Kitu gani kilikuwa kinamfanya Magufuli amheshimu Edward Lowassa?

Ila Mbowe na genge lake walichemsha sana kumpokea huyo mzee na kumpa nafasi ya kugombea urais. Ni kama waliwapa ccm escape route rahisi ya agenda ya ufisadi. Ni kitendo kile kimepoteza haiba ya cdm juu ya mapambani yao ya ufisadi. Kama tungekuwa na tabia ya uwajibikaji, Mbowe hakupaswa kuendelea tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwa blunder ile.
Hata Sasa mnaweza kumtoa mkitaka.

Anyway huenda alifanya hayo akiamini ujio wake ungeinufaisha Cdm, na kweli alivuna wabunge wengi.
 
Ni nadra sana kumsikia akimzungumzia Lowassa vibaya. Kuna watu ambao inaonekana Magufuli alikuwa anawaheshimu. Na mmoja wapo alikuwa ni Lowassa.

Sifahamu kwa nini. Najiuliza sana kwa jinsi ambavyo Magufuli alikuwa na dharau kwa watu ambao aliona either hawana elimu au uwezo flani kisiasa, au aliona kuwa walikuwa wanafik na walioharibu chama. Nini kilimfanya amheshimu Lowassa?
Kumbuka Lowassa akiwa CCM pale Dodoma 2015 alishawishi kambi yake yote imuunge mkono Magufuli badala ya Membe baada ya mpasuko na kuimba tuna imani na Lowassa na jina lake kukatwa. Na hapo JPM akapata kura nyingi za Mkutano Mkuu kupitia Kura za Lowassa na kisha kupata ushindi wa kugombea urais kupitia CCM. Historia inasema hivyo inaweza ikawa sababu ya JPM kumuheshimu Lowassa.
 
Kwa mgombea yupi huyo wa Urais ?

Dr. Slaa ndio aliyekuwa sahihi, Lowassa alikuja na utapeli kuwa alikuwa aje na wabunge 50 toka CCM kitu ambacho si kweli. Ifahamike CHADEMA ndio chama kilichofanya kazi ya kisiasa kuanzia 2010 baada ya uchaguzi mpaka 2015. Ndio chama kilichofanya mikutano mingi nchini kuliko chama chochote cha siasa ikiwemo ccm. Ndio kilichotoa elimu ya uraia kuliko chama chochote cha siasa. Hayo yote yalifanyika Lowassa akiwa ccm. Kama ni rahisi kupata kura 6m+ ukiwa na miezi miwili kwenye chama, Lowassa angeenda TLP au NCCR kisha apate kura zile. Msitake kumpa Lowassa sifa asiyostahili hata kidogo.
 
Ni nadra sana kumsikia akimzungumzia Lowassa vibaya. Kuna watu ambao inaonekana Magufuli alikuwa anawaheshimu. Na mmoja wapo alikuwa ni Lowassa.

Sifahamu kwa nini. Najiuliza sana kwa jinsi ambavyo Magufuli alikuwa na dharau kwa watu ambao aliona either hawana elimu au uwezo flani kisiasa, au aliona kuwa walikuwa wanafik na walioharibu chama. Nini kilimfanya amheshimu Lowassa?
Kwa maneno yake alisema ALIMSAIDIA kwenda kusoma NG'AMBO pale ambapo wako WALIOMBANIA.....

#Siempre JMT🙏
 
Kama ni rahisi kupata kura 6m+ ukiwa na miezi miwili kwenye chama, Lowassa angeenda TLP au NCCR kisha apate kura zile. Msitake kumpa Lowassa sifa asiyostahili hata kidogo.
Unadhani Lowasa hakuwa na mchango kwenu hata kupata kura 6m+.

Huyo Slaa mwaka 2010 alifika hata 4m ?...yaani Yale mafuriko ya Lowasa leo hii huyakumbuki ?
 
Mafuriko yalikuwepo bila hata Lowassa. Kwani kigezo cha kupata kura 2010 ndio kipimo cha kura 2015? Alikuwa na mchango gani wakati alikuwa akipanda jukwaani anasema kipaombele ni elimu elimu elimu, wala hawezi kuongea tena. Kama yeye ndio sababu ya kupata kura 6m+ akiwa ma miezi miwili, je alileta viti vingapi akiwa na zaidi ya mwaka ndani ya cdm. Msidhani hatujui nguvu kubwa ya cdm ilitokana na nini. Magufuli aligoma cdm kundelea kufanya siasa nchini sio kwa sababu ya uwepo wa Lowassa, bali ni kuepuka ukweli ambao ccm wasingeuweza na hawatakaa wauweze.

Cdm bila hata umoja wa ukawa, au ujio wa Lowassa ingepata kura nyingi na viti vingi vya ubunge + udiwani pia. Lowassa hakuwa chochote wala lolote. Lowassa namfananisha na mchezaji aliyeingia uwanjani dakika ya tisini na kukuta timu inaoongoza bao tatu, kisha yeye akafunga goli la nne kwa mbwembwe mtake ionekane bila yeye timu isingeshinda.
 
Kama mlifahamu ujio wake haukuwa mzuri kwenu kwa wakati huo (sababu ya ajenda ya kupinga ufisadi ) na bado Cdm ikampitisha agombee urais, ilionyesha Cdm haikuwa inajua inachokitaka.
 
king maker, Lowasa yule mzee hata nyerere aliona nguvu yake ndio maana siku mzee mamvi aliporudi chamani kamati kuu yote ya ccm walienda kumpokea pale lumumba
King maker ni yule mnyamwezi wa tabora aliyenunua tigo,lowasa hakua na pesa 1995 Wala 2015,Ila hao wenye asili ya Asia ndiyo wakimtumia
 
Kama mlifahamu ujio wake haukuwa mzuri kwenu kwa wakati huo (sababu ya ajenda ya kupinga ufisadi ) na bado Cdm ikampitisha agombee urais, ilionyesha Cdm haikuwa inajua inachokitaka.
Mchaga anafanya biashara pale,akasaidiana na marehemu mpemba,bilioni 12 waziache kivipi yaani!!!
 
Mafuriko yalikuwepo bila hata Lowassa. Kwani kigezo cha kupata kura 2010 ndio kipimo cha kura 2015? Alikuwa na mchango gani wakati alikuwa akipanda jukwaani anasema kipaombele ni elimu elimu elimu, wala hawezi kuongea tena. Kama yeye ndio sababu ya kupata kura 6m+ akiwa ma miezi miwili, je alileta viti vingapi akiwa na zaidi ya mwaka ndani ya cdm. Msidhani hatujui nguvu kubwa ya cdm ilitokana na nini. Magufuli aligoma cdm kundelea kufanya siasa nchini sio kwa sababu ya uwepo wa Lowassa, bali ni kuepuka ukweli ambao ccm wasingeuweza na hawatakaa wauweze.

Cdm bila hata umoja wa ukawa, au ujio wa Lowassa ingepata kura nyingi na viti vingi vya ubunge + udiwani pia. Lowassa hakuwa chochote wala lolote. Lowassa namfananisha na mchezaji aliyeingia uwanjani dakika ya tisini na kukuta timu inaoongoza bao tatu, kisha yeye akafunga goli la nne kwa mbwembwe mtake ionekane bila yeye timu isingeshinda.
Mkuu tind

Ifike mahali tutambue chama chochote cha siasa lengo lake ni kupata uungwaji mkono wa wananchi kupitia sanduku la kura ili kuunda serikali.

Si lengo la chama cha siasa duniani kote, kuwa chama kinachoshabikiwa tu kila uchaguzi unapofika na mwisho wa siku kushindwa kuunda serikali ama kupata wawakilishi kwa idadi kubwa ili kuunda serikali mbadala katika chombo cha wananchi.

Maamuzi ya CHADEMA mwaka 2015 yalikuwa maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Lowasa alikuwa ni USHINDI kwa CHADEMA kama mazingira yangekuwa katika uwanja ulio sawa.

Alikuwa na watu, ushawishi na zaidi ya yote alikuwa na uchumi uliokiwezesha chama hicho cha upinzani katika harakati zake za kushika dola. Kwamba Mbowe na "genge" lake walifanya makosa kutumia turufu ya Lowasa kukibomoa chama na kupoteza maono ya chama katika kile walichokisimamia?...je zilikuwa hesabu za kisiasa sahihi?...kwangu jibu ni ndio.

• Si jambo la ajabu vyama vya siasa au wanasiasa waliohasimiana kuunga na kuunganisha nguvu kushinda ama kuongeza ushawishi wao katika medania za kisiasa. Raila na Uhuru ni mfano mzuri.

• Ni ushabiki tu na upenzi ndio unaotusukuma kusema kwamba bila Lowasa CHADEMA ingepata viti vingi tu na kura zaidi ya walizopata katika uchaguzi ule.

Lowasa alikuwa ni "kura" na kama CHADEMA wangekuwa na msimamo kama wako juu ya Lowasa 2015 chama hicho kisingekuwa na wabunge wala kura walizopata mwaka ule mbali na uwanja wa mchezo kulalia upande mmoja.

Lazima tukubali, hesabu za kisiasa ni muhimu sana kuangaziwa katika vyama vyetu vya siasa. Kufikilia chama kuendelea kutokuwa na mnyumbuliko wa kisera, kiuongozi na kutumia fursa na mazingira mazuri yanapojitokeza yanayoweza kukuhuisha chama, ni vuashiria vibaya vya chama kwenda kuwa "chama cha upinzani kinachounga mkono serikali na chama tawala"
 
Ila Mbowe na genge lake walichemsha sana kumpokea huyo mzee na kumpa nafasi ya kugombea urais. Ni kama waliwapa ccm escape route rahisi ya agenda ya ufisadi. Ni kitendo kile kimepoteza haiba ya cdm juu ya mapambani yao ya ufisadi. Kama tungekuwa na tabia ya uwajibikaji, Mbowe hakupaswa kuendelea tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwa blunder ile.
Afadhali wewe umesema ukweli, tukisema sisi mnatuporomoshea matusi. Hiyo kitu ilinifanya niachane kabisa na chadema maana ilikuwa ni unafiki wa hali ya juu.
 
Lowassa hakuwa mtu wa harakati wala tishio la kumng'oa katika utawala wake. Kwa ufupi hakuwa na athari.
Lowasa alikuwa tishio kwa namna alivyokuwa na nguvu za ushawishi haswa kwa makundi yanayopiga kura sana...wanawake na vijana...udhoofu wa afya wa Lowasa nyakati zile wenda ndizo zinazokufanya umuone kama mtu asiyekuwa tishio kwa utawala ule. Lakini aliyeshinda alitambua nguvu za bwana huyu akijua fika kabisa yawezekana leo Lowasa hatumii nguvu zake za kisiasa kuniwekea ugumu katika uongozi wangu kwa sababu ya mdololo wa afya yake, lakini JPM aliona mbali kwamba magonjwa yanatibiwa na anaweza akapona na kutumia ushawishi kuniwekea mazingira magumu kuongoza, hivyo nimdhibiti mapema tena akiwa bado katika hali ya ugonjwa. Akafanya hivyo AKADHIBITIWA!
Hata Sasa mnaweza kumtoa mkitaka.

Anyway huenda alifanya hayo akiamini ujio wake ungeinufaisha Cdm, na kweli alivuna wabunge wengi.
Chama chochote kisichoweza kutumia fursa, nafasi na ushawishi ama kuingia katika makubaliano na kundi flani au mtu flani mwenye ushawishi kwa namna ya kutaka kujiongezea ushindi, na kung'ang'ania sera zake zile zile ni chama Mfu!...na kamwe hakitaweza kushika dola!
 
Back
Top Bottom