Acha upotoshaji! Wewe mafanikio makubwa unayapimaje? Acha kutujaza ujinga na wa kutuaminisha bila Chama fulani kuwa madarakani hakuna mafanikio. Tunataka nchi iongozwe na mtu yoyote au chama chochote chenye Sera Bora.Nitolee mfano wa nchi yoyote ya Africa iliyo badili utawala wake wa vyama na kupata mafanikio makubwa katika nyanja zote ulizo ainisha hapo juu ! Ngoja nikurahisishie orodha,
1.Zambia ?
2. Malawi?
3. Kenya?
4. Libya?
5. Comoro?
6. Sudani kusini ?
7. Ivory coast ?
8. .......
Acheni kupumbazwa na political rhetoric za wapinzani, hakuna namna wanaweza kufanya lolote la tofauti zaidi ya ulaghai na kurudisha nyuma nchi ! Mara waseme CCM haijafanya lolote kwa miaka 60 ! Mara hao hao tena majukwaani wanaorodhesha mafanikio makubwa yaliyofanywa na tawala za awamu ya kwanza hadi ya nne [emoji15] wakionesha kua haya mambo makubwa anayofanya rais Magufili hakuyaanza yeye bali hata Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na wakoloni wa ujerumani na waingereza pia walifanya makubwa sana kwa nchi hii! Sijui hua wanajitoa ufahamu ? Mara waseme wanataka maendeleo ya watu na sio vitu ilhali vitu hivyo hivyo ndio wanatumia pia kama ndege zetu, barabara zetu, hospitali zetu, shule zetu na vinginevyo! Hao hao pia wameanza kuwaahidi wananchi kule Mufindi, Rukwa, kigoma kuwajengea barabara na miundo mbinu mingine wakisahau hayo ni maendeleo ya vitu! Jamani !
Very inconsistent assertions! Worse enough their arguments are embbed in hatred and deep sense of division among social fabric ! Very bad, kwa mfano kuwaita wana CCM eti maCCM ! Sowing very dangerous seeds of hate in our mother land !
Kimsingi, Umejiconfine kwenye hoja za kitoto. Kuna Mambo mengi ya msingi yanazungumzwa na TL. Kwa mfano suala la FAO la kujitoa. Wewe unaona ni sawa hiki kinachofanywa na Serikali yetu? Huoni kama hii ni dhurma ya wazi? Kama Sera hii ni nzuri, kwann isiwahusu Wabunge na Mawaziri?Wao hawapendi kuja kufaidi baada ya miaka 60 kama wafanyakazi wa chini walivyowafanyia??
Suala la Katiba Mpya, utakuwa ni mwendawazimu Tu kama utapinga hili. Sote tunakubaliana kuwa Katiba yetu ya Sasa ni Mbovu. Na wakwanza kutuambia haya ni CCM. Baada ya Kula mabilioni ya Kodi zetu, Mchakato wa Katiba Mpya ukasitishwa. Tunataka Katiba Mpya Sasa.
Usipotoshe, TL akiwa Mufundi alisema, kuna haja gani kujenga Daraja la kupita juu ya Maji Dar Kwa Mabilioni wkt Huku Kwa wazalishaji, Barabara ni Mbovu hivi??Kimsingi Daraja lile ni just Luxury. Kuna mifano mingi ya namna hii. So ni upotoshaji kusema TL anapinga Ujenzi wa Miundombinu, anachosema ataprioritize kitu ambacho sasa hivi hakipo. Ni kikundi cha watu wachache wanaamua na kutekeleza miradi mikubwa kihuni Kwa gharama za wananchi walio wengi.
Ili umwelewe TL, jitahidi kusikiliza na kuelewa speech nzima za TL. Usisikilize vipandevipande vinavyopostiwa na akina Steve Nyerere na Pierre.