Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Samcezar,
Dhulumiwa siyo DHURUMIWA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mohamed Said, ni kweli kuwa Dr. Vedasto Kyaruzi hakuwa muasisi wa TAA japo ungekuwa muungwana kwa kukiri kuwa alionyesha mchango mkubwa ktk kui-shape TAA.
Kwanza alikuwa Katibu wa TAA Tawi la Makerere mwanzoni mwa mwaka 1942 wakati akiwa Uganda kwa ajili ya masomo.
Kipindi hicho Mwl. Nyerere hakuwa active kisiasa na wote wawili walikuja kutana pale Makerere University mwaka uliofuata - 1943.

Pia Dr. Kyaruzi aliporudi Tanganyika 1948 aliendekea kuwa mwanachama hai wa TAA na alikuta chama kimepooza sana kikiwa kimejaa wazee wa kiswahili na illiterate wasiokuwa na mikakati madhubuti ya kumuondoa mkoloni. Hakuna vikao vya kimkakati vilivyokuwa vikiendelea na wazee hao walijitenga na wasomi - akina Dr. Kyaruzi na wenzake wachache.

Baada ya rais wa TAA wakati huo Dr. Luciana Tsere mnamo mwaka 1950 kuhamishiwa Tanga, Dr. Kyaruzi alichukuwa urais wa TAA wakati huo wazee wakikataa vikao halali.

Hata hivyo, Dr. Kyaruzi alifanyiwa figisu na wakoloni baada ya kuona TAA imetekwa na wasomi na aliambiwa akasome kule Ulaya.
Hakwenda na bado alipewa transfer kwenda Morogoro ktk gereza la Kingolwira kama MO in-charge.

Mwl. Nyerere ndipo alipoingia TAA na kuwa rais akipewa kijiti na Dr. Kyaruzi (RIP).

Mkuu Mohamed Said, kama hutambui mchango wa Dr. Kyaruzi ktk kuijenga TAA sema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iselamagazi,
Umeandika vizuri sana lakini kuna makosa katika maelezo yako.

Nyerere hakupokea kijiti kutoka kwa Dr. Kyaruzi bali kutoka kwa Abdul Sykes.

Wakati Nyerere anaingia katika uongozi wa TAA baada ya uchaguzi uliofanyika Arnautoglo Hall, Dr. Kyaruzi alikuwa keshaondolewa Dar es Salaam yuko Nzega.

Uchaguzi ule Nyerere alichaguliwa Rais na Abdul Sykes Makamu wa Rais.
(Angalia Tanganyika Standard 19 September 1953).

Naamini hujasoma kitabu cha Abdul Sykes ndiyo maana una wasiwasi na msimamo wangu kuhusu mchango wa Dr. Kyaruzi.

Mimi ndiye niliyemrejesha Dr. Kyaruzi katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Katika historia rasmi Dr. Kyaruzi hajatajwa popote.

Dr. Kyaruzi nimekutananae katika Nyaraka za Sykes 1950 alipoingia katika ungozi wa TAA kama Rais na Abdul Sykes akiwa Katibu.

Ushindi huu wa hawa vijana wasomi ulifanikiwa kwa mchango wa Schneider Abdillah Plantan ambaye yeye alisimama kushinikiza Rais wa TAA wa wakati ule ambae ni kaka yake, Thomas Saudtz Plantan na Clement Mohamed Mtamila, Katibu waondolewe madarakani.

Nyinyi mnaandika historia hii kwa watu ambao wako mbali sana nanyi.

Mimi hawa ni wazee wangu na ndiyo maana unaona nina taarifa nyingi sana ambazo huwezi kuzipata kokote pale.

Ingia hapo chini usome taazia niliyomwandikia Dr. Kyaruzi kufuatia kifo chake mwaka wa 2013:

 
Samcezar,
Dhulumiwa siyo DHURUMIWA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Inawezekana tatizo ni kuwa hatufahamiani.

Inaelekea wengi wenu ndiyo kwanza mnasoma historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kama nilivyoaindika miaka 22 iliyopita na ndiyo maana mmepata mshtuko mkubwa ambao kwa bahati mbaya imesababisha taharuki kwenu kupelekea kuandika katika njia si ya kiungwana na pia kutoa vitisho dhidi yangu na kuitaka serikali ifanye kadha wa kadha dhidi yangu.

Mnadhani kuwa sifahamiki.

Ingekutosheni tu kwa kuona kuwa naandika kwa jina langu halisi na picha zangu zipo mnaziona.

