Kitila Mkumbo acha kuchukia juu ya ukweli anaousema Lissu, hayati JPM asingefanya huu uozo. Muache aende Chato kueleza ukweli

Kitila Mkumbo acha kuchukia juu ya ukweli anaousema Lissu, hayati JPM asingefanya huu uozo. Muache aende Chato kueleza ukweli

Kitila wewe ni kielelezo cha Unafiki wa watanzania..Mm sieezi kamwe kusoma ili niitwe Dr au Prof mnadhalilisha sana wewe na Msukuma tofauti yenu ni ipi?? Kwenye uelewa wa mambo...Ulikua unapiga kelele sana kumbe njaa..ulipopewa Ukatibu Mkuu akili zile za kelele zikaisha...
 
Kumlaumu Magufuli kuhusu bunge ni sawa na zile lawama za watu wenye kumlaumu Nyerere kwa kuona matatizo yote ya hii nchi aliyasababisha yeye.
 
Watanzania wengi hamuwezi kufanya siasa za kidhahania zinazoangalia sera na hoja bila kuangalia watu?

Mtu ambaye kaendesha nchi kwa mabavu, kalifubaza bunge, kaua upinzani bungeni, kakata majina ya watu machachari, mpaka tumekuwa na bunge dhaifu lililokosa upinzani na kupitisha IGA.

Leo wapinzani waliomsema sana wanaenda kumshobokea mtu huyo huyo?

How come?


Kwa hii hali inavyoenda naona kabisa karata zilipowekwa mezani uchaguzi mkuu 2015, hazikurudi mfukoni hata baada ya kutolewa mchezoni.

Hii mambo ya Bunge la chama kimoja na mengine ya upinzani ni Kama yaliachwa yatokee na yatimie strategically tu, ili Haya yanayotokea sasa hivi iwe rahisi Kama ambavyo imekua.

Sioni kabisa vyombo vyetu vyenye mamlaka ya usalama wa nchi na watu wake, mali zao na “wadau” wa nchi wakiachia hayo yatokee bila wao kuhitaji yatokee hivyo.

Halafu kwani mzee Mbowe alipotoka jela alienda wapi kwanza?




Politics ni Polifix.
 
Pamoja na ukatili wake kwa wanaompinga kwa hoja wakati wa utawala wake, JPM asingethubutu kutuingiza kwenye uchafu huu, aliipenda Tanganyika vibaya mno na ndiyo sababu alivunja mikataba ya hovyo hovyo na ndiyo maana tuna makesi kibao mahakama za kimataifa.

Lissu upo sahihi, nenda kawajuze na zwanachato kwamba JPM hahusiki na uchafu huu wa kuuzwaji wa Bandari zetu kwa mwarabu afu kwa mkataba wa milele.
Hivi kulikuwa na ulazima wa Lissu “kumtakasa” Magufuli ili hoja yake dhidi ya hujuma za CCM (awamu ya sita) ieleweke? Naona kama Lissu amejipagawisha kupita kiasi katika hili. Ni zaidi ya mhemuko. Amevuka mstari.

Sikutarajia Lissu (of all people) amtumie Magufuli, andante malaika hivi, ili kujenga hoja ya kukengeuka kwa Rais wa sasa hasa ikieleweka kuwa wote ni sehemu ya uozo wa CCM unaolitesa taifa hili. Hawa wote wamekuwa na mchango hasi sana katika utawala bora miaka ya karibuni. These people are basically full of evil/crafty intentions. No need to reference them.
 
Alisema lakini "TUTAMKUMBUKA" Nani alijua TUTAMKUMBUKA kwa lipi? Aliongeza hakutuacha gizani "KWA MEMA NA SI MABAYA" alifahamu kitu ndani yake ndani ya chama chake na wanaomzunguka kuwa akiondoka watakuwa na kiu ya matendo yao nao watatugeuza asusa nasi TUTAMKUMBUKA!
Tatamkumbuka kwa kukataa katiba mpiya
 
Back
Top Bottom