Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Kwa kuchelewa kaka ,ila kuna mwamba alitokea hiyo shule alikua anasema miaka ya nyuma ilikua ya wa asia tupu, au alikua anatusokota?😁😄
Hiyo shule ni ya Aga Khan, walikuwa wanasoma hapo waasia kina Isa Shivji wamesoma shule hiyo.

Shule yao ya msingi ilikuwa Muhimbili Primary, wakimaliza hapo sekondari ilikuwa Tambaza.

Ila serikali ya Tanzania iliondoa mambo hayo siku nyingi tu, hata majina yalibadilishwa, wakati sisi tunaingia hapo ilikuwa shule ya wote.
 
Hiyo shule ni ya Aga Khan, walikuwa wanasoma hapo waasia kina Isa Shivji wamesoma shule hiyo.

Shule yao ya msingi ikikuwa Muhimbiki Primary, wakimaliza hapo sekondari ilikuwa Tambaza.

Ila serikali ya Tanzania iliondoa mambo hayo siku nyingi tu, wakati sisi tunaingia hapo ilikuwa shule ya wote.
Umenielewesha vizuri mkuu ,mimi nilikuwa same boys😆
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni chuo bora Tanzania. Kiko mbali mno kwa ubora kulinganisha na vyuo vingine. Kikubwa zaidi ni kuwa wanaodahiliwa Mlimani ni vipanga watupu. Bila Div One & Two ni ngumu mno kuwa mwanafunzi wa UDSM. Ni ndoto ya watanzania wengi kusoma pale. Hata mimi ilikuwa ndoto yangu kusoma pale ila haikuwezekana. Nitaeleza kwanini.

Kwa upande wangu nilishindwa kujiunga na UDSM kwa sababu kwenye maombi yangu sikuambatanisha baadhi ya vitu hivyo maombi yangu kutofanyiwa kazi. Nakumbuka siku chache kabla ya Marticulation exam pale Arusha Tech ndo nilipokea majibu kuhusu makosa niliyofanya wakati wa kutuma maombi. Ikabidi nikajiunge na chuo kingine ambacho bado hawakuwa wamefika deadline ya kutuma maombi.

Je, wewe kwanini ulishindwa kusoma UDSM undergraduate?
We ni poyoyo tu sasa km hujasoma UDSM unajuaje ubora wake. Tuulize tuliosoma kule, ni pa kawaida sana na walimu hawafundishi kivile tena wengine ndio wavivu kabisa. UD ni jina zaidi kuliko uhalisia
 
Inategemea unataka kusoma nin,
Kwa watu wa Afya, UDSM huwa hatuiwazi kabisa 🤣 tunawaza Muhas na UDOM tu,

So usiwaze kila mtu mwenye akili anaenda Udsm, huko kwa wanaosomea siasa na vitu vya ajabu ajabu kama mazingira na international relations 🤣🤣
Kwanza UD hakuna mambo ya Afya, hiyo MUHAS ndiyo ilikuwa sehemu ya UD iliyokuwa inahusika na mambo ya utabibu
 
Inategemea unataka kusoma nin,
Kwa watu wa Afya, UDSM huwa hatuiwazi kabisa 🤣 tunawaza Muhas na UDOM tu,

So usiwaze kila mtu mwenye akili anaenda Udsm, huko kwa wanaosomea siasa na vitu vya ajabu ajabu kama mazingira na international relations 🤣🤣
Hiyo afya unayojinasibu nayo imezaliwa UDSM. MUHAS, UCLAS/ARU, DUCE,MUCE,Nk hao wote ni watoto wa UDSM. Engineers unaowajua wewe nchi hii majority wamesoma hapo UDSM.

Apparently kozi za afya, agriculture, ualimu nk zimerudi UDSM.

Ni denial tu, ukilaza wako na wivu ndiyo vitakufanya usikubali kwamba UDSM ndiyo the best university siyo Tanzania tu bali kwenye ukanda huu wote wa EA.
 
Binafsi Mimi nililetwa dar na chuo
Nilipiga one. But that doesn't mean much.

Ila tulishaanza kuondoka Tanzania. Dada yangu mdogo hata sekondari (O Level) hakusoma Tanzania alisona Uingereza.

Tanzania shule hazina walimu, hazina vifaa, matatizo kibao, divisions zake, hususan za miaka hiyo, hazina maana.

Unaona vijana siku hizi wanapata one kama zinagawiwa kwa sadaka.
Mimi ile shule ya mkoani Tena wilayani nili faulu kwa Ile division na kwenda shule ya vipaji haikua bahati mbaya..
 
Binafsi Mimi nililetwa dar na chuo

Mimi ile shule ya mkoani Tena wilayani nili faulu kwa Ile division na kwenda shule ya vipaji haikua bahati mbaya..
Hongera zako.

Mimi Dar kwetu tangu siku za kabla ya Mjerumani kuja.

Baba yake bibi yangu kajenga kanisa hapo Azania Front, wamemaliza kujenga mwaka 1903.

Niliona nishaupita kimo mji nikaamua kwenda Dar ya dunia. New York City.
 
Leo nime tembea kwa miguu umbali mrefu kariakoo nimegundua sisi sa bongo uwezo mdogo Sanaa akili hata Kumbukumbu
 
Back
Top Bottom