Ombi langu kwenu ni kuweni watulivu someni historia hii kwani kuna wengi wamenufaikanayo.
Tufahamiane:
  1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  6. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
  8. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  9. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigania Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
  10. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  11. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
  12. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
  13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  24. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  26. Awards: Several Awards
  27. Visiting Scholar: (2011)
  28. University of Iowa, Iowa City, USA
  29. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  30. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  31. OTHER COUNTRIES VISITED
  32. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
You've posted this shit ad nauseam miaka na miaka hadi inatia huruma. Kwa kifupi, umeishiwa Mzee Mohamed Said. Huna uwongo mpya.
 
You've posted this shit ad nauseam miaka na miaka hadi inatia huruma. Kwa kifupi, umeishiwa Mzee Mohamed Said. Huna uwongo mpya.
Ndjabu...
Hapana haja ya kutukana.

Nitaweka mara nyingi kwa kuwa wako wengine ndiyo leo wananisoma na hujua huyu mgeni kutokana na maswali na namna wanavyoandika.

Hii ndiyo sababu najirudia.

Niko hapa kusomesha na mwalimu siku zote hurrudia masomo yake kwa wanafunzi wapya.

Kuishiwa si kweli nimeongeza vitabu sita nilivyoandika na vimetoka mwezi uliopita vitabu vitano na cha sita kimetoka siku ya mwaka mpya 2020:
  1. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
  2. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  3. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigania Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
  4. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  5. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
  6. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Anasoma Kwa Furaha
Kuna mahali nimesoma kuwa kila mtu hutoa kile alichokuwanacho.

Mwenzangu si haba umejaaliwa matusi nakumbuka picha ulizokuwa unaniwekea hapa kunitukana.

Mimi nina vitabu na picha mfano wa hiyo hapo juu ya binti anasoma kitabu changu kujifunza Historia na Lugha ya Kiingereza.
 
Wengi tushakuzoea Mzee Mohamed Said. Umeishiwa huna jipya sasa unakuja na promo ya hii "The School Trip To Zanzibar". Sarakasi hizi.
 
Wengi tushakuzoea Mzee Mohamed Said. Umeishiwa huna jipya sasa unakuja na promo ya hii "The School Trip To Zanzibar". Sarakasi hizi.
Ndjabu...
Angalau hukuja na matusi.
Mapya ninayo na In Shaa Allah utanisoma hapa Majlis.

Wengi wamevutiwa na kitabu cha Abdul Sykes.
Publisher ameniomba nifanye, ''review,'' ya kitabu anasema yapo mengi ya kuongezwa.

Jina langu ni promo tosha.
Kwa hakika nimefaulu sana katika kuvitangaza vitabu vyangu.
 
Sitaki kuifundisha serikali kazi yake sisi tunasambaza upendo wengine wanasambaza udini na chuki kuna watu wameota mapembe ni yakukata sasa.
 
Sitaki kuifundisha serikali kazi yake sisi tunasambaza upendo wengine wanasambaza udini na chuki kuna watu wameota mapembe ni yakukata sasa.
The boy tz,
Historia lazima ielezwe kama ilivyo hata kama kuna watu hawatapendezewanayo.

Leo Israel ipo Holocaust Museum pamehifadhiwa historia nzima ya mauaji ya Wayahudi wakati wa WW II, ''gas chambers,'' za Auschwitz Poland zipo hadi leo na watu wanazitembelea halikadhalika Afrika Kusini kuna Apartheid Museum ambamo kuna kumbukumbu ya uovu waliofanyiwa Waafrika na Makaburu.

Huku si kusambaza chuki ni kuweka kumbukumbu ili dunia ijirekebishe isirudie makosa.

Kuhifadhi historia hizi si kusambaza chuki bali ni kutaka watu wajifunze ubaya wa dhulma na wala hizi si pembe za kutafuta kukatwa.

Soma kitabu cha Mandela "Long Walk to Freedom," utazame nini kaeleza kuhusu historia ya ubaguzi katika nchi yake.

Ikiwa umesoma kitabu cha Abdul Sykes utaona katika maisha yake vipi aliweza kuwaunganisha watu na hasa wazee mashuhuri wa Dar es Salaam nyuma ya Mwalimu Nyerere na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ushapata kujiuliza vipi Mwalimu alipata umaarufu ghafla na kuwa karibu sana na watu kama Rajab Diwani, Iddi Faiz Mafungo, Mashadò Plantan, Mshume Kiyate, Bi. Chiku bint Said Kisusa kwa kuwataja wachache?

