____________________________________________________________________
Katiba ya Zanzibar ya 1984
SURA YA KWANZA
ZANZIBAR
Sehemu ya Kwanza
Zanzibar
1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
2.Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi.
3.(1) Kutakuwa na Muhuri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ambao alama yake itakuwa kama itavyokubaliwa na sheria iliyotungwa
na Baraza la Wawakilishi.
(2) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo wa
kuweka kitu chochote kitachokuwa kielelezo cha Serikali kama
itavyokubaliwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
4. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria
nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote
inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu
na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafia
Soma zaidi :
Source :
Katiba ya Zanzibar, toleo la 1984 pamoja na masahihisho ya 2010