Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Wapi nimemaanisha hivyo?Conclusively unamaanisha utiaji saini wa mkataba huu mmoja,kwasasa upewe baraka,huku tukishughulikia kuweka mfumo imara?
Unaweza kunipa nukuu hiyo?
Unajua kusoma kwa ufahamu?
Watanzania wengi wana tatizo la kufikiri kwa style ya one track mind.
Yani kwao, ukimshambulia Magufuli, basi lazima wewe ni Chawa wa Mama. Ukimshambulia Mama, basi wewe ni Sukuma Gang.
Ndiyo maana wewe unauliza hilo swali la false dichotomy.
Mimi sioni tofauti kubwa kati ya Magufuli na Samia.
Nakwambia hivi, hata huyo Samia aliyesaini mkataba huu, ni product ya Magufuli.
Magufuli angekuwa kiongozi mzuri hivyo mnavyotaka kutuaminisha, Makamu wake asingesaini mkataba mbaya kama huu.
Magufuli angekuwa kiongozi mzuri hivyo, hao mawaziri wake wengi waliopo mpaka leo wasingekubali kuwa sehemu ya serikali iliyokubali mkataba huu.
Magufuli angekuwa kiongozi mzuri hivyo, bunge alilolipitisha mwenyewe kwa kukata watu, kununua wapinzani na vituko vingine vyote lisingepitisha mkataba huu.
Magufuli angekuwa kiongozi mzuri hivyo mnavyomsema, angepeleka bungeni miswada iwe sheria za kushurutisha uwazi katika mikataba ya serikali. That is systemic change. Magufuki alikuwa anapiga kelele za maigizo tu, hakufanya systemuc change.
Na Watanzania wanavyopenda maigizo wamemkubali. Bika ya kujiukiza, hivi, huyu akifa leo, haya maigizo yake yatatufikisha wapi?
Leo kafa, tunaona yale maigizo yake yote hayatupeleki popote.
Uwazi ni tatizo kubwa sana.
Nikiandika makala mwaka 2011 kuhusu uwazi.
Hii hapa.
A campaign for greater transparency: Tanzania government contracts
Should government contracts be open to the public eye? Kiranga, Vijana FM's guest blogger, discusses this need.
www.vijana.fm
Magufuli hata hakufanya lolote kuleta uwazi. Zaidi, kafanya the opposite. Kaleta sheria za kubana uhuru wa habari na uwazi. Mpaka majadiliano ya bunge tu hatukuweza kuyaona live.
Kwa nini mna mu whitewash huyu mtu aliyetuletea systemic failure kwa sababu mnafikiri tu asingesaini mkataba huu?
Why are you people so narrow minded?
Hivi mnaelewa kwamba kuna mikataba mingi sana hamjaiona na mmeona huu mmoja kwa kuvuja tu?
Hivi mnaelewa Magufuli alikuwa na nafasi ya kuondoa usiri huu, na hajaondoa?
Hivi mnaelewa usiri huu ni chaka kubwa sana la rushwa na madudu mengine mengi ambayo hata hatujaanza kuyajua?
Sasa hapo mnamsifia vipi Magufuli?