Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
unakataa ukweli ambao upo uchi kabisa... unadhani kwa nini mbowe alimkubali lowassa akaona slaa aende zake tu? lowassa alikuwa na nguvu sana na baada ya hapo aliachana na siasa kabisa. alishakata tamaa hakutegemea tena. na haitatokea tena cdm ikawa vile ilikuwa mwaka 2015
Mbowe alimkubal Lowassa maana alimpa hela, Slaa alikuwa na hela gani ya kumpa Mbowe? Lowassa hakuacha siasa kwa kupenda bali afya mgogoro.
KuP kurudi kwa mfumo wa vyama vingi,Hakuna mgombea kutoka upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kwenye uchaguzi kumzidi Lowasa. Kidogo labda Mrema na kwa mbali Lipumba,hawa kina Slaa walipata kidogo sana.
Kwa hiyo huwezi kuponda Mbowe kumleta Lowasa, ukweli Lowasa alikuwa asset kwa wakati huo.
Hizi habari za ufisadi ni uzushi tu, kwani hata Magufuli alipong'ang'ana kujenga mahakama ya mafisadi watu wengi waliamini ni kwa ajili ya Lowasa, lakini hakuna aliyemgusa, mahakama ikakosa wateja na sijui kama iliwahi kupata ukiondoa kesi ya mchongo ya Mbowe.
Magufuli alikuwa anajua kwa hakika nguvu ya Lowasa ndio sababu alifanya juu chini kuhakikisha anamrudisha ccm,na yeye mwenyewe anampokea pamoja na kamati kuu nzima.
Narudia tena, kama aliweza kuleta kura 6m akiwa na miezi miwili, sema alileta kura ngapi akiwa na mwaka mmoja. Kura za cdm zilipatikana kwa juhudi za cdm wenyewe kutokana na kufanya kazi yake ya siasa. Naona wote mnazunguka tu hakuna anayeonyesha nguvu ya Lowassa baada ya uchaguzi.
Magufuli hakuwahi kupambana na mafisadi, bali alikuwa anakomoa na kulipa visasi kwa aliohitilafiana nao kabla hajawa rais. Alimpokea Lowassa kwenye kampeni yake ya kujibrand ya kuunga juhudi, na sio kwamba alikuwa anamuheshimu. Labda ww ndio ulikuwa unaona ni bonge ya fahari kupokelewa na Magufuli. Isitoshe hiyo mahakama ya mafisadi hakuwa na nia nayo, bali alipora ajenda ya cdm ili kulazimisha kukubalika na umma. Hakuna mtu anayepambana na ufisadi akawa adui wa vyombo vya habari. Sana sana Magufuli alipambana na matumizi ya neno fisadi na sio ufisadi.