Usikatae moja kwa moja ukweli unaweza kuwepo na pia uongo unaweza kuwepo. Yote yanawezekana, japo mara nyingi wengi waligundulika si kweli.
Issue ya rizwan kukamatwa na unga China alafu baba yake akawapa wachina gesi ili uachie ilikua inazungumzwa na top politicians kabisa na waandishi nguli. Mwisho ikaja kujulikana si kweli
Mwaka 2015 Kuna yule kijana aliyeandika mkuu wa majeshi mwansansu amelishwa sumu. Ilikua hot topic humu na magazetini. Chadema wakaingia front kumsaidia yule dogo alipokamatwa, alifikishwa mahakamani kuthibitisha mkuu wa majeshi kalishwa sumu. Yule kijana watu walikua wakimvimbisha kichwa kuwa ni kweli, utetezi basi akasisitiza ana uhakika mkuu wa majeshi kalishwa sumu na yupo hoi kitandani Kama ni uongo wampeleke pale mahakamani. Kumbe mwansansu yupo anaendelea na kazi na kesho yake alienda kuzindua uwanja wa ndege wa jeshi morogoro. Yule kijana nadhani hadi Leo alijifunza somo kubwa sana