Kitendo cha Rais kusimamisha hotuba kisa Adhana ya waislam imakaaje hii kitaifa?

aisee hapo hakuna baya lolote,wala siyo udini,ni heshima kwa wananchi,serikali haina dini ila watu wana imani zao na dini zao,kwenye kuapishwa mbona wanashika bibilia ama msahafu na hatuhoji,tupunguze kuwa vijana wa hovyoo eti "WAKRISTO TUVUMILIE" uvumilie nini?
 
Mkuu, kitaifa imekaa vizuri tu wala hakuna tatizo. Na yeye alisema kuwa ni vema kuheshimu mila na tamaduni zetu.

Hata Rais Uhuru Kenyata alikatisha hotuba yake Adhana ilipoanza kusikika sio tu mbele ya watanzania bali mbele ya viongozi wa kimataifa na kimsingi aliheshimu jambo hilo ilhali yeye ni Mkristo kama wewe.

Sasa sijui wewe umepatwa na hisia gani kiasi uone ni jambo la kujadili.

Lakini pia eneo lile la uwanja wa mpira ni karibu sana na mahala msikiti ulipo. Wote wanatumia vipaza sauti, sio rahisi kusikilizana ikiwa nayeye angeendelea kuhutubia.

Mwisho, utaumia roho bure kwa kuona hata jambo dogo hilo wewe unakwazika. Ingekuwa vibaya kama na wewe umelazimishwa kufanya hivyo bila hiari yako.
 
Mbona Hata Rais Uhuru Kenyatta alifanya hivyo wakati wa mazishi ya Magufuli pale uwanja wa Taifa? Ni suala la kuheshimu Dino ya Mawenzi on tu.
 
Ameheshimu watu wake ambao wana imani ya kiislam...Big up mama kwakua na heshima kwa imani za raia wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…