Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Nilicho kuja kugundua yaan ili uwe Bora Zaidi ni wewe mwenyewe kua Bora Zaid na zaidi.

Nidhamu, kujituma,kufanya kazi kwa bidii bila kusahau kumtanguliza mwenyezi Mungu.

Hili Hali husiani na chuo maana course yoyote mfano law inasomwa miaka mi 4 SAUT WAKATI mzumbe,udsm, udom, Tumain ni miaka mi 3 na masomo ni Yale Yale.
UDSM hauwez kusoma law kwa miska 3. Ni kuanzia miaka minne. Na ili upate NAFASI ya kusoma law udsm lazma uwe na angalau dvsn 1-7. Ya kidato Cha sita.
 
Ila VETA pia nimeenda na imeniokoa sana.

Wasomi nendeni pia VETA.
Mie nilienda VETA, kwenye mtihani wa BASIC DRIVING nikaongoza darasan! You know 😂

IMG_20250320_154859.jpg

​
TICHA akaenda kuangalia matokeo ya sekondari, akakuta ni NUMBER ONE 1️⃣! Yeah, You Know 🙏🏾
 
Inategemea unataka kusoma nin,
Kwa watu wa Afya, UDSM huwa hatuiwazi kabisa 🤣 tunawaza Muhas na UDOM tu,

So usiwaze kila mtu mwenye akili anaenda Udsm, huko kwa wanaosomea siasa na vitu vya ajabu ajabu kama mazingira na international relations 🤣🤣
Wewe ni uko Outdated sana UDSM toka 2015 wanatoa MD na kwasasa wana DDS hata hiyo MUHAS ilikuwa UDSM, Pia kwa Afya UDOM bado bado ni vile tu unafuu wa Ada CUHAS&KCMCU ni far better kuliko hapo
 
While my daughter was attending JKT nilimwombea chuo. Sikupenda UDSM kutokana na life style ya pale, though her pass was good enough.

Niliomba chuo kingine.
Ulikuwa sahihi kile Chuo kama huna ndonga ya kutoenda na Usasa na Mambo ya mjini mjini unapotea
 
While my daughter was attending JKT nilimwombea chuo. Sikupenda UDSM kutokana na life style ya pale, though her pass was good enough.

Niliomba chuo kingine.
Ulikuwa sahihi kile Chuo kama huna ndonga ya kutoenda na Usasa na Mambo ya mjini mjini unapo
ila alichosema ni kweli,

kozi ambazo ni dili kwa udsm ni chache sana , ambazo zinapatikana COET, CONAS na UDBS na MBEYA kule college of health ya udsm. nje ya hapo unaenda kupoteza muda tu.

ukweli ni kwamba hakuna sababu ya kwenda udsm kama unaenda kusoma kozi tofauti na za hizo college
Sio UDSM pengine ni Nchi nzima sasa wenzetu Makerere wameona hilo baadhi ya Programmes zisizo na maana wamefuta Mtu unasoma BA in history yanini, sijui BA in Philosophy wakat akina Aristotle washapotea sijui huko karne ya 5
 
Sasa wangesomea wapi na chuo kilikuwa ni hicho tu mkuu. Ni sawa na kusema muhimbili imefanya pasuaji za kibingwa nyingi kuliko hospitali yoyote wakati pengine yanyewe ilikuwa ikitegemewa kwa jukumu hilo..

Sijawahi kuelewa utukufu wa UDSM unatoka wapi unless mtu awe ni mwanamkoa mwenzetu ambaye ndoto ya kufika mjini dar isingefanikiwa bila kupitia UDSM
Hizi waga ni hoja wa kipimbi sana et Majizi wote wametokea hapo ulitaka wasome wapi!? Na wasichokijua utakuta kuanzia VC, maDVC sijui Dean Principal wa hivyo vyuo ni zao la UDSM hapo ndio nachooa kabisa
 
Inategemea unataka kusoma nin,
Kwa watu wa Afya, UDSM huwa hatuiwazi kabisa 🤣 tunawaza Muhas na UDOM tu,

So usiwaze kila mtu mwenye akili anaenda Udsm, huko kwa wanaosomea siasa na vitu vya ajabu ajabu kama mazingira na international relations 🤣🤣
Wewe kijana mdogo.
Wakati huo mitihani ya matriculation kujiunga UDSM inafanyika ya lazima, hiyo MUHAS bado ilikuwa ni sehemu au chini ya UDSM.
Ilikuwa hivyo kwa Ardhi University ikiitwa UCLAS, nadhani na SUA. Zipo taasisi zingine kibao zimetoka ubavuni mwa UDSM.
Ukisikia UDSM kiheshimu hicho chuo kikuu hutapungukiwa na kitu kama mleta mada alivyo kiheshimu ingawa alikosa nafasi.

Alumni wa MUHAS na vingine Tanzania kuitukana UDSM sawa sawa na Alumni wa UDSM kuitukana Makerere University wakati UDSM ilizaliwa ubavuni mwa hicho chuo.
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo bora Tanzania. Kiko mbali mno kwa ubora kulinganisha na vyuo vingine. Kikubwa zaidi ni kuwa wanaodahiliwa Mlimani ni vipanga watupu. Bila Div One & Two ni ngumu mno kuwa mwanafunzi wa UDSM. Ni ndoto ya watanzania wengi kusoma pale. Hata mimi ilikuwa ndoto yangu kusoma pale ila haikuwezekana. Nitaeleza kwanini.

Kwa upande wangu nilishindwa kujiunga na UDSM kwa sababu kwenye maombi yangu sikuambatanisha baadhi ya vitu hivyo maombi yangu kutofanyiwa kazi. Nakumbuka siku chache kabla ya Marticulation exam pale Arusha Tech ndo nilipokea majibu kuhusu makosa niliyofanya wakati wa kutuma maombi. Ikabidi nikajiunge na chuo kingine ambacho bado hawakuwa wamefika deadline ya kutuma maombi.

Je, wewe kwanini ulishindwa kusoma UDSM undergraduate?
Mimi nilichaguliwa kusoma pale Iła nilikacha baada ya kupata offer ya kwenda kusoma nje ya nchi kwani elimu ya kukariri tu bila reasoning sikuitaka.
 
Sijui kwanini wahitimu wa vyuo vingine wanababaika sana wakisikia mtu amesoma Udsm tokea mwanzo mwa uzi ni udsm udsm udsm ,huwezi kusikia mtu anaattack nit, ardhi au mzumbe.
Wakati wa nyuma tulipokuwa tukifanya selection za vyuo tulikuwa tunajaza nafasi 5 kuanzia unayopenda zaidi 1st choice hadi 5th UDSM niliweka 3rd nikachaguliwa kwa kweli hakuna maajabu yoyote kama watu ambao hawajapita hapo wanavyo babaika.
Napo fanyia kazi na washikaji zaidi ya 30 kutoka DIT kwa kweli jamaa wako vizuri sana tofauti na vyuo vingine wanajua mambo mengi sana.
 
UDSM hauwez kusoma law kwa miska 3. Ni kuanzia miaka minne. Na ili upate NAFASI ya kusoma law udsm lazma uwe na angalau dvsn 1-7. Ya kidato Cha sita.
Hiyo ya miaka mnne unasimuliwa? Mengine yote ni kweli Ila iyo ya law eti udsm miaka minne ileteee ushahidi??
 
Back
Top Bottom