Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kweli uchawi upo.

Kijiji fulani huko mikoa ya nyanda za juu Kusini. Ni msimu wa uchaguzi. Kampeni kila siku kila mahali. Mshikemshike narudisha kadi nahamia upinzani mara narudisha kadi nahamia CCM.

Siku hiyo ni zamu ya upinzani kwenye moja ya vitongoji hapo kijijini. Mwenyekiti wa kitongoji ni CCM pure. Akawaambia CHADEMA kuwa sitaki upinzani kwenye kitongoji changu. Wakampuuza wakafunga mziki mnene wakitumia jenereta.

Matangazo yakaendelea, kelele mtindo mmoja.

Mara wingu hafifu angani. Hakuna aliyehofu maanake ni katikati ya kiangazi. Hakuna hata dalili ya manyunyu.Burudani kwa kwenda mbele.

Ghafla ilishuka radi kavu, ilikula kuanzia jenereta, spika, hadi mic zote.

Usiniulize kilichofuata. Ninashukuru Mungu hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
😂😂😂Waambie walete dar bac au kisa kila mtu anajielewa
 
Yaani inaposema kwenye maombi manaake Mungu,sa Mungu hawezi shindwa!
Either huyo mtumishi level yake ndogo...
Yes maana spiritual iwe Nuru su Giza Kuna 3 level.....Deep, deeper and deepest.....
Ss km mwenye shida(nguvu za Giza) Yuko level ya juu kwenye Nuru Yuko chini hawezi kumsaidia....
Ndo maana hata watumishi wanatofautiana nguvu .....
Though sbb za kutofautiana nguvu pia zipo nyingi...

Kingine roho ya maarifa
Macho ya rohoni ,kuona na kutambua chanzo Cha tatizo na namna ya kuliondoa tatizo....
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂Duuu ..kweli Tanzania tutachelewa Sana kufika
 
😂😂😂Ndio...coz kitu ambacho ni real haliwezi kuchagua watu sijui mipaka. We Kama una hao waganga waambie wayarushe..ni mwezi mzima Sasa...tusitishane utoto bana nachoka na Mimi mjue
Hapa hoja sio kurusha majini wala kurogana hatukuwa tukibishana kwamba naweza kukuroga au siwezi, hata mimi ninayeamini uchawi naweza kusema hakuna anayeweza kuniroga wala kunitupia jini.

Mpaka sasa wewe unayedai hakuna uchawi ni kukosa tu uelewa umeshindwa kutetea hoja yako na imeonyesha wazi hujawahi kutafuta ukweli kuhusu kama ni kweli ama si kweli.
 
We skia...tusipotezane mda kuongea story za Babu yake nani Kijiji fulani ambae huyo Babu hata kuandika hajui.. tuwe serious na maisha halisi sawa
Mimi nakuelezea maisha halisi ambayo watu tunaishi huku, wewe ndio unatuletea maisha ya wazungu jinsi wanavyoishi huko ambayo sio maisha ya afrika ndio maana hauna mifano halisi ya kinachoendelea afrika katika huko kupinga kwako uchawi.

Wewe endelea kuangalia movie zako za Thor hapo kwa mjomba wako tu.
 
😂😂😂Kuna tofauti gani...Thor ni Mungu Kama unavyoamini Allah na Yahweh na Kuna jamii ziliamini Thor ni Mungu na ana nguvu na yupo ndo anasababisha radi. Ila hizo jamii zilivyojua radi ni kitu natural Wakaelimika saa hivi Thor ni movie tu. Sasa wewe muafrika unataka babu yako aliamini kitu na wewe uamini .ndo maana huendelei
Mkuu issue sio kuamini walichoamini mababu bali uhalisia wa kitu chenyewe, nimeeleza kuwa uchawi afrika unaaminiwa na kufanyika kwa vitendo na athari zake zinatokea ila wewe uliyekariri wanasayansi huko wanaopinga uchawi ndio unasema athari za uchawi ni za kubahatisha.
 
😂😂😂Sawa bac walete wachawi huku tuwaone hata Mimi naweza toa shuhuda za uwongo
Watu wakieleza visa vyao unasema mara vya kutunga mara hallucinations, yani kupinga hivyo unavyopinga wewe ni kitu rahisi sana hadi sasa sijaona huo ulewa na elimu uliyokuwa.

Hivi kwa mtu ambaye anafuatilia haya majadiliano yetu na hayupo upande wowote kati yetu unadhani hoja ipi atashika kutoka kwako?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Hujajibu swali. Sisi kanisa letu halikemei ujinga ambao haupo. Mi nasema kuwa na Mungu, kuwa na muumbaji wa mbingu na nchi, Inahusiana Nini na uchawi kuwepo.
Ila huwa mnakemea kitu gani?
 
Hapa hoja sio kurusha majini wala kurogana hatukuwa tukibishana kwamba naweza kukuroga au siwezi, hata mimi ninayeamini uchawi naweza kusema hakuna anayeweza kuniroga wala kunitupia jini.

Mpaka sasa wewe unayedai hakuna uchawi ni kukosa tu uelewa umeshindwa kutetea hoja yako na imeonyesha wazi hujawahi kutafuta ukweli kuhusu kama ni kweli ama si kweli.
Bac ...Kama upo leta uthibitisho...mbona mnazunguka.
 
Mimi nakuelezea maisha halisi ambayo watu tunaishi huku, wewe ndio unatuletea maisha ya wazungu jinsi wanavyoishi huko ambayo sio maisha ya afrika ndio maana hauna mifano halisi ya kinachoendelea afrika katika huko kupinga kwako uchawi.

Wewe endelea kuangalia movie zako za Thor hapo kwa mjomba wako tu.
😂😂😂😂😂😂😂😂Dogo....huyo mjomba mbona unamkazania. So Africa uchawi upo..bac tuonyeshe. Nimekuambia siku hizi mpaka ajali barabarani zinarekodiwa Kuna majengo Yana camera watu Wana Simu...Ila uchawi unachagua kijijini ambapo hamna camera ili watu watunge story
 
Mkuu issue sio kuamini walichoamini mababu bali uhalisia wa kitu chenyewe, nimeeleza kuwa uchawi afrika unaaminiwa na kufanyika kwa vitendo na athari zake zinatokea ila wewe uliyekariri wanasayansi huko wanaopinga uchawi ndio unasema athari za uchawi ni za kubahatisha.
Sayansi haikaririwi Ina badilika. Ndo maana mwanzo hakukuwa na chanjo ya corona baadae zikapatikana...ndo Sayansi. Sayansi inaendeleza jamii uchawi ni ujinga tu na umaskini
 
Watu wakieleza visa vyao unasema mara vya kutunga mara hallucinations, yani kupinga hivyo unavyopinga wewe ni kitu rahisi sana hadi sasa sijaona huo ulewa na elimu uliyokuwa.

Hivi kwa mtu ambaye anafuatilia haya majadiliano yetu na hayupo upande wowote kati yetu unadhani hoja ipi atashika kutoka kwako?
Kwamba ni hallucinations na mifano ipo...Kama issue Ni watu wengi..unataka uniambie jua Lilichezacheza kule Fatima Portugal...no...watu 3000 wanaweza kuona kitu ambacho hakipo..it's possible 😂so bado hamna hoja
 
Bac ...Kama upo leta uthibitisho...mbona mnazunguka.
Nilete uthibitisho upi sasa? Waganga wenye kutibu matatizo ya kichawi umesema ni kubahatisha tu halafu unakuja hapa unataka uthibitisho sasa sijui uthibitisho upi? Yani kama tunajadili suala la kufikirika wakati muda wote nimesema hapa kuwa uchawi unafanyika kivitendo.

Sioni huo uelewa wala kuelimika kwako naona ubishi tu.

Dogo mchana mwema.
 
Back
Top Bottom