Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Bac then kama Kuna uwezekano wa Mimi kuelezea tukio na lika make sense kwamba sio kurogwa. It means uchawi haupo..ni kwamba tu we umeshindwa kuelewa tukio Hilo ukaita uchawi kisa uvivu
Mkuu hatuiti uchawi kwa sababu ya uvivu bali tunaona watu wanatibiwa na kupona huo uchawi ambapo wewe unadai wanabahatisha.
 
Mwaka jana nimelala katika nyumba moja na familia tangu na mwenzangu na familia yake tukaibiwa TV MBILI yani yakwangu na ya kwake jamaa yangu pasipo kuvunjwa ama kufunguliwa milango yetu ya nyumba na huo wezi ulishamili mahali nilipo mpaka leo
 
😂😂😂Unanipa black n white fallacy..unataka nikujibu Nini..we umejiridhisha vipi kwamba Thor wa ukweli mpiga radi hayupo?
Afrika watu wana wanajihusisha na uchawi kivitendo hivyo ni rahisi mtu kuweza kujiridhisha kama uchawi ni kweli ama si kweli, ila wewe haufanyi hivyo upo JF unataka watu wakupe evidence na wasipofanya hivyo unahitimisha hakuna uchawi.

Hivyo ni ajabu kuja kulinganisha uchawi na habari za Thor.
 
Ndivyo hallucinations ilivyo.

Rafiki yangu alipoteza mama yake mzazi, nilienda kulala kwake kama kumfariji kama week mbili baadae baada ya kifo cha mama yake.

Nakumbuka tupo tuna watch WWE kwenye Tv akasimama gafla anaongea Mama halafu yupo anatabasamu huku anafuata uelekeo wa kutoka nje.

Ikabidi nimshtue anaendelea kuita mama mpaka anafika nje ya geti ndo namshika kwa nguvu ananiambia kapotea alikuwepo hapa na kilio juu.

Yupo mama mitaa ya ukonga mombasa, kapoteza mtoto wake wa kiume, yule jamaa alikuwa anauza genge barabarani huyu mama mpaka sasa anaweza akatoka kwake akasimama upande wa pili wa barabara anaita jina la mwanae ile sehemu ambapo genge lipo na mpaka sasa lipo. Anamwita jina lake halafu anamwambia mwanangu niletee machungwa. Na mtoto alishafariki miezi3 inakaribia.

Hiyo ni mifano michache hakuna uchawi hapo.
Nenda soma serer mythology za senegal na gambia.
Kwahiyo nguvu za giza hakuna ndugu basi hata nguvu za kiroho zisingekuwepo ebu nifundishe nielewe
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Sa hayo mapepo (nguvu za Giza)
Wanamtibu nn?
Apelekwe kwenye maombi,Ngoma hiyo inapigwa anarudishiwa aliyefanya huo ushenzi
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Kweli uchawi upo.

Kijiji fulani huko mikoa ya nyanda za juu Kusini. Ni msimu wa uchaguzi. Kampeni kila siku kila mahali. Mshikemshike narudisha kadi nahamia upinzani mara narudisha kadi nahamia CCM.

Siku hiyo ni zamu ya upinzani kwenye moja ya vitongoji hapo kijijini. Mwenyekiti wa kitongoji ni CCM pure. Akawaambia CHADEMA kuwa sitaki upinzani kwenye kitongoji changu. Wakampuuza wakafunga mziki mnene wakitumia jenereta.

Matangazo yakaendelea, kelele mtindo mmoja.

Mara wingu hafifu angani. Hakuna aliyehofu maanake ni katikati ya kiangazi. Hakuna hata dalili ya manyunyu.Burudani kwa kwenda mbele.

Ghafla ilishuka radi kavu, ilikula kuanzia jenereta, spika, hadi mic zote.

Usiniulize kilichofuata. Ninashukuru Mungu hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Hizi ni hadithi mnadanganyana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mkiwa na ndugu yenu anaonekana kuwa kama chizi na mkatibu hospitali wapi, peleka kwenye maombi kila unapopasikia wapi hapo unafanyaje?
Yaani inaposema kwenye maombi manaake Mungu,sa Mungu hawezi shindwa!
Either huyo mtumishi level yake ndogo...
Yes maana spiritual iwe Nuru su Giza Kuna 3 level.....Deep, deeper and deepest.....
Ss km mwenye shida(nguvu za Giza) Yuko level ya juu kwenye Nuru Yuko chini hawezi kumsaidia....
Ndo maana hata watumishi wanatofautiana nguvu .....
Though sbb za kutofautiana nguvu pia zipo nyingi...

Kingine roho ya maarifa
Macho ya rohoni ,kuona na kutambua chanzo Cha tatizo na namna ya kuliondoa tatizo....
 
Kwani ukiwa kanisani huwa mnakemea NGUVU za Giza au hamkemei?
😂😂😂Hujajibu swali. Sisi kanisa letu halikemei ujinga ambao haupo. Mi nasema kuwa na Mungu, kuwa na muumbaji wa mbingu na nchi, Inahusiana Nini na uchawi kuwepo.
 
Nimeleta hoja ya waganga kutibu na kutatua shida za watu katika masuala ya kichawi ila umeishia kusema wanabahatisha na ukashindwa kueleza kivipi.

Nikakuuliza kwanini hallucinations ziwatokee sana watu maeneo maalumu kama barabarani wakati wanaendesha magari,baharini hasa wavuvi na baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kutokea mauzauza? Ila umeishia kutoa majibu na kusema we sio doctor.
Tena kuna hadi visa za nyumba watu kushindwa kuishi kutokana kuwa na mauzauza.

Ila wewe unaishia kuleta mifano yako ya kuona jua.
😂😂😂Ndio...coz kitu ambacho ni real haliwezi kuchagua watu sijui mipaka. We Kama una hao waganga waambie wayarushe..ni mwezi mzima Sasa...tusitishane utoto bana nachoka na Mimi mjue
 
Mkuu hatuiti uchawi kwa sababu ya uvivu bali tunaona watu wanatibiwa na kupona huo uchawi ambapo wewe unadai wanabahatisha.
Je..hao watu wanaweza kutibiwa na kupona bila huo uchawi? If yes...then uchawi haupo..ni kwamba mtu kapona naturally
 
Mwaka jana nimelala katika nyumba moja na familia tangu na mwenzangu na familia yake tukaibiwa TV MBILI yani yakwangu na ya kwake jamaa yangu pasipo kuvunjwa ama kufunguliwa milango yetu ya nyumba na huo wezi ulishamili mahali nilipo mpaka leo
😂Duu...haya bana story nzuri
 
Afrika watu wana wanajihusisha na uchawi kivitendo hivyo ni rahisi mtu kuweza kujiridhisha kama uchawi ni kweli ama si kweli, ila wewe haufanyi hivyo upo JF unataka watu wakupe evidence na wasipofanya hivyo unahitimisha hakuna uchawi.

Hivyo ni ajabu kuja kulinganisha uchawi na habari za Thor.
😂😂😂Kuna tofauti gani...Thor ni Mungu Kama unavyoamini Allah na Yahweh na Kuna jamii ziliamini Thor ni Mungu na ana nguvu na yupo ndo anasababisha radi. Ila hizo jamii zilivyojua radi ni kitu natural Wakaelimika saa hivi Thor ni movie tu. Sasa wewe muafrika unataka babu yako aliamini kitu na wewe uamini .ndo maana huendelei
 
Back
Top Bottom