Kitakachofuata kwa Mdee na wenzake baada ya Rais Samia kuhudhuria mwaliko wa kongamano la BAWACHA, kitawaumiza sana CHADEMA

Mzee hiyo ishaisha si umesikia mawakili wamesema hawana cha kuendelea kuwaoji hao wamama,Kama zilivyofutwa kesi za LEMA basi na za hao wamama zitafutwa.

Kesi ya Mdee kafungua mwenyewe, akiifuta inamaana maamuzi ya baraza kuu yanasimama na wanakosa uanachama. Pona pona yao waendelee na kesi tu.
 
..kesi ya Lema ilifutwa na serikali.

..kesi ya Halima anatakiwa aifute mwenyewe.

..na akiifuta uamuzi wa baraza kuwafukuza unasimama.

..ndio maana nasema ili kuweka mambo sawa ni lazima kesi iishe kwa kuwapa ushindi Halima na wenzake.

Na huo ndio ukweli mkuu. Watu wengi wa CCM hawaijui hii kesi wanashabikia as if CHADEMA waliifungua.
 
Mzee hiyo ishaisha si umesikia mawakili wamesema hawana cha kuendelea kuwaoji hao wamama,Kama zilivyofutwa kesi za LEMA basi na za hao wamama zitafutwa.

Kesi bado inaendelea. Upande wa kina Mdee utaanza kuhoji upande wa CHADEMA. Msiwe na haraka ya kuongea.
 
Mzee mbona hauelewi hayo mambo yashaisha,wewe kama ulitegemea viti maalum wewe hachana na huo mpango tafta kazi ya kufanya.

Ulikuwepo mahakamani leo?. Proceedings zinazofuata ni baraza la wadhamini kuhojiwa Basi. Chama kikikataa kwamba hakikuwadhamini Basi kesi inaishia hapo.
 

Unaongea hivyo huku ukiona aibu. Samiah kakaribishwa na BAWACHA Kama Rais sio Kama Mwenyekiti wa CCM. Ukisema hivyo inamaana Rais Samiah ni Rais wa CCM pekee yake ambacho sio kweli. Halafu siasa za kupigana ziliondoka na Magufuli Samiah kaja na diplomacy.
 
Mbowe ndo CHADEMA na CHADEMA ndo Mbowe. Kamati kuu ni rubber stamp.

Ingekuwa hivyo angejiamulia mwenyewe kuwafukuza uanachama. CHADEMA inaongozwa na katiba sio bla bla. Ndio maana akina Halima Mdee walikimbilia mahakamani basi. Ila kiukweli akina Halima walijiangusha wenyewe kwa kushindwa kuvumilia kwa muda mchache.
 
Kwani hiyo kesi imefunguliwa na nani?

Amandla...
 
Muasi gani anatamani kurejea chadema. Chadema ni debe tupu linalovuma. Wakati ccm ya samia inawapa vigogo wake kamba wale malisho kwa urefu wa kamba zao chadema wamepewa kamba ya kujinyongea na samia.
Time will tell

Slaa mbona karudi kwa mlango wa nyuma?. Halafu mbona akina Halima Mdee wamekomaa mahakamani wanalilia uanachama wa CHADEMA?.

Kifo Cha CHADEMA sio leo wala kesho, alishindwa kikwete, akaja Magufuli na Sasa mama Samiah kaamua kukaa nao kwa pamoja. Kamba ya kujinyonge labda kwa CCM sio kwa CHADEMA. Chadema hawana Cha kupoteza, hawapo bungeni, serikalini na hata kwenye halmashauri na mitaa, una wanyonga kwa ajili ya Nini?
 
Kina Mdee na Mzee Slaa watasamehewa na kurudi chamani...

Labda Slaa, ila Halima na hao Wenzake hapana, kwanza kikatiba wamejifukuzisha chama kwa kufungua kesi, kuachana na usaliti.
 
Mbona hujaandika hapo chini ni mganga kutoka wap,i namba hujaweka nguruwe wewe!!
 
mbona inajulijana kuwa wanasamehewa maana hiyo ruzuku wanayopewa ni pamoja na hao wabunge wakiwafukuza ruzuku hiyo hawataipata

Naona mnapotosha, Ruzuku haitokani na kura za viti maalum. Halafu Ruzuku ni haki ya chama sio hisani.
 
Uamuzi wa Mbowe hauwezi pingwa na baraza kuu zaidi ya kuubariki.

Hayo unasema wewe. Baraza kuu laweza kukataa kuwasamehe mpaka waombe msamaha. Walipewa hiyo nafasi wakafanya kiburi . Hai waende ACT au CCM walipo Sasa hivi.
 
Ingekuwa hivyo angejiamulia mwenyewe kuwafukuza uanachama. CHADEMA inaongozwa na katiba sio bla bla. Ndio maana akina Halima Mdee walikimbilia mahakamani basi. Ila kiukweli akina Halima walijiangusha wenyewe kwa kushindwa kuvumilia kwa muda mchache.
Najua kwa sasa wanachama wa CHADEMA mnapitia wakati mgumu sana ila naona muendelee kula hiyo adhabu maana tukiwaambia CHADEMA ni mali binafsi ya Mbowe mnakuwa hamuelewi.
 
Ulikuwepo mahakamani leo?. Proceedings zinazofuata ni baraza la wadhamini kuhojiwa Basi. Chama kikikataa kwamba hakikuwadhamini Basi kesi inaishia hapo.
Watajua wenyewe ila mm nnachokiamini ni kwamba hayo Mambo yashaisha.
 
Mkuu mbona unaongea ujinga....ww husikiliza hotuba za LEMA na mama aliongea nini alipokuwa pale userliver?
Kwanza ni USA river not userliver, pili alisema atafuta kesi zote! Ndio maan nimekuuliz unaweza kutueleza hapa hayo madhambi ya Lema yaliyopelekea kua na kesi? Samia alisema atafuta kesi zote but hajaainisha hayo madhambi unayodai. Hivyo ni vzr ulieleze jukwaa hili hayo madhambi ya Lema!!!
 
Inaonekana uko ndotoni unaota, hata hujui kuwa Mdee na wenzake ndo wameistaki chadema mahakamani.... Kifupi hii ya Samia kukubali mualiko wa Chadema imewaumiza sana vijana wa Lumumba [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…