Kitendo cha Lema na Familia yake kupewa Asylum Canada kinaashiria Taifa limeanza kutengeneza wakimbizi wa kisiasa, jambo ambalo halina afya


Bora ukaishi jobless huko Canada kuliko kuwa waziri kondoo hapa nchini.
 
Huyo Lissu angefanya vijiji viwe mjini? Una mawazo ya kiboya
Kwanini mo dewji ni tajiri na wewe ni masikini? Kwanini msiwe sawa? kwanini Tanzania ba
ukishakuwa shabiki wa chama cha kijani you become a fool it doesn't matter how far you went to school.your cannot distinguish wrong and right you become completely useless
 
Hujitambui wewe, unasema ingewezekana mngehama wote wala huelewi kanada wamekuwa wakitangaza watu waende huko kuongeza nguvu kazi? Si muende sasa

Mnadandia mambo msiyoyajua
 
Ukitaka kujua kwenda Canada ni kuula kimaisha, leo hii Wacanada waseme wanaotaka kwenda Canada waende, uone kama hamjabaki wazalendo uchwara tu hapa nchini. Yaani kwa kwenda Canada atakuwa na maisha bora kuliko aliyokuwa nayo hapa akiwa mbunge.
Masikini siasa unayoijua ni ya chadema tu wala huelewi siasa za dunia

Unachoandika ni aibu
 
Uingereza ilimpa Oscar Kambona hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa kwa kutofautiana na Mwalimu Nyerere. Mwisho wa yote alirudi mwenyewe Tanzania, Mwalimu akingali hai, akaanzisha chama cha siasa ambacho hakikuwa na mafanikio yo yote hadi akafa.
Ujeremani nayo ilimpa Joseph Kaselabantu hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa kwa kutofautiana na Mwalimu, na walidiriki hata kumpa uraia. Mwisho wa yote alirudi mwenyewe, Mwalimu akiwa bado hai. Hakuna mtu aliyeshughulika naye hadi akajifia.
Tusubiri tuone ya wakina Lissu na Lema.
 
Madeni
 
Ukimbizi wanajitengenezea wenyewe, mbona huo Ubalozi wa Canada haukumuuliza Lema kipindi akiwa jambazi wa kuiba magari aliua watu wangapi kama kweli kafanyiwa veting ya kutosha kabla ya kupewa hifadhi ya ukimbizi?
Kiongozi huo ni uchochezi, ina maana vyombo vya usalama, tume ya uchaguzi, bunge na serikali ya JMT kwa ujumla hawakujua kwamba Lema alikuwa jambazi na aliua watu? Ilikuwaje mtu wa aina hiyo awe mbunge? Ama unataka kusema serikali yetu inakumbatia wahalifu?
 
Hili si jambo jema kwa nchi yenye hadhi yakupokea wakimbizi na kusuluhisha migogoro ya nchi nyingine.
Matukio mabaya ambayo hayakujulikana hatua zilizo chukuliwa na vyombo vya usalama/serikali vinachangia kwa baadhi ya ndugu zetu kulazimika kuwa wakimbizi.
Kuna vigezo na taratibu ngumu sana mtu kukubaliwa kuwa unayo haki ya kupewa ukimbizi, kama Canada wamekubali kwamba Lema na familia yake wanayo haki ya kupata hifadhi ina maanisha kwamba wamejiridhisha na sababu za wao kuomba ukimbizi, hivyo viongozi wetu wajue suala hili sio la kubeza hata kidogo.
 
Hawana unyama huo, usitake kuleta vitisho vya kishamba. Utakiwe mabaya na mzungu kwa lipi? Nchi hii bado tuko kwenye elimu ya kunawa mikono ukitoka chooni, ndio kuwe na wazungu wasiotutakia mema?
Skripal na binti yake wala hujawasahau nina hakika! Walifanywa specimens!!! Unataka hivyo hivyo hutaki hivyo hivyo.
===
Mkuu, waweza kujiunga na Lema ule ubweche wa bwelele baada ya kuukosa kwa Mzee Rungwe. Ha hahaa!

Wakuu, mwenye masikio na asikie, mwenye macho atazame na mwenye pua anuse! Dunia hii hakuna kitu cha bure!!.

Mkuu, Tindo wala 'sikutishi kishamba' (ndiyo lugha zenu za kifedhuli na kejeli).

Kwa taarifa yako, Mashirika makubwa ya kijasusi ya nchi kubwa na zenye nguvu yalikuwa yanatafuta kwa udi na uvumba sampuli za damu za raia wa nchi masikini ambapo mahasimu wao kijasusi walikuwa wamekita mizizi! Na hiyo ni sehemu ndogo sana ya 'ubaya ufanywao' kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti zinazoheshimika. Na si miaka mingi ujue. Hiyo tu, ikusaidie kujua kuwa mbali ya Tanzania kuingia uchumi wakati bado nchi hasimu za wezakuwa kututumia kama "uwanja wa mapigano ya kijasusi"!

Na sasa kwa tamaa za baadhi ya wenzetu na kushindwa kujikubali kuwa wana uwezo kusimama wenyewe wanajikuta wanajipeleka kwenye " mdomo wa chatu huku wakijipia vigelegele".

Kumbuka kuimarika kwetu kama nchi, kuna kera sana waliozoea kutudhulumu.
 
Lema sio mheshimiwa
Tupunguze chuki/jazba, maana kwenye uheshimiwa hata wewe umo. Tukiondoa nafasi aliyokuwa nayo Lema kiuongozi, bado anaingia kwenye kundi la waheshimiwa wananchi ukiwemo na wewe.
 
Ukimbizi una vigezo vyake, na moja ya kigezo kikuu ni usalama wa muhusika, kama nchi flani imempa mtu hifadhi ya ukimbizi ina maanisha imejiridhisha/ina fanyia uchunguzi maombi ya hifadhi kwa muhusika.
Nchi kuwa katika utulivu haimaanishi kwamba kila raia yuko salama, na pia nchi kuwa katika migogoro haimaanishi raia wote wako hatarini.
Hata raia kutoka nchi mbali mbali zenye migogoro wapo walio kubaliwa maombi ya ukimbizi katika nchi walizoomba hifadhi, na wapo walio kataliwa maombi yao kwa kigezo kikuu cha usalama wa muombaji kule anakotoka.

Ni kweli wazungu sio wajinga, na mabalozi wao wapo kweli na wanajua kila kitu, mfano mzuri ni hivi majuzi mabalozi hao hao walipo funga safari ya kumpeleka Lissu airport chini ya uangalizi wao. Hii ni hatari isiyo elezeka yaani mtu unakosa usalama ndani ya nchi yako adi inabidi wageni ndio wachukue jukumu la kukulinda.

Haya yanayo tokea ni mambo mazito na yakufikirisha sana, hivyo tunapo yaona mepesi kwa kigezo cha mtu kukosa ubunge inaweza kujengeka hisia kwamba tunaunga mkono maovu yanayo wakuta ndugu zetu.
 

Achana na hizo conciperancy theories ambazo unazitumia kujenga hoja za vitisho, kana kwamba hatujui lolote. Kwahiyo hayo mashirika ya kijasusi yalikuwa yamesimama shughuli zao walikuwa wanangoja Lema apate ukimbizi, kisha ndio waanze kuimplement huu utapeli unaousema hapa? Ni kipi wazungu wananikosa hapa kwetu wakikitaka kisa tumeingia huo uchumi wa chini wa kati?

Kama ni uchaguzi wote tumeona uhuni, ushenzi na uhayawani wa wazi uliojitokeza, je udhalimu ule umefanyika kwa hizo sababu zako ulizoweka hapo juu? Ni kipi so special ambacho wazungu wamekikosa hapa nchini mpaka wawe na chuki na sisi? Hayo madini hadi tunavyoongea wazungu ndio wanayachimba, na wala sio Lema aliwaruhusu au wanamtegemea yeye awaruhusu. Hizi story eti wazungu wamechukia sisi kuingia uchumi wa chini wa kati, ni story za wakomunist wenye mawazo ya kizee. Eti tumeimarika kiuchumi, nimecheka kwa nguvu, yaani kuwa na flyover, reli ambayo hata Morogoro haijafika ndio wazungu wachukie? Kwahiyo kuimarika kwetu kwa uchumi kuna mahusiano gani na dhuluma kwenye box la kura, ili ccm itawale kwa shuruti?
 

Peleka utoto mbali, kwahiyo kila anayedaiwa leo akienda ubalozi wa Canada atapewa ukimbizi wa kisiasa? Uza ubongo ubongo huo dogo, maana ni hasara kuendelea kukaa nao.
 
Amekimbia madeni yake yaliyosomwa bungeni ya milioni zaidi ya 400?

Lema unazidi kuwachafua zaidi wachaga, dawa ya deni ni kulipa siyo kukimbia na kujifanya mkimbizi feki, sasa umekimbilia kwa wazungu watakupa kazi ya kuosha vibibi na vibabu.
Kwani alikwambia hiyo kazi anaichukia ? pengine anaipenda zaidi kuliko kazi aliyokuwa nayo
 

Ati “...Familia yake itaishi kwa raha na watoto watasoma vizuri zaidi ya hapa...” Hivi unadhani ukimbizi katika mataifa ya magharibi ni sawa na ukimbizi kwenye mataifa ya dunia ya tatu?

Hakuna kambi za wakimbizi huko; hakuna kula kulala wala hakuna cha bure. Msaada mkubwa unaopata ni kibali cha kufanya kazi ili uweze kuendesha maisha yako!
 
Haahaaaa....
 
Magufuli na genge lake watawajibika siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…