Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Mtama...
Vijana gani umewakusudia wahimizwe kazi?
Vijana gani hawahitaji kuhimizwa kazi?

Wakishahimizwa kazi dhulma dhidi yao itakuwa ishaondoka?
Ndio maana my first point ilikuwa kuhusu usawa timilifu. Haupo duniani. Kila jamii itakuwa tu na watu ambao ama kwa halali au kwa hisia, wataona wanaonewa na kudhulumiwa.

Kuhusu kuhimiza vijana, point yangu ni kuwa; kulalamika kuhusu dhulma kila siku, hakutawasaidia hao unaosema wanadhulumiwa. Maana hapa tulipo sasa hivi sijui kama kuna mtu ana appetite na kufukua makaburi ya 1960's, yalikoanza haya mambo.

Binafsi sina shida na kujifunza historia, na naamini kuna mambo mengi sana ambayo yanatakiwa either kuwa updated au kubadilishwa kama kuna ushahidi wa upotoshoshaji, kwa lengo la kuweka historia sawa. Ila kama lengo ni kuonyesha tu dhulma dhulma kila siku; unatengeneza mazingira ambayo kusikilizana itakuwa ngumu.

Ni hayo tu, kila la kheri. Nitatafuta copy yangu
 
Mtama...
Kitabu cha Abdul Sykes nilikiandika kwa nia ya kusahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kitabu ulichosoma ni matokeo ya utafiti huu.

Kutokana na utafiti ule yakaingia mambo mengi mathalan kwa nini walioandika historia ile walifanya juhudi kubwa ya kupotosha ukweli.

Moja ya mambo niliyogundua ni hofu iliyokuwapo ya kuwaadhimisha wale waliopigania uhuru ambao wengi walikuwa Waislam.

Kuanzia hapa ndipo yakaanza kufunguka mengi na yote ni ya kutisha.

Wewe umeliona hili na unajaribu kuhalalisha dhulma iliyojengwa na kupangwa kwa kutaka iaminike kuwa yanayowasibu Waislam ni ya kutegemewa kwa kuwa hakuna chembelecho, "usawa timilifu."

Lakini ukiingia katika historia ya Tanganyika utakuta kuwa sababu ya hali hii ni kutamalaki kwa njama wala mimi sikukusudia kuwepo na usawa uliokamilika.

Ushauri wangu kwako ni huu.

Jizuie.

Waachie wanaotuhumiwa wajibu tuhuma zao.

Lau una hamu ya kushiriki mjadala huu himiza mtuhumiwa ajibu tuhuma zake.

Wala sijaandika haya kama malalamishi.

Ningefanya hivyo ningewadogosha sana wazee wangu waliounda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hii ni kazi nzito ya kutafuta utangamano katika nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waachie wanaotuhumiwa wajibu tuhuma zao.

Tatizo unapotuhumu kwamba viongozi wa nchi wanaotoka dini fulani, by extension unawagusa na watu wa dini hiyo.
 
Waachie wanaotuhumiwa wajibu tuhuma zao.

Tatizo unapotuhumu kwamba viongozi wa nchi wanaotoka dini fulani, by extension unawagusa na watu wa dini hiyo.
Mtama...

Hapana mtu wa kawaida haingii humo.

Ikiwa unataka kujua haya vipo vitabu unaweza kusoma kupanua uelewa wako.

Msome Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).

Bahati mbaya kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku lakini kipo katika mtandao unaweza kukipata.

Kitabu vyote hivyo vina historia yake nikiwa na maana ya kuwa vilipotoka na kujulikana yaliyomo ndani hofu ilitanda.

Bergen na Sivalon havimo tena katika mzunguko yapata sasa miaka 20 na zaidi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuuliza maswali yafuatayo:
1. Kwenye kitabu chako kuna maoni yoyote ya upande wa viongozi wa kanisa?
2. Kanisa unaloliongelea ni lipi kwa sababu Tanzania kuna makanisa mengi sana.
3.Kwa nini unadhani hilo kanisa ulilolichagua peke yake ndiyo linachagiza mambo serikalini?

Ukinijibu haya nitaleta mengine.
 
Mkuu Kichuguu maalim MS kunaswali LA kumuuliza anaposema "KANISA" anamaanisha nini?
Huyu mzee ana tabia ya kukimbia maswali au ufafanuzi kuhusu maandishi yake mwenyewe. Inaonekana hajiamini au hajui anachoandika. Kanisa kwa maana/definition ipi na ya nani? Dhehebu/madhehebu gani? Taasisi zipi? Jee ni Uongozi pekee au inajumuisha Uongozi pamoja na Waumini wao?
 
Kinyungu,
Soma kitabu utapata majibu ya maswali yako.

Ingia mohamedsaidsalum.blogspot.com fanya search kwa majina haya: Bergen, Sivalon na Njozi.

Utapata makala nyingi nilizoandika na mengi ya kuelimisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndjabu...
Huwa mnanifurahisha mnapoanza na "huyu mzee."

Akili yako tayari ushaiwekea jiwe zito juu.

Hapo mimi tena wala sishughuliki hadi ghadhabu za mchangiaji zipoe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinyungu,
Soma kitabu utapata majibu ya maswali yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini ushindwe kumjibu maswali yake hadi anunue kitabu chako kwanza na kukisoma? Huoni hapo inaleta walakini kwamba unafanya kila jitihada kuepuka kujibu moja kwa moja maudhui ya maandishi yako mwenyewe? Mfano, mimi nimesoma mchango wako fulani wa warsha/semina moja uliyofanya Berlin, lakini umeshindwa kunijibu swali langu hadi leo. Jee, hiyo imekaaje?
 
Hiyo picha ya mwisho ni wakati wq vita vya MAJIMAJI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndjabu...
Nani kazungumza kuhusu kununua kitabu?

Nimesema asome kitabu.

Haya si masuala ya kujibiwa kwa mstari mmoja.

Nisingeweza kusahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa kuandika sentensi hata 100.

Nimeandika kitabu cha kurasa zaidi ya 300+.

Huu wangu si uwanja wa watu wasio na uwezo wa kusoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Kichuguu maalim MS kunaswali LA kumuuliza anaposema "KANISA" anamaanisha nini?
Nilimwuliza swali hilo mwanzo hakunijibu. Mara nyingi maandiko yake ni ya kushtumu sana dini ya Nyerere; na anaposema udini, huelekea kuamini kuwa Nyerere aliwaacha waislamu na kuweka watu wa dini yake (wakatoliki). Mara zote neno Udini kwake ana maana ya Ukatoliki dhidi ya Usilamu, na neno kanisa lina maana ya Ukatoliki.

Katika serikali ya Nyerere kulikuwa na wakatoliki wawili tu; Nyerere mwenyewe na George Kahama. Lakini kuna wakati huyu bwana aliwahi kuashilia kuwa Nyerere aliweka Padri wa katoliki kuwa waziri wa Elimu (Padri Simon Chiwanga) kusudi apendelee wakatoliki tu na kuwazima waislamu kielimu. Yaani hakufanya hata utafiti kidogo tu kujua kuwa Chiwanga huyo hakuwa mkatoliki. Yeye anaposikia ukristo anaamani kuwa ni taasisi moja inayopingana na uislamu, yaani hajui kuwa ukiristo una denomination nyingi sana ambazo hazikubaliani kiitikadi, ni kama uislamu ulivyo na denomination nyingi zisizo kubaliana kiitikadi, mfano Sunni vs Shiite. Kwa mheshimiwa huyu mambo yangekuwa sawa kama nchi yoote ingekuwa inaongozwa na waislamu tu, ingawa sijui huwa anataka waislamu wa namna gani!
 
Tuseme keshasoma hicho kitabu lakini bado ana maswali? Kwanini inakuwia vigumu sana kujibu tu ya maswali ya wachangiaji bila ujanja ujanja wenye kuashiria unakwepa wajibu wako kama Mwandishi?
 
Asante nitavitafuta
 
Well said!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichuguu,
Umeandika vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhadzabe,
Rusumo,
Kuna mtu kaniuliza tafsiri ya hiyo cover.
Mimi sijui kwani usanifu wa cover kafanya publisher.

Nitamuuliza In Shaa Allah.
Kitabu hiki muombe mtu akununulie hapa Dar es Salaam.

Mzee Mohamed Said, unajidhalilisha kwa maneno yako mwenyewe kwamba hujui tafsiri ya cover ya kitabu chako!
Watu wanao design cover ya kitabu kwa kawaida hupewa short synopsis toka kwa author kuhusu overall mood, tone na theme ya kitabu husika. Hizi components husaidia kutengeneza cover nzuri ya kitabu yenye ujumbe wenye afya. Ikiwa huna unalojua kuhusu cover ya kitabu chako basi wewe ni bogus!
Imagine upo ana kwa ana na mtangazaji wa TV anakurushia swali kuhusu tafsiri ya cover ya kitabu chako kisha unajibu kuwa huna ulijualo labda aulizwe publisher!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…