Kitu gani kinazorotesha kasi ya maendeleo yako?

Kitu gani kinazorotesha kasi ya maendeleo yako?

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Habari za asubuhi watu wa Mungu nyie siyo watu wangu 😎 😎

Leo nimewaza sana kwamba kuna vitu fulani au tabia fulan tunazo maishani zinatufanya tutumie hela rafu na kujikuta mwaka unaisha maisha yako yapo kama ya mwaka uliopita. Kuna baadhi ya mambo yanapelekea tunatumia fedha kidogo tunazopata kuyafanya na kujikuta hatusogei kabisa kimaisha.

Sitoi lecture namna ya kutumia pesa zako. Kwa mimi ntataja baadhi ya vitu vinavyomaliza pesa zangu.

1.0 Gari
Haka kagari yaani kanakula sana sehemu kubwa ya fedha zangu ambazo kananisaidia kuzipata yaani tunaenda paso kwa paso
mafuta, service, urembo( Kila kinachopendezesha gari nikikiona lazima nikitafute kwa gharama yoyote, Sport Rims, Profile tyres, Android radio NK.

2.0 Gambe
Yaani nikipata pesa ambayo haikuwa kwenye official mishe zangu lazima niitie kiberiti naweza kupata 70k mchana ikifika usiku nina 10k.

3.0 Wanawake
Kuna kipindi nilikuwa na mahusiano na wanawake wa4 aisee, yaani ni kama wana majini siku nikipata hela tu ndio siku hiyo nakumbukwa na kila mmoja, nikipigwa mizinga ya 20k tu na kila mmoja 80k inadondoka nkaachana na watatu amebaki mmoja tu mtarajiwa😎

Ukipata demu mpya lazima utumie zaidi ya ulichopanga yaani kukutana na demu mara moja tu matumizi hayapungui 70+
(sipeleki demu kwangu so lodge inahusika + vinywaji+chakula na posho+ usafiri). Siku hizi hawanipi shida sana kwa kuwa naweza kuchepuka mara moja tu ndani wiki6 saivi mi sio mtumwa saaaana wa sex haya nimemwachia Zero IQ.

4. Bando
Haka kaeneo nako kanachangia sana maana siwezi kutokuwepo hewani maana internet pia kwa sehemu flani inaendesha maisha yangu nje ya ajira.

Kuna mengine mengi ila kwa leo haya yanatosha kuyafanya maisha yangu kutosogea kwa kasi ninayoipanga.

Hebu tutajie nini kinarozotesha kasi ya maendeleo yako?
 
Habari za asubuhi watu wa Mungu nyie siyo watu wangu 😎 😎

Leo nimewaza sana kwamba kuna vitu fulani au tabia fulan tunazo maishani zinatufanya tutumie hela rafu na kujikuta mwaka unaisha maisha yako
Katika hayo mambo nina full control na yote isipokuwa bundle tu😂 siwezi kaa bila internet hata nusu saa! Nitakufa 😂😂😂
 
Sasa hapo namba 4 Bando linakulaje man. Au una smart house, Smart TV etc maana kama simu tu halizidi elfu 50 kwa mwezi.

Mi gari aisee. Ngoja nikae kimya tu.
Smart tv ipo ndomana nalalamika, Andoid car radio vinakula sana bando
 
Gari siwezi sema inakula pesa coz naona inanisaidia sana, ila gambe daah [emoji119][emoji119][emoji119]
Garama za six cylinder kutoka Kwa Komba hadi Kivukoni sio mchezo mkuu, nataka kutafuka ka-I10

imgres.jpg
 
Back
Top Bottom