Kitabu cha Erick Kabendera: Ni vema atoe ushahidi wa tuhuma alizochapisha kuhusu Magufuli kuhusika kifo cha Ben Saanane

Kitabu cha Erick Kabendera: Ni vema atoe ushahidi wa tuhuma alizochapisha kuhusu Magufuli kuhusika kifo cha Ben Saanane

Huyu jamaa kazua kizaazaa naona mitandao yote inajadili kitabu cha kabendela ameamua kujitoa mhanga
Uzuri watanzania sio wanunuzi wa vitabu hawapendi kusoma tabu lake labda awauzie wazungu

Lakini kwa Tanzania asahau akiuza copy 500 aniiite mbwa koko

Soko la vitabu kama hicho chake halipo Tanzania

Akitarajia kutajirika kupitia hilo tabu lake soko Tanzania halipo
 
354 pages of sanctimoniousness so sad
chrome_screenshot_Jan 2, 2025 6_12_00 PM GMT+03_00.png
 
Labda ana tafuta pesa hata kwa kuuza fake news, si unajua alishindwa kesi na Vodacom majuzi kati, anafikiri mambo ni rahisi rahisi.
Huyo Kabendera anasoma Ph.D Katika chunky cha King’s College London moja ya vyuo vikuu bora kabisa duniani akiwa na Scholarship. Pia ni mwandushi wa magazeti mbalimbali duniani yakiwemo Guardian na the Economic
 
Usikatae moja kwa moja ukweli unaweza kuwepo na pia uongo unaweza kuwepo. Yote yanawezekana, japo mara nyingi wengi waligundulika si kweli.

Issue ya rizwan kukamatwa na unga China alafu baba yake akawapa wachina gesi ili uachie ilikua inazungumzwa na top politicians kabisa na waandishi nguli. Mwisho ikaja kujulikana si kweli

Mwaka 2015 Kuna yule kijana aliyeandika mkuu wa majeshi mwansansu amelishwa sumu. Ilikua hot topic humu na magazetini. Chadema wakaingia front kumsaidia yule dogo alipokamatwa, alifikishwa mahakamani kuthibitisha mkuu wa majeshi kalishwa sumu. Yule kijana watu walikua wakimvimbisha kichwa kuwa ni kweli, utetezi basi akasisitiza ana uhakika mkuu wa majeshi kalishwa sumu na yupo hoi kitandani Kama ni uongo wampeleke pale mahakamani. Kumbe mwansansu yupo anaendelea na kazi na kesho yake alienda kuzindua uwanja wa ndege wa jeshi morogoro. Yule kijana nadhani hadi Leo alijifunza somo kubwa sana
Hakujawahi kuwa na mkuu wa majeshi mwenye jina hilo
 
Back
Top Bottom