Hawa nimekutajia makusudi kwa kuwa wana waliyofanya makubwa katika TANU na kupigania uhuru ambayo nina hakika wewe na wengi wengine hamyajui.

Kwa nini historia imewasahau wazalendo hawa?
Hii ni kwa kudhamiria au ni bahati mbaya?

Kusahauliwa kwao na kufutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni moja ya changamoto zilizokuja na uhuru.

Mimi hawa ni wazee wangu na nimeandika historia zao ndani ya kitabu changu ili kuhifadhi mchango wao katika taifa hili.

Matokeo ya kitabu hiki baada ya kusomwa kote ndani na nje ya mipaka yetu haikuwa wasomaji kutaka serikali inikamate inisimamishe mahakamani kwa kosa la kuandika kitabu cha historia.

Hapa nchini kutokana na kitabu changu iliamuliwa lazima historia ya nchi yetu iandikwe upya na mashujaa wa uhuru wetu waadhimishwe.


Kushoto Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashad Ali na Sheikh Ahmed Islam

Nilizungumza na Prof. Haroub Othman na akanieleza vipi yeye ameathiriwa na yale aliyoyakuta katika kitabu changu kiasi ilimbidi kuonana na Mwalimu na kumuomba aandike historia ya maisha yake.

Hili Prof. Haroub alilifanya baada ya yeye mwenyewe kuwa na mazungumzo na Ahmed Rashad Ali kuhusu historia ya Abdul Sykes kwani wawili hawa walikuwa marafiki toka utoto wao katika miaka ya 1930 wakawa pamoja Dar es Salaam katika miaka ya 1950 wakati wa vuguvugu la uhuru linaanza na wakawa pamoja Cairo mwanzoni mwa miaka ya 1960 baada ya uhuru na wakawa pamoja tena Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 1960.

Ahmed Rashad Ali, Mzanzibari kaona yote kwa macho yake na alisadikisha kila nililoandika kuhusu historia ya TANU.

Rashad alikuwa mtangazaji wa Radio Free Afrika iliyokuwa Cairo radio aliyoanzisha Gamal Abdul Nasser kwa ajili ya ukombozi wa Afrika na akijuana vyema na Nyerere.

Mwalimu alikubali historia yake iandikwe na yeye mwenyewe atazungumza na jopo lakini hakuwahi kwa ajili ya maradhi,


Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Kamatha

Kazi hii ya kuandika maisha ya Mwalimu imefanywa na Kavazi la Mwalimu Nyerere utafiti ukiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Issa Shivji.

Nina taarifa kuwa kitabu cha historia hii kipo njiani na jopo hili lilifika nyumbani kwangu kunihoji kuhusu niyajuayo katika historia ya TANU.

Niliwazawadia baadhi ya Nyaraka za Sykes na picha nilizokusanya katika utafiti wangu.
Oxford University Press Nairobi wakanitia katika mradi wa kuandika vitabu vya historia kwa ajili ya kufundisha Kiingereza shule za msingi za Afrika ya Mashariki na kitabu changu, ''The Torch on Kilimanjaro,'' kikachapwa mwaka wa 2007.


Hiki kitabu ni toleo la pili

Harvard na Oxford University Press New York wakanitia katika mradi wa kuandika Dictionary of African History (DAB) mwaka wa 2008 nikiwa mwandishi na mshauri na kazi ikakamilika 2011 kwa kuchapwa volume sita.

Prof. Emmanuel Acheampong msimamizi wa mradi huu aliniomba niandike maisha ya Kleist Sykes.


Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography

Ajabu wewe ndugu yangu badala ya kunipongeza unataka serikali inipoteze kwa kuandika kitabu kilichoeleza historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Laiti ningesambaza udini na chuki ndani ya kitabu changu kitabu hiki kisingeachiwa kuwepo katika mzunguko kwa miaka 22 sasa na wala hawa wote walioshirikiana na mimi katika kuchapa kazi zangu wasingefanya hivyo.

Hujasoma kitabu changu.

Kisome ujue kwa nini kitabu hiki kimekuwa maarufu na kwa nini niliingizwa katika miradi hiyo hapo juu.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali mengi sana kwa Mohamed Said, mimi kama kijana naona ktk majibu yako mengi huku ukutumia utulivu mkubwa nikupongeze, ila naona kila namna ya watu wametoa mchango wao ktk uhuru wa Tanganyika.

Wapo Wazulu toka Mozambique / South Africa , wapo 'Wanyasa' wa Malawi, Wadengereko, waSomali, Wahindi, Watu wa Kigoma , watu wa Kaskazini mwa Tanganyika, watu wa Nyanda za juu Kusini, WaComoro , WaZanzibari n.k ila hili la kuwafuta asili yao na kuwaweka ktk makundi ya udini wao ndiyo umeharibu hali ya hewa ktk kazi yako nzuri. Wengine walibadili dini ili wazee wake au makazi mjini au nafasi za masomo n.k

Maana kwa kuweka majina yao na asili yao unaweza kuwatambua mchango wao ila kwa kuweka dini yao na kuficha asili/maeneo watokayo hujaitendea haki historia.
 
Bagamoyo,
Haikuwa "kila mtu,"kama unavyosema.

"Kila mtu," ilikuja baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka wa 1958.
Hii Kura Tatu ni historia ya kusisimua na nimeiandikia kitabu, "Uamuzi wa Busara wa Tabora."



Kwa nini nimeaiandikia kitabu?

Nilitaka kueleza historia ya wazee wangu walivyompiga pete Muingereza na kumshinda katika mchezo wake mwenyewe.

Juu ya haya yote hata kama wewe na wengineo haiwapendezi historia hii mchango wa Waislam haukuwa na mfanowe.

Soma, ''Uamuzi wa Busara wa Tabora,'' uone vipi Uislam ulivyotumika kuwaunganisha Watanganyika kudai uhuru kama taifa moja.

Huu ndiyo ukweli na ndiyo historia ilivyokuwa.
Lakini wapi historia ya Sheikh Rashid Sembe shujaa wa Kura Tatu ilipoandikwa?


Sheikh Abdallah Rashid Sembe

Nani anaejua dua iliyofanyika Mnyanjani Mwalimu Nyerere na Amon Kissenge wakishiriki kumuomba Allah ainisuru Tanganyika na fitna za Waingereza?

Kipindi hiki suala la dini lilikuja juu kiasi cha kutishia kuikata TANU mapande mawili.
Nani anaeijua historia hii?

Jambo la kusikitisha kuna waandishi wanathubutu kusema kuwa All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) ambayo ni matokeo ya Kura Tatu kilikuwa chama cha Waislam,

AMNUT iliundwa na Mashado Plantan na Waislam wachache sana waliojitoa TANU na hii ni historia ya kusisimua sana na nimeieleza katika kitabu changu.

Mimi bila kupepesa huwajibu kuwa kama Waislam walikuwa na chama basi chama chao ni TANU.

Sasa ikiwa historia ya kweli imefutwa ndiyo ilitakiwa mimi niiache ipotee?

Bahati nzuri historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni historia ya wazee wangu sikuweza kustahamili kuona imefanyiwa khiyana.

Ilikuwa lazima niiandike.

Sasa kuandika historia hii lakini niache vitu muhimu kwa kuhofu ati nisieleze historia kama ilivyokuwa hili kwangu halikuwezekana na ni muhali mkubwa sana na kwa hakika hii hofu ya kueleza mchango wa Waislam uko hapa kwetu tu.

Kote nilikoalikwa kuhadhiri kuhusu historia hii na "book reviews," zilizofanywa na wasomi mashuhuri katika African History kama John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan hili wala halikujitokeza bali liliongezwa katika somo kama "field of enquiry," yaani elimu ya kufanyiwa utafiti kujua kwa nini ilikuwa hivyo.

Hata mazungumzo yangu na Prof. Haroub Othman na Prof. Shivji hawakuniuliza kwa nini nimechagua kuandika historia ya Waislam.

Hawakuniuliza kwa kuwa walikuwa wanatambua ni historia iliyokuwa inatakiwa ifahamike.

Mfano iliwezekanaje Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akawa mstari wa mbele bega kwa bega na Mwalimu Nyerere katika TANU kupigania uhuru wa Tanganyika?


Sheikh Suleiman Takadir ni huyo pembeni kwa Nyerere, Clement Mtanila na Bi. Titi Mohamed
nyuma kulia ni John Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere

Kiliwashinda kitu gani mapadri kujitokeza wakasimama juu ya jukwaa moja na Nyerere bega kwa bega kudai uhuru kama aliyofanya Sheikh Suleiman Takadir?

Imekuwaje historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ilipoandikwa masheikh hawa majina yao hayako popote?

Hii ndiyo aina ya maswali ninayoulizwa kote nilikopita.
Sijapata kuulizwa kwa nini nawataja Waislam?

Kisome kitabu cha Abdul Sykes kuna mengi yatakushangaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mohamed Said,
Swali moja Maalim, swali ni nini kilikusukuma kufuta asili ya hawa wapigania uhuru na kuwatambulisha kwa 'dini za kuja' wakati sisi ni watu huru wenye historia ya majina yetu, asili zetu, tamaduni zetu, mila na desturi .

Kuweka nyuma asili zetu Huoni unautia doa uhuru waliogombania mababu hawa ambao walijitambua kama waTanganyika lakini unafuta asili zao na kuwatambua kwa kuwatia uasili wa Mashariki ya Kati chimbuko la dini hizi?
 
January 6, 2020
Ujiji, Kigoma

Mzee Juma Ambrose na Simulizi za vuguvugu la kutambuliwa uasili wao kuelekea Uhuru
Wabembe na Wagoma wa Ujiji wakataa kutupa utambulisho na utamaduni wao mbele ya Waarabu. Harakati za Mzee Omari Buhoro aliyetumia ndumba za kienyeji ili vijana wa Ujiji wasiweze kulazimishwa kujiunga na jeshi la mkoloni kwa ajili ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia WWII
Mzee Juma Ambrose asilimulia jinsi wazee wa Ujiji walivyowadindia Waingereza na Waarabu, kisa majina yao kutotamkwa vyema na haiwezekani washurutishwe watupe Miungu yao ya kiasili kirahisi na kukumbatia Miungu ya Dini za kuja.

Wazee wa Kigoma Ujiji wanasema Miungu yao ya Asili ndiyo kitambilisho chao, mfumo wao na ndiyo salama yao. Nyumba maarufu ya Tanganyika House na milango ya vyumba vyake asili yake ni nini. Magonjwa ya Mizimu ya Kale dini hizi za kuja haziwezi kuyapoza lazima utaratibu wa mila ufuatwe Mzee Juma Ambrose anaendelea ktk simulizi sahihi za sisi ni kina nani kama waTanganyika...na matokeo yanakuwa mazuri watu wanaishi salama bila bughudha za dini za kuja...

Mambo haya ya asili yanatuunganisha kwani yanafanana ktk jamii ya kiTanganyika hata unaweza kukabidhiwa mikoba uwashikie watani zako kujilinda hawa watu wa kuja na mashua wakikubadilikia anaendelea kuelezea umuhimu kuweka asili mbele Mzee Juma Ambrose...wa Ujiji Kigoma Tanganyika.

Chemchem ya Lutale na maajabu yake bila kumsahau Kamchape mtu aliyeeneza amani katika jamii na mchango wake kwa Tanganyika. Treni za ajabu usiku wa manane mali za Mzee mmoja. Simulizi kali zetu wenyewe toka ktk mazingira tunayoyajua na kuyaishi.

Sasa natambua kwanini waTanzania wanakuja juu kutambulishwa kwa makundi ya dini za kuja badala ya mchango wao kama wao ktk kuunda nchi huru Tanzania.
Source: Dar24 Media
 
Bagamoyo,
Swali lako naona umelikosea kuliuliza.

Naona umetia hisia zako ndani ya swali kwa hiyo mimi hapo unanipoteza kwa kuwa inatakiwa nifanye staha na niwe na adabu kwa hisia zako.

Siwezi kukupinga kwa fikra zako za ''dini za kuja,'' kwa sababu mimi namuamini Allah SW muumba wa ulimwengu na mila yangu ni mila ya Nabii Ibrahim.

Hapa tumetofautiana pakubwa kwani wewe ni unaamini ''asili.''

Ikiwa utaweza kuniuliza swali kutokana na maudhui ya kitabu bila kuingiza hisia zako nitajaribu kukujibu kama nitaweza.
 
Bagamoyo,
Katika Uislam hakuna kushurutishana katika mambo ya dini.

Bwana Ambrose ana haki ya kuamini akitakacho na hairuhisiwi kumbughudhi madam yeye hajawafanyia uadui wengine.

Haya ndiyo mafunzo ya Uislam.
 
Bagamoyo,
Katika Uislam hakuna kushurutishana katika mambo ya dini.

Bwana Ambrose ana haki ya kuamini akitakacho na hairuhisiwi kumbughudhi madam yeye hajawafanyia uadui wengine.

Haya ndiyo mafunzo ya Uislam.
Kwa hiyo naweza kwenda Saudia tena Maka nikafungua Kanisa na kuanza kueneza Injili kwa vibali pasipo kujali katiba yao inasema nini na wakanikubalia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…