Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Mimi bila mambo ya chuo ingenichukua miaka mingi sana kuikanyaga Dar. Labda ningekuja kwenye msiba wa Shangazi mwaka 2014 na harusi ya binamu 2016.
 
Nimetoka chuo miaka 15 iliyopita.
 
Mimi niliselect vyoo viwili tu ikiwepo UDSM na vyuo vyote viwili vilinikubalia.
Cha kushangaza ni kwamba vyuo ambavyo sijaviomba viliniselect sijui taarifa zangu walizipata wapi na kwa nini walifanya vile.
 
Enzi hizo watu hawafiki dar hadi wapitie Kenya. Na hapo wakirudi, tunaambulia juice na mikate ya Kenya pamoja na story za kariakoo

At least mimi nilikuwa mjini kidogo, huko kijijini inaonekana uliwavuna sana mkuu 😁😁
 
Wenye uchungu kwa kusoma nje ya UDSM utawajua tu..!!
Labda mkuu uniambie what is so special with UDSM?

Mbona waliosoma hapo hawana tofauti yoyote na wale waliosoma vyuo vya juu ya ghorofa huku chini fremu za biashara.

Au tuambie wameifanyia nini hasa nchi zaidi ya kuzalisha machawa?
 
Enzi hizo watu hawafiki dar hadi wapitie Kenya. Na hapo wakirudi, tunaambulia juice na mikate ya Kenya pamoja na story za kariakoo

At least mimi nilikuwa mjini kidogo, huko kijijini inaonekana uliwavuna sana mkuu 😁😁
Hahaha.............yaani hilo jina tu kwamba unasoma Chuo Kikuu DSM lilifanya hata wakati wa kuelekea Chuo, unaagwa na Kijiji kuzima

Enzi hizo Mjumbe wa Nyumba 10 kama ana binti mzuri, anakwambia Kijana karibu nyumbani umsalimie mwenzio 😜

Hiyo fursa ilikuwa sio ya kuikosa 🀸🀸
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…