Kitendo cha Yanga kumleta Koffi Olomide ni ujanja wa kujaza uwanja kwenye siku ya Wananchi, hawana watu wala nini

Kitendo cha Yanga kumleta Koffi Olomide ni ujanja wa kujaza uwanja kwenye siku ya Wananchi, hawana watu wala nini

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ikiwa kama tunataka kupima uwezo wa timu kujaza mashabiki kwenye kinachoitwa Yanga Day , basi ni vema tuache kujidanganya kutumia ujanja ujanja kama huu ambao yanga wanautumia.

Kitendo cha kumleta Mopao uwanjani hii inamaanisha hata mimi Mwanasimba lazima nihudhurie tu , sisi wengine ni wapenzi halisi wa Rhumba na mimi ni mpenzi wa kutupwa wa Koffi , sasa kwenye nchi ambayo uchumi umekufa kiasi cha mapromota kushindwa kuleta mwanamuziki yeyote kwa miaka 8 , halafu inatokea nafasi ya kucheza Rhumba la Koffi hatuwezi kuacha.

Kwahiyo hata mkiona siku yenu watu wamejaa sana mjue sisi wengine tutakuja kusakata Rhumba tu , msije mkadhani MNA WATU , ukweli ni kwamba hamna lolote , kama mnabisha muondoeni Koffi Olomide muwekeni Konde Boy halafu muone nani atakuja.

 
Ikiwa kama tunataka kupima uwezo wa timu kujaza mashabiki kwenye kinachoitwa Yanga Day , basi ni vema tuache kujidanganya kutumia ujanja ujanja kama huu ambao yanga wanautumia .
Mbona wakati Mikia wanamtumia Diamond kujaza watu hukuona kwamba ni ujanja ujanja?! Au umesahau kwamba huu ujanja ujanja umeasisiwa na kina Babara?!
 
Huu ni ushabiki maandazi japo me ni Simba ifike kipindi ushabiki wa kipuuzi tuuwache unaua mpira wetu mbona Msimu uliopita kwenye hilo tamasha lao walijaza bila koffi olomide mbona sisi Simba tulimleta Diamond kwenye tamasha letu la Simba Day? Hao wasanii wanaletwa kwa lengo la kunogesha Tamasha.
 
Huu ni ushabiki maandazi japo me si Simba ifike kipindi ushabiki wa kipuuzi tuuwache unaua mpira wetu mbona Msimu uliopita kwenye hilo tamasha lao walijaza bila koffi olomide mbona sisi Simba tulimleta Diamond kwenye tamasha letu la Simba Day? Hao wasanii wanaletwa kwa lengo la kunogesha Tamasha.
we yanga au simba?
 
Tamasha la mwananchi lililopita watu walijaa kupitia kiasi milango ya uwanjani ilifungwa mapema lakini bado watu waliokua nje walikua wengi Sana wakitaka kuingia ndani hakukua namsanii yoyote mkubwa kutoka nje ya Tanzania Sasa hii inayokuja sijui itakuaje.
 
Ikiwa kama tunataka kupima uwezo wa timu kujaza mashabiki kwenye kinachoitwa Yanga Day , basi ni vema tuache kujidanganya kutumia ujanja ujanja kama huu ambao yanga wanautumia...
Nimependa utani wako vijana wanatelemsha matusi si unajua malezi siku hizi bwana. Mm mwenyewe mwnasimba nutaenda kusakta rumba na toto ya mboka. Wanayanga hamjui utani acheni hasira
 
Back
Top Bottom