Uchawi sio story dogo nimekwambia uchawi unafanyika kwa vitendo na mfano mfano mmoja wapo ni waganga ambako wanashughulika na masuala ya kichawi kitu ambacho wewe unasema wana bahatisha. Sasa utasemaje tena kuwa uchawi ni story tu za vijijini?
Ni ajabu kuhitimisha kuwa hakuna uchawi kisa mie sijakupa ushahidi, habari za uchawi sio za juzi wala jana ila cha kushangaza watu kama nyie huwa hamtaki kujiridhisha wenyewe ukweli wa huo uchawi ila mnaishia kudai kupewa uthibitisho tu, kama uchawi ni story za kijijini we lini ulienda huko kijijini ukajiridhisha kuwa hakuna ukweli kwenye uchawi ni imani tu haina athari kiuhalisia?