FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Kwanza inabidi nikuombe samahani lengo langu la kuandika ujio wa uislaam ulikuwa karne 4 hadi ya 5 nimefanya makosa ya kiuandishi.. Ndivyo nilivyo. Hilo nadhani tumelimaliza isipokuwa nachotaka kujua huyu mwandishi anapochanganya Ujio wa waarabu ma wahindi walokuja fanya biashara nchini walikuja fanya biashara na watu gani ikiwa Wabantu hawakuwepo? na kwa nini waarabu walilita bara letu bara la weusi. halafu anasahau kuna Utawala wa Kiarabu (Oman) tofauti kabisa na ujio wa WaYemen au Wa Afghan/Pakistan. Kuna swala la Dini kutoka Saudia kupitia Magadishu na kushika kwetu vinahusiana vipi vyote hivi na biahsara ya Utumwa au Mapinduzi ya Zanzibar.
Halafu nikwambie kitu, Ibrahim Noor anafanya makosa makubwa ya kujaribu kupamba historia mabya kwa mafuta, kwa sababu hata huku Marekani wapo wazungu wabaguzi na tunawajua, wanajaribu sana kusema hapakuwepo na Utumwa, hawakuwepo na mauaji ya watu weusi isipokuwa watu weusi ndio Thugs. Kwa hiyo mimi ananipa picha tofauti kabisa kwa sababu huwaona hawa wazungu wanavyojaribu kujikosha kwamba wao ni watu wazuri sana na kwamba yaloandikwa kuhusu wao ni uzushi mtupu, sisi waafrika ndio tuliuzana wenyewe ktk Utumwa..
Hii mbaya sana kuanza kutenganisha watu kwa rangi zao maana historia yetu haiandikwi kwa makundi ya rangi za watu ama imani zao ila kuna historia za makabila. na anapozungumzia Uislaam unazungumzia watu wote kwa sababu Uislaam ulisambazwa Afrika sio na waarabu bali wasomi walokwenda jifunza dini wengine walikuwa waafirka weusi waloijua dini kuliko waarabu wenyewe. Sio kila mwarabu aliujua Uislaam ama alikuwa mwalimu wa dini wengi walikuja kwa sababu ya biashara na wengine kutawala.
halafu biashara ya Utumwa inajulikana wazi kwamba wote wazungu, waarabu na wayahudi walishirikiana kufanya biashara hiyo hakuna mwenye nafuu zaidi ya mwenzake. Mwarabu akiwa mtawala alipewa deal la WATU kuwa wanatakiwa kwenda kufanya utumwa Ulaya na bara Amerika na kichwa ni Dollar 10,000. Mwarabu akaingia bara alikokubalika maana walikuwa wakifanya biashara za vito na spices wakakusanya watumwa na kuwaleta Coast kuwauzia Wazungu.
Ndio maana masoko yote ya Utumwa yalikuwa makanisa yenye undergraound kupitishia watumwa hadi ufukweni. Na Wayahudi ndio walokuwa na utajiri wa Melikebu zao wakinunua watumwa na kwenda wauza Ulaya, hii ni history ilofichwa na pande zote kwa sababu Muafrika haweki kumbukumbu zake na rahisi kudanganywa. Mimi sina sababu ya kumsma Ibrahim Alnoor kwa sababu anachokifanya ni makosa ni sawa kabisa na washawishi wa KKK wanaojaribu kuonyesha upendo kwa weusi huku ndani ya roho zao wakijua machafu yao hayasafishiki..
Uislaam has nothing nothing to do with Waarabu au Wahindi. Imani ya dini haihusiani na mambo waloyafanya waarabu au wahindi ama kuwapa uhalali juu ya bara hili isipokuwa tuishi pamoja na kwa mapenzi ya UTAIFA na kutojali tofauti zetu za rangi na imani maana leo hii wewe FaizaFoxy ukienda Arabuni hutapewa haki sawa na mwarabu hata kama babu wa mababu wako walikuwa na asili huko. Nenda Pakistan, Afghanstan japo weuzi walikuwepo kwa karne bado hawana haki sawa na mwarabu mweupe. Hata Hadith za Mtume zimetueleza juu ya Bilal iwe hawa! what happen - happened tuyaache tusianze kukumbushana yalopita.
Mkandara umechanganya mada nyingi sana mpaka inaniwia vigumu ku "concentrate" na majibu sahihi.
Kwa kuanzia, umekosea tena, najuwa kwa uandishi tu, kule uliandika 14 na 15 hapa umeandika 4 na 5. Unanchanganya.
Hilo la kuhusu Waraabu nimejaribu sana tena sana kuelezea humu JF mara nyingi kuwa Waarabu hawakuja Afrika, ni kwao. Walikuja kutoka wapi?
Hili la Waarabu linataka wasaa sana na ntakuelezea kiutaratibu kila tunavyoendelea kujadili lakini kabla sijaanza, naomba kukuuliza, Jee, umekisoma kitabu cha Professor Noor? mimi nnacho.
Maana tusijadili kitu ambacho mimi najibu kutokana na niliyoyasoma na kuyatafiti japo kiduchu kupitia mtandao lakini mwenzangu unajadili kwa uzoefu na bila kukisoma hicho kitabu.
Naomba tutatuwe hilo kwanza kisha ntaelewa kama nnajadili na aliyekisoma kitabu kinachoongelewa au la.

