda chake na kumuita kwa jina lake, Enoko akainuka na kuwaangalia.
Enoko aliogopa, anasema uso wake ulitetemeka mno lakini malaika mmoja akamwambia: “Usiogope”.
Walimwambia walitumwa na Mungu kumchukua na kumpeleka mbinguni, kwa yote ambayo angekutana nayo huko basi angewaambia watoto wake, wajukuu na vizazi vyote mbeleni.
Anasema hakutaka kuwapinga, akatoka na kwenda kuonana na watoto wake, Mathusal, Regim na Gaidad, akawaambia kuhusu malaika hao na kile walichomwambia, baada ya hapo, wakamchukua na kuanza kupaa naye kwa kumbeba kwenye mbawa zao.
View attachment 3134566