Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

UDSM ni well known.

Nimeweza kutunukiwa Shahada ya kwanza ya Sheria (Second Lower Class with Honours).

Kina wakufunzi wazoefu.

Ila VETA pia nimeenda na imeniokoa sana.

Wasomi nendeni pia VETA.
 
Ulichukua umaamuzi sahihi , Elimu ya Tanzania karibia ngazi zote ni kukariri tu wakati mwingine kusomeshwa vitu visivyokunufaisha.

Hiyo la vifaa duni ni aibu sana , mambo ya practical mtu unafundishwa theoretically Mwalimu anakuwa kama anasimulia muvi "Sodium ikiCombine na Nini inazalisha Fulani yenye Sifa Fulani"
Tusome
Tupate kazi
Tupate ajira
Tupate hela
Tupate pesa
Tupate mkwanja
Tupate maokoto
Tujenge majumba
Tujenge mahekalu
Tununue mashamba
Tumiliki vyombo vya moto
Tupate familia
Tulishe familia

Ndio lengo hayo mengine kamuulize Bibi yako wa enzi za Mwalimu nini maana ya Elimu atakupa jibu
 
We mzee kwenye ule mgomo wa kina Samuel sitta wa siagi na maziwa na we ulikua mmoja wao hapo jalalani.
Me niliingia miaka 3 baadaye hali ikiwa shwari 🤗

Ila maisha ya Shule miaka ile yalikuwa mazuri kuliko sasa ambapo Wanafunzi wanapewa boom lakini baada ya muda hata hela ya chakula wanakosa
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo bora Tanzania. Kiko mbali mno kwa ubora kulinganisha na vyuo vingine. Kikubwa zaidi ni kuwa wanaodahiliwa Mlimani ni vipanga watupu. Bila Div One & Two ni ngumu mno kuwa mwanafunzi wa UDSM. Ni ndoto ya watanzania wengi kusoma pale. Hata mimi ilikuwa ndoto yangu kusoma pale ila haikuwezekana. Nitaeleza kwanini.

Kwa upande wangu nilishindwa kujiunga na UDSM kwa sababu kwenye maombi yangu sikuambatanisha baadhi ya vitu hivyo maombi yangu kutofanyiwa kazi. Nakumbuka siku chache kabla ya Marticulation exam pale Arusha Tech ndo nilipokea majibu kuhusu makosa niliyofanya wakati wa kutuma maombi. Ikabidi nikajiunge na chuo kingine ambacho bado hawakuwa wamefika deadline ya kutuma maombi.

Je, wewe kwanini ulishindwa kusoma UDSM undergraduate?
Nilisoma PCB nikafaulu vizuri sikua na option nyingine zaidi ya kwenda MUHAS
 
Back
Top Bottom