Kitu gani kilikuwa kinamfanya Magufuli amheshimu Edward Lowassa?

Alikuwa anajua kuwa bila Lowasa, yeye E3 asingekuwa Rais.

Ufahamu kuwa utawala ulimwandaa Membe kuwa Rais. Wakakata majina ya wote ambao wangesababisha ushindani kwa Membe. Wakamwekea membe washindani dhaifu, wale ambao waliamini wajumbe wa mkutano mkuu, hawawezi kuwachagua. Mmoja wa hao dhaifu kabisa alikuwa ni Magufuli. Mwenye nguvu kubwa aliyekatwa alikuwa ni Lowasa.

Waliotaka kumpa kura Lowasa, wakazira kupiga kura, wakatoka nje ya ukumbi. Baadaye wakaambiwa kuwa wenzao waliobaki ndani ya ukumbi wameanza kugawiwa karatasi za kupigia kura. Wakajadili, na haraka wakakubaliana kuwa kura zao wampe yule asiyetakiwa kabisa ili kumkomoa Jakaya. Na mtu huyo alikuwa ni Magufuli. Wakafanya hivyo.

Kwa ufupi, kura alizozipata Magufuli ndani ya CCM zilikuwa za Lowasa, na Magufuli alilijua hilo.
 
Jaribu kulinganisha uchaguzi wa serikali ya mitaa mwaka 2009 na ule wa 2014 utajua ukweli wa kulinganisha mwaka 2010 na mwaka 2015
 
2015 aliyechaguliwa na wananchi ni lowassa . aliyetangazwa kuwa rais ni magufuli . na hilo alikuwa akilitambua .
Hii chadme ya kwenye majiji tu ndio iishinde ccm 2015..?
Mkwe wake lowasa wa TRA asingesota jela kama Magufuli alimuogopa
na kutoka aliporudi CCM.
Lowasa ushawahi kumuona anamuongelea vibaya Magufuli???
Aliwaambia acheni siasa za harakati wanaufipa hamkusikia sasa join the chain mnaaibika.
 
Alimdharau kwa kujiona yeye ni strong enough kuliko Lowassa, akidhiirisha kwa kupiga push ups
 
Ni kwa vile aliujua ukweli kuwa Kwa kura halali Lowasa alishinda na ndiye alistahili kuwa Rais,yeye alikuwa Rais wa mchongo tu
 
Siku wakiweka wazi kura halali zilizopigwa utajua kwann Magufuri alikuwa anamheshimu El
 
Alidhani Lowasa ana uadui na the old CEO
 
Ile nguvu ya lowassa huwezi jidanganya kuwa hukuiona. Utakuwa unaficha kichwa chini ukidhani huonekani. Lowassa ndiye aliyebeba CDM mwaka 2015. Hilo la wabunge inawezekana walikubaliana but baadaye jamaa wakageuka na hilo huwezi laumu mtu. Dr. Slaa si alikuwa CDM sasa hivi yupo wapi?

CDM wenyewe wenye chama wanakubali nguvu ya Lowassa. Wewe kalindililye unajidai huoni. 😁
 
Alimdharau kwa kujiona yeye ni strong enough kuliko Lowassa, akidhiirisha kwa kupiga push ups
Then push ups hazikuonesha yupo strong kuliko ambaye hakupiga. Maana aliyepiga amefariki ambaye hakupiga yupo hai.
 
Hivi kwa nn watu wanasahau sana?
Tumesahau...
1.Friends of Lowasa
2. M4U
3.ULIPO TUPO
Ule mkutano Shehe Amri Abeid still unasemaj hakua na nguvu??

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwasababu kwenye uchaguzi wa 2015 Lowassa alimshinda Magu mbali tu
 
King maker ni yule mnyamwezi wa tabora aliyenunua tigo,lowasa hakua na pesa 1995 Wala 2015,Ila hao wenye asili ya Asia ndiyo wakimtumia
kaka ile ni combination ya huyo mmaasai na muasia na apo kila mtu ana jukumu lake ndio maana, baada ya muasia kuwauzia kijani tv na radio yake akamrudisha mmasai kundini bila tabu mpaka wale waliokua wanamtukana mmasai wakawa wanajichekesha tu akiwemo mwendazake
 
Afadhali wewe umesema ukweli, tukisema sisi mnatuporomoshea matusi. Hiyo kitu ilinifanya niachane kabisa na chadema maana ilikuwa ni unafiki wa hali ya juu.
wewe haukua CDM na haujui sayansi ya siasa inavyofanya kazi. in politics there no permanent enemy or friend but always a permanent interests
 
Kama mlifahamu ujio wake haukuwa mzuri kwenu kwa wakati huo (sababu ya ajenda ya kupinga ufisadi ) na bado Cdm ikampitisha agombee urais, ilionyesha Cdm haikuwa inajua inachokitaka.

Hakuna taasisi isiyofanya makosa, kama ipo nitajie moja leo hii.
 

Mkuu sipingi unachoamini, mimi nasimamia kwenye uhalisia na sio hicho usemacho. Kabla ya uchaguzi cdm ilikuwa na uungwaji mkono mkubwa, hata kwenye kujiandikisha watu walikuwa na hamasa kubwa sana wakiamini Lowassa ndio angekuwa mgombea wa ccm. Hapo ndio jina kitambulisho cha kura kilipewa jina kichinjio kwa ajili ya kumchinja Lowassa. Nakuhakikishia cdm ingepata kura nyingi kama Slaa ndio angekuwa mgombea. Na kikubwa haiba ya cdm ingebaki hata kama isingeshinda kiti cha urais. Kama Lowassa alishindwa kuwaleta hao wabunge wa ccm 50+ aliosema atakuja nao, unapata wapi nguvu ya kusema alileta viti vingi akiwa na miezi miwili chamani? Pesa alizotoa zilikuwa ni za nafasi yake ya kugombea urais na sio kwenye kampeni za wagombea wengine wa chama.

Acheni upotoshaji usio na tija yoyote. Weka idadi ya viti alivyoleta akiwa na zaidi ya mwaka chamani ili tujue nguvu yake.
 
Kweli lowasa alitukamata Sana Mwaka ule!!!Jamaa mtulivu hana majigambo LAKINI aliwapigisha kwata wapinzani Wake!!kama ndugu yangu Suleiman kova asingewatia wale vijana Wake wahesabu Kura kizuizini leo tungezungumza mengine aiseh!!!bora wangeweka kambi kule kenya kabisa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…