Tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi,Hakuna mgombea kutoka upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kwenye uchaguzi kumzidi Lowasa. Kidogo labda Mrema na kwa mbali Lipumba,hawa kina Slaa walipata kidogo sana.
Kwa hiyo huwezi kuponda Mbowe kumleta Lowasa, ukweli Lowasa alikuwa asset kwa wakati huo.
Hizi habari za ufisadi ni uzushi tu, kwani Magufuli aling'ang'ana kujenga mahakama ya mafisadi na wengi tuliamini ni kwa ajili ya Lowasa, lakini hakuna aliyemgusa,zaidi tuliona ufisadi mpya wa kununua wabunge.
Magufuli alikuwa anajua kwa hakika nguvu ya Lowasa ndio sababu alifanya juu chini kuhakikisha anamrudisha ccm,na yeye mwenyewe anampokea pamoja na kamati kuu nzima.