Kitendo cha kuwakatalia Wakurugenzi wa Kenya na kuruhusu wengine ni ubaguzi

Mkuu utakuta huyu aliyeleta hii habari ni Mkenya,na Wakenya ni wabinafsi sana , sijui analia nini wakati tuna Wakenya kibao hapa Tanzania na wengine wana vikampuni vyao vya mikobani,analia sababu anajua kwa ubinfsi wao vile vitenda vyote vingekuwa vyao, Ni afadhari mara mia huyo Mmisiri kuliko Wakenya,
 
Hujuitabia za wakenya hivyo acha watu wafanye kazi zao na wewe fanya kazi yako
 
Mbona ame-build case yake vizuri tu?? Hii Tanzania is a sovereign state imeingiaje kwenye hii hoja??
 
Wahindi, wachina na waarabu wamejazana hapa huku ndugu zetu tukiwakatalia
 
Mkuu ni visasi vya kuachwa nyuma kimaendeleo
 
Hatuhitaji majasusi na wahujumu wa uchumi wa nchi yetu. Bado somo la pression air na meneja wake mkenya tunalo kichwani. Wenye kufikiri na kuona kwa undani tulielewa jinsi pression air na meneja wake walihusika kuhujumu air tanzania.
 
Kama hao Wakenya wana uwezo mkubwa sana katika utendaji waende wakaajiriwe Uganda, Rwanda n.k

Afrika mashariki ni kubwa sana, mbonaTanzania huwahailalamiki kicha ya wabongo kunyimwa fursa huko Kenya.
Mbona huko Rwanda na Uganda pia wapo .... Elimu ya Kenya iko juu kulinganisha na nchi zote za Africa Mashariki!!
 
I
Ishu ni kwamba wananyimwa wa Kenya kwa kusema hata watanzania wapo wenye sifa matokeo yke hawapewi watanzania wanapewa watu wamataifa mengine tena ya mbali.
Inaelekea kuna bifu kubwa sana kati ya hizi mamlaka mbili ambapo sisi raia hatuzijui. Hapa Tz kuna makampuni mengi sana wakurugenzi na watendaji ni wageni na tena wanabadilishana wao kwa wao for years. Kwanini shida inakuka kwa wakenya tu. Labda usalama wa taifa wana taarifa mbaya na hao watu.
 
Mtachoka ninyi wakenya mnaodhani kuwa tanzania ni shamba la bibi. Sisi wenye nchi hatutachoka kuwaambia mpaka mtakapoelewa.
Kwa hiyo shamba lako kuliwa na Wa-Misri na Wahindi sawa, lakini sio Wakenya?

NI watu walio na raisi wa aina fulani ndio wanakuwa na mawazo kama haya
 
Huyo anajibainisha ni raia mTanzania mhamiaji toka Kenya. Inaonyesha uKenya haukumtoka, bado anapenda sana nchi yake ya asili.
 
Mleta mada angeweka sifa za hao waliokataliwa na hao ambao wamekubaliwa. Haitoshi tu kusema waKenya wamekataliwa hata bila kuonyesha 'qualifications' walizokuwa nazo kulinganisha na za hao waliokubaliwa.
 
Issue kubwa siyo wakenya tu hata hao wengine wawekwe pembeni, utaratibu uwekwe wa kupeleka mtaalamu wa kiwanda chako kwenda huko Kenya kujifunza au aje mtaalamu kufundisha jinsi ya kuiongoza hiyo nafasi then alipwe arudi kwao ili kuinua watu wetu wa ndani na kweli hawana skills na ujanja nje ya elimu ya darasani wakikabiziwa kampuni wanaiporomosha chini, wenzetu wapo juu hilo tusikatae imagine tu wanamakanisa mengi lakini huwezi kukuta wanafanya mikutano na kwenda kanisani katikati ya wiki na Kama ni msikiti wanatenga ofisi moja ya kuswalia yaani hakuna kupoteza muda weekdays ni kazi na kuheshimu kazi, ikija kwenye skills wapo mbele hivyo kampuni vipeleke huko watu wao kwa mafunzo ili kuondoa hizi kesi za kuajili watu wa nje.
 
In fact, mtoa mada atakuwa Mkenya. Tanzania ni nchi huru wacha ifanye maamuzi inavyopenda. Wakenya hawana quality hiyo tunayoifikiria kuwa wanayo. Sana sana wanaongea Kiingereza na kuchimba mikwara tu sehemu za kazi. Hamna lolote hawa. Mfano nzuri tazama taasisi za kibenki za Kenya zilizopo hapa zinazoendeshwa na Wakenya ukiondoa DTB inayoendeshwa na Mkenya Mhindi. NCBA, Equity zote ziko hoi sana. KCB imekaa miaka 11 bila kubreak even. Let Kenyans remain at their homes. Tunao baadhi ya Wakenya katika bodi mbalimbali kazi yao ni kuchonga madili na kurekebisha is na was tu kwenye documents zilizoshiba issues.
 
Soma alichoandika vizuri uelewe
 
Kwani kuomba kibali ni lazima upewe?

Au ombi kwenu Wakenya ni amri?

Kwa hiyo kama muomba kibali ni hatari kwa usalama na ustawi wa nchi apewe tu kwa kuwa ni Mkenya?

Acheni ujinga zenyu Wakikuyu
 
Tusubiri mtanzania Jeremiah Sanga akawe bosi wa SafariCom
 
Uzuri wa security screening sio lazima wanaokunyima kibali wakupe sababu za kwa nini wanakunyima.

So kuna baki na speculation kama hizi za mtoa mada "labda ubaguzi" "upendeleo" "chuki" nk. Ambazo kimsingi hazina nguvu kisheria kwa alienyimwa kibali kulalamika kisheria.

Kwenye screening kuna vitu vingi sana ambavyo huangaliwa kimsingi kutokana na chunguzi fulani mnaweza kuamua watu kutoka taifa fulani hamtaruhusu wapate vibali vya nyadhifa fulani katika kulinda mnachoamini hakitakuwa salama ikiwa mtu huyo atapewa access fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…