Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Maalim Mohamed Said,

Sijaona nafasi ya wasio na imani za kuja na majahazi au merikebu, maana tafiti na maadiko ya kiserikali ynasema sensa kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika kulikuwa na idadi kubwa kwa asilimia walioamini ktk mambo ya jadi. Hivyo 30% Islam 30%:Christian na 40 % imani ya jadi .

Je kwanini kuwapuuza hawa wengi asilimia 40% wa dini ya jadi. Na inakuwaje kuwaondosha hawa wenye imani ya jadi kama hawakuwepo eneo la Tanganyika kabla ya imani za kuja na hata baada ya uhuru,

Nini mantiki ya kupambanisha au kufanya ulinganifu wa makundi ya dini za kuja na kuwaona wale wa jadi ni washenzi, hawajastarabika na hawana mchango ktk historia ya Tanganyika ingawa pia wengi wao hawa walugaluga pia walipitia shule rasmi na kuelimika kama hawa wengine wa dini za kuja na kuendesha maisha yao kama wakulima, wafanyabishara wadogo / wakubwa , watumishi wa mkoloni/ umma n.k.
 
Acha kufundisha chuki,haitasaidia Yale yaliyopita zaidi ya kuwatia jazba watoto na wajukuu.uislam ulikua Tanganyika kabla ya ukristo,walijenga shule?walijenga misikiti?walijenga hospital?walijenga seminary?kwanini?

Inakubidi ueleze kwanini hawakufanya maendeleo ya watu mpaka wamissionari walipokuja?Babu zenu waliwazuia baba zeyu kwenda shule za kanisa kwa hoja watalishwa mbuzi katoliki.ndipo elimu kwa umma wa Islam ikayumba Leo unaeneza chuki kupata mkate wako.

Ikiwa una Nia njema ungeshirikisha serikali na vitabu visiuzwe tu misikitini Nia kuwafanya wawe na chuki na ukristo.miwalaumu Babu zenu kwanini waliwaaminisha mkienda Soma shule za kanisa mtakula ze kitiiiiz.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mtoto anashinda madrasa unategemea atafaulu? Never. Elimu ni kwa wenye akili tu
Wapelekeni watoto wenu shule
 
= kudhulumiwa

Mbona umeshajenga taswira hasi? Mwenzetu umeshakisoma kitabu?
 
Kuonewa mentality ni kupoteza nguvu za kuitoa ulipo na kutafuta kuonewa huruma, ni ujinga. Jikukung'ute makalio angalia unajikomboa vipi songa mbele. a kuzungumzia udini Tanzania ni ujinga, kwetu Lindi, unahama dini unavyotaka sio mambo ya mbwembwe unayoyaleta hapa. Unauliza ukioa wake wawili unakua dii gani unaambiwa mwislam, basi unao mke wa pili a kuanza kuiita muislam wakati hata msikiti huujui, hivyo kwenye koo zetu wapo wote uaowataka wewe wakristo, waislam, wasabato wasionadini huo ujinga wakujipandua udini sana kwetu hakuna wote tunakula kitimoto waislam, wasabato, waktistu a wasio na dini hizo mbwembwe zako za waislam wakristu cheza nazo huko huko.

Watu wenye kuchochoa haya mambo ya dini ni wanufaika wa hayo mambo ipo uwezekaNO UNALIPWA NA WENYEKUFAIDIKA NA HUO UDINI UNAOJARIBU KUUWEKA KWENYE MIOYO YA WATANZANIA AMBO NI KWA FAIDA YAKO WEWE KWA SASA LAKINI LENGO LAKO NI KUWAARIBIA WATOTO NCHI YAO INAYOKUA WAKATI WEWE USHA ZEEKA NA UNAELEKEA KUFARIKI, KWA HERI BWANA KAMSALIMIE MANANI. Waachie watoto nchi yao wewe kama ukusoma mpeleke mwanao akasome.
 
Kingekuwa ni kitabu cha kuwaeleza waislam wajikwamue vipi kimaisha hasa kuhusu elimu, ingekuwa jambo jema na lakheri kwa Waislam wote.
Kuwakumbusha yaliyopita ni kuwatengenezea chuki mioyoni mwao na kuwafanya wanyonge na wagonjwa.
Kitakachowakomboa Waislam ni Elimu tu na sio majambia, ngamia au punda, mkumbuke kuna bunduki na vifaru.
Elimu, elimu, elimu, hamtaki basi andaeni kizazi chenu kuishi maisha ya dhiki na chuki, magereza yapo, risasi zipo, bahari ipo na maeneo ya kuzika yapo. Kitabu buku 2!!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha maneno mengi ndgu MS umeambiwa unaposema "kanisa" unamanisha nn?
 
Mzee duniani hakuna nchi yenye usawa timilifu. Vitu vingine ni kuviacha tu, wewe himiza vijana wapige kazi.
 
Kaka maneno yako ni makali sana.

Wengine tumeona tu picha ya kitabu, wala hatujakisoma na kujua kama mwandishi anataka kutuambia nini.

Kujibu bila kujua kusudio la mwandishi ni kumhukumu bila hata kumsikiliza.

Anayo haki ya kisikilizwa, na baadae kama ipo haja basi ajibiwe kwa hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Security Code,
Msikilize marehemu Kitwana Selemani Kondo:

''Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu. Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga. Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.''

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)
 
Mzee duniani hakuna nchi yenye usawa timilifu. Vitu vingine ni kuviacha tu, wewe himiza vijana wapige kazi.
Mtama...
Vijana gani umewakusudia wahimizwe kazi?
Vijana gani hawahitaji kuhimizwa kazi?

Wakishahimizwa kazi dhulma dhidi yao itakuwa ishaondoka?
 
Kama mtoto anashinda madrasa unategemea atafaulu? Never. Elimu ni kwa wenye akili tu
Wapelekeni watoto wenu shule
McMahoon,

''Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu. Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga. Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.''

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)
 
Huenda hujawahi kusoma vitabu vyake na kujua maudhui yake; hiki siyo kitabu chake cha kwanza